Mfahamu Box Jelly fish, Samaki mwenye sumu kali kuliko kiumbe chochote duniani!

Sidhani kama atakua na sumu mwili mzima,kuna Samaki fulani ana sumu kali na anafaida kiafya mwilini lakini hutengenezwa na Certified or approved chef only, watu wa Asia wanamla ila ni ghali sana, sasa sijui ndio huyu anayeongelewa hapa?

Wanaliwa na kasa mkuu transcend
 
Nashukuru kwa somp jipya. Ila naomba uniongezee hapo namba yake ya kuua. Mf koboko anatema mate na kugonga pia.
 
Huyo Nyegere ndo kiumbe gani Mkuu? Naomba uweke hapa uzi wake kama hutojari
1468091803386.jpg
 
....pia kuna familia ya hii samaki nilikua nakutana nao velani mtwara enzi naogelea.ukimgusa anapiga shoti kama ya umeme ule wa baskeli.!!!
 
Mkuu, kutana kwanza na huyo papa kwenye anga zake ndio useme hivyo. Kwanza papa hana haja ya kukuuma maana hizo neva zitafeli kabla hata hajakusemesha

hahahahahahaha, na kiashiria kikubwa wenzako watakachokiona huku juu ya maji ni mapovu ya mashuzi utakayokuwa unayatoa ukiwa chini ya maji face to face na mzee papa
 
View attachment 348750

View attachment 348753

Nawasalimia wakuu wangu,

Nataka tumjadili samaki aina ya Box Jelly fish (Sea wasp), ni samaki anaepatikana baharini,hasa katika bahari ya Pacific (Indo-Pacific) pia katika bahari ya Atlantic.Hupatikana kwa wingi katika nchi za Australia,New Zealand,Philippenes na mji wa Hawaii ulioko USA.

Samaki huyu hujulikana kama 'the most deadliest fish in the world', 'the world most venomous creature', na 'the most notoriously dangerous specie in the world' yaani kiumbe hatari kuliko vyote duniani,yote hii katika kumsifia kutokana na uwezo wake wa kuua kwa sumu kali na kwa haraka kuliko kiumbe chochote duniani. Box Jelly fish ukubwa wake unakuwa na urefu wa cm 20, na 'miguu' yake inakuwa na urefu wa kufikia mita 3, na ana uzito wa kg 2.Ana jumla ya macho 24,ambayo huwa yamekaa yamekusanyika sita na yakiwa katika kona nne za mwili wake.Wanaishi muda wa mwaka mmoja tu toka wazaliwe.

Ukimuangalia kwa umbo unaweza kusema ni kiumbe kidhaifu na hata cha kufuga ili uchezee,maana yupo kama maua.Kwa wale walioangalia movie ya Seven Pound ya Willy Smith watakuwa wamemuona pale mwishoni.

Kwa viumbe wa ardhini na majini tunaweza kupima ukali wake wa kuua kwa sumu kwa kuangalia vigezo viwili
(a) Sumu yake anayotoa kwa kipimo cha ounce (ounce 1=28.3 grams),kina uwezo wa kuua watu wangapi?
(b) Hiyo sumu inaweza kuchukua muda gani kuua mtu?

Kwa kutumia vigezo hivyo hapo juu, utaona kuwa Box Jelly fish anawazidi kwa mbali viumbe vingine wote wa baharini na nchi kavu kwa kuwa na sumu kali yenye kuweza kuua watu wengi na kwa haraka.Box Jelly fish anaweza kuua kwa kipimo cha ounce moja ya sumu yake kuua watu 60 kwa mpigo! Na hao watu kwa sumu hiyo lazima wafe chini ya dakika 3 tu!Hapa utaona hata yule nyoka tunayemuogopa zaidi duniani ambae ni Black Mamba au maarufu kwa jina la Koboko..Hafui dafu hata kidogo kwa samaki huyu.

Black mamba akimuuma binadamu itamchukua mtu masaa 7 hadi 15 kufa,wakati samaki huyu ni DAKIKA 3 tu!Sumu yake akikupiga inaenda kwa haraka kushambulia moyo na kuua mifumo ya neva kwa haraka hivyo kukuzimisha fasta! Lkini kama ilivyo kila mbabe ana mbabe wake,samaki huyu hazungushi kwa turtles (kasa),ambao sumu ya jelly fish huyu haimdhuru..akimkuta mahali anamla tu kama hana akili nzuri..kama Nyegere anavyomla cobra.Huyo ndo Box Jelly fish a.k.a marine stinger...

Mkuu black mamba sumu yake ni dakika 25 unakua umekufa msome vizuri black mamba tena
 
Black mamba masaa 7-15?!
Sikubali. Kuna nyoka wengine nusu saa tu nyingi.....na black mamba ndo baba lao kwa ukali wa sumu.
Black mamba anasumu aina mbili akikunganta unachukua dakika 25 lazima uwe umekufa sasa ujamaa na mshangaa
 
Back
Top Bottom