Mfahamu Box Jelly fish, Samaki mwenye sumu kali kuliko kiumbe chochote duniani!

Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
10,351
9,845
box-jellyfish-hawaii.jpg

box-jellyfish-2.jpg

Nawasalimia wakuu wangu,

Nataka tumjadili samaki aina ya Box Jelly fish (Sea wasp), ni samaki anaepatikana baharini,hasa katika bahari ya Pacific (Indo-Pacific) pia katika bahari ya Atlantic.Hupatikana kwa wingi katika nchi za Australia,New Zealand,Philippenes na mji wa Hawaii ulioko USA.

Samaki huyu hujulikana kama 'the most deadliest fish in the world', 'the world most venomous creature', na 'the most notoriously dangerous specie in the world' yaani kiumbe hatari kuliko vyote duniani,yote hii katika kumsifia kutokana na uwezo wake wa kuua kwa sumu kali na kwa haraka kuliko kiumbe chochote duniani. Box Jelly fish ukubwa wake unakuwa na urefu wa cm 20, na 'miguu' yake inakuwa na urefu wa kufikia mita 3, na ana uzito wa kg 2.Ana jumla ya macho 24,ambayo huwa yamekaa yamekusanyika sita na yakiwa katika kona nne za mwili wake.Wanaishi muda wa mwaka mmoja tu toka wazaliwe.

Ukimuangalia kwa umbo unaweza kusema ni kiumbe kidhaifu na hata cha kufuga ili uchezee,maana yupo kama maua.Kwa wale walioangalia movie ya Seven Pound ya Willy Smith watakuwa wamemuona pale mwishoni.

Kwa viumbe wa ardhini na majini tunaweza kupima ukali wake wa kuua kwa sumu kwa kuangalia vigezo viwili
(a) Sumu yake anayotoa kwa kipimo cha ounce (ounce 1=28.3 grams),kina uwezo wa kuua watu wangapi?
(b) Hiyo sumu inaweza kuchukua muda gani kuua mtu?

Kwa kutumia vigezo hivyo hapo juu, utaona kuwa Box Jelly fish anawazidi kwa mbali viumbe vingine wote wa baharini na nchi kavu kwa kuwa na sumu kali yenye kuweza kuua watu wengi na kwa haraka.Box Jelly fish anaweza kuua kwa kipimo cha ounce moja ya sumu yake kuua watu 60 kwa mpigo! Na hao watu kwa sumu hiyo lazima wafe chini ya dakika 3 tu!Hapa utaona hata yule nyoka tunayemuogopa zaidi duniani ambae ni Black Mamba au maarufu kwa jina la Koboko..Hafui dafu hata kidogo kwa samaki huyu.

Black mamba akimuuma binadamu itamchukua mtu masaa 7 hadi 15 kufa,wakati samaki huyu ni DAKIKA 3 tu!Sumu yake akikupiga inaenda kwa haraka kushambulia moyo na kuua mifumo ya neva kwa haraka hivyo kukuzimisha fasta! Lkini kama ilivyo kila mbabe ana mbabe wake,samaki huyu hazungushi kwa turtles (kasa),ambao sumu ya jelly fish huyu haimdhuru..akimkuta mahali anamla tu kama hana akili nzuri..kama Nyegere anavyomla cobra.Huyo ndo Box Jelly fish a.k.a marine stinger...
 
Mkuu sio Kweli kwamba black mamba sumu yake inaweza kukaa mwilini mwa majeruhi kwa masaa hayo 15 kama ulitangulia kusema.
 
Elimu nzur sana mkuu.
Juu ya jelly fish naomba kama unadata za umuhimu wake pia utuletee tuendelee kupata Elimu. Kuna taarifa kwamba huyu samaki ana protein ambayo husaidia kufight aging na mengine mengi tu.
 
View attachment 348750

View attachment 348753

Nawasalimia wakuu wangu,

Nataka tumjadili samaki aina ya Box Jelly fish (Sea wasp), ni samaki anaepatikana baharini,hasa katika bahari ya Pacific (Indo-Pacific) pia katika bahari ya Atlantic.Hupatikana kwa wingi katika nchi za Australia,New Zealand,Philippenes na mji wa Hawaii ulioko USA.

Samaki huyu hujulikana kama 'the most deadliest fish in the world', 'the world most venomous creature', na 'the most notoriously dangerous specie in the world' yaani kiumbe hatari kuliko vyote duniani,yote hii katika kumsifia kutokana na uwezo wake wa kuua kwa sumu kali na kwa haraka kuliko kiumbe chochote duniani. Box Jelly fish ukubwa wake unakuwa na urefu wa cm 20, na 'miguu' yake inakuwa na urefu wa kufikia mita 3, na ana uzito wa kg 2.Ana jumla ya macho 24,ambayo huwa yamekaa yamekusanyika sita na yakiwa katika kona nne za mwili wake.Wanaishi muda wa mwaka mmoja tu toka wazaliwe.

Ukimuangalia kwa umbo unaweza kusema ni kiumbe kidhaifu na hata cha kufuga ili uchezee,maana yupo kama maua.Kwa wale walioangalia movie ya Seven Pound ya Willy Smith watakuwa wamemuona pale mwishoni.

Kwa viumbe wa ardhini na majini tunaweza kupima ukali wake wa kuua kwa sumu kwa kuangalia vigezo viwili
(a) Sumu yake anayotoa kwa kipimo cha ounce (ounce 1=28.3 grams),kina uwezo wa kuua watu wangapi?
(b) Hiyo sumu inaweza kuchukua muda gani kuua mtu?

Kwa kutumia vigezo hivyo hapo juu, utaona kuwa Box Jelly fish anawazidi kwa mbali viumbe vingine wote wa baharini na nchi kavu kwa kuwa na sumu kali yenye kuweza kuua watu wengi na kwa haraka.Box Jelly fish anaweza kuua kwa kipimo cha ounce moja ya sumu yake kuua watu 60 kwa mpigo! Na hao watu kwa sumu hiyo lazima wafe chini ya dakika 3 tu!Hapa utaona hata yule nyoka tunayemuogopa zaidi duniani ambae ni Black Mamba au maarufu kwa jina la Koboko..Hafui dafu hata kidogo kwa samaki huyu.

Black mamba akimuuma binadamu itamchukua mtu masaa 7 hadi 15 kufa,wakati samaki huyu ni DAKIKA 3 tu!Sumu yake akikupiga inaenda kwa haraka kushambulia moyo na kuua mifumo ya neva kwa haraka hivyo kukuzimisha fasta! Lkini kama ilivyo kila mbabe ana mbabe wake,samaki huyu hazungushi kwa turtles (kasa),ambao sumu ya jelly fish huyu haimdhuru..akimkuta mahali anamla tu kama hana akili nzuri..kama Nyegere anavyomla cobra.Huyo ndo Box Jelly fish a.k.a marine stinger...
Kwa ufahamu wangu na chapisho la national geographical channel wana m -consider Stone fish world venomous fish
 
Sidhani kama anastahili nafasi hiyo ya juu,kwasababu hata ukisoma machapisho yake inaonekana 'anaweza kusababisha kifo',na hakuna rekodi zozote za watu kufa kwasababu yake.Wanasema "No death have been recorded in Australia since the European arrival"(Underhill,1987) Na hata hiyo ingekuwepo tungelinganisha ounce ya sumu yake inaweza kuua watu wangapi?Na hiyo sumu yake inaweza kuchukua muda gani mpaka kuua?Sasa ukiangalia hilo nalo unaona mtu akichomwa na miba ya stone fish yenye sumu inaonekana kuwa kama ni mtu mzima atateseka tu na maumivu na hawezi kufa.Wakati ukipigwa kitu na Box Jelly fish kwanza kama upo kwenye maji lazima upate shock na uzame,huwezi fika hata nchi kavu,na ndani ya dakika tatu unakuwa umekufa...Na ukiangalia boxy jellyfish Philippines kati ya watu 20-40 hufa kila mwaka kwa sababu yake.Unaweza kuwa upo right of course lakini kwa vigezo hivyo viwili bado boxy jellyfish ni kiumbe hatari zaidi
 
Back
Top Bottom