Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,850
- 34,300
AfyaYako Mfadhaiko (Depression) wathibitishwa kwa mara ya kwanza kuwa na uhusiano na protini maalumu
Matokeo ya utafiti mpya yaliyotolewa kwenye jarida la taasisi ya sayansi ya
Marekani yanaonesha kuwa watafiti wamegundua kuwa protini ya aina ya FGF9 inahusiana na mfadhaiko.
Watafiti wamegundua kuwa kwenye sehemu muhimu ya ubongo, kiwango cha protini
ya FGF9 ya watu wanaopata mfadhaiko ni juu kuliko cha watu wa kawaida. Utafiti
huo umegundua kuwa ongezeko la protini hiyo mwilini litasababisha mfadhaiko, na
kama mtu akikabiliana na shinikizo, kiwango cha protini hiyo pia kitaongezeka.
Kundi la watafiti limetangaza kuwa wataweza kutafuta dawa mpya ili kudhibiti
protini ya FGF9 kwenye mwili wa watu wanaokabiliwa na mfadhaiko.
Ukiwa na Shida yoyote ile unaweza kunitafuta Kwa mawasiliano Kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano