Meza ya Wandewa

Meza ya Wandewa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
MEZA YA WANDEWA

Juzi Mwl Kalinga Jonas nilikuwa kwenye harusi bhana. Kwanza picha linaanza nimefika pale nimevaa suruali ya Kadeti (mapigo ya Wandewa hayo).

Nikakaa Meza moja na matajiri wa Kigoma

Eeh mi si nakwambia watu wakajua na mimi ni mndewa, ile Meza walikuwa wanaleta mavitu ya bei kubwa me sikujua kumbe nimekaa meza ya wanakamati.

Eeh mi nabugia tu yaaani wanaleta mijuisi ya embe ya South Afrika, juisi imepanda ndege acha na za Azam zinakuja kwa miguu. Supermarket yanauzwa Afu 5 meza zingine wanawapa maji ya jero.

Basi mademu wote macho kwangu mwaaaaaah, nikasema leo KUKU KABEBA MWEWE😁😁 ukikaa na wandewa inabidi uwe na uelewa na siasa na michezo.

Hasa maswala yanayoendelea duniani. Kuhusu kule Parestina na Israel si unajua.

Basi WATU wanabishana pale wengine wanasema ule ugomvi ni kwa maslahi ya Wamarekani, wengine wanasema ni mgongo wa siasa ila wanaisingizia dini.

Wakasema hapa tumekaa na kijana msomi, anaonekana ametoka chuo huyu ngoja tusikilize mawazo yake.

Wakasema eeh kijana unamawazo gani juu ya hili?

Nikasema "NAAAAM"

Hapo mi sielewi hata kama Palestina na Israel wanagombana, nikasema ukisikia kuaibika ndio huku sasa.

Kwanza nikanywa juice kidogo....

Nikasikia mzee mmoja anasema kijana mwenye uelewa juu ya haya mambo lazima anywe juice kidogo kabla hajaongea ili kurekebisha koo kidogo.

Mimi kimoyomoyo nikase kurekebisha koo tena....

Kama Mungu alikuwa upande wangu wakati nashusha juisi ile mara Dj akapiga ule wimbo wa Mondi Eeeh wandewa wanaingia.

Oya nikasimama fast nikaanza kucheza, Dj akasema meza ya kamati amkeni mcheze kidogo aiseeeeeeee nilicheze kwa sifa vibaya mno WATU wanajua nacheza wimbo mzuri kumbe mimi nacheza Mungu kaniokoa kuaibisha ukoo.

Nikasema hapa ngoja nihame meza, nikaanza kutafuta sehemu nyingine yenye meza za kukaa, hamna ukumbi umejaa nikasema LEO MANJU KAMEZA NGOMA.

Nikasimama nyuma ya ukumbi nikawa nacheza cheza, mara mlinzi akanifuata akaniambia muheshimiwa samahani akanishika akanirudisha kwenye meza ya kamati🤣

Kufika pale wakawa wamebadili mada bhana wanaongelea mambo ya kwenda vacationa na familia zao mwisho wa mwaka.

Mwingine anaenda Dubai, mwingine anaenda China wengine Marekani, ikafika zamu yangu kusema nitaenda wapi.

Nikasikia mzee mmoja anasema vijana siku hizi wadogo wanakuwa na pesa sana, sikutegemea kama huyu kijana anaweza kuwa mwanakamati.

Hapo mwana kamati alikuwa anatoa million moja kama mchango.....

Kijasho chembamba kikaanza kunitoka😁😁

Kuna mzee akasema huyu ndio kijana yeye alitoa million mbili, lakini hajaudhuria kikao hata kimoja tuliambiwa alikuwa Italy huko kuweka uwekezaji ndio maana alitoa mchango ila hukuwepo kwenye vikao.

Vipi kijana, uwekezaji nje ya nchi unalipa sana nini mbona vijana wengi mnaenda huko siku hizi?

Kimoyomoyo nikasema kuwekeza nini labda kuwekeza kwenye hili tumbo ndio kitu naweza🤣🤣

Mungu hamuachi mja wake, mara MC akasema mwenye gari Haria nyeusi new model akapaki vizuri hapo nje.

Nikasimama, mara na mzee mmoja hivi ana kipara naye akasimama, akasema kijana na wewe una Haria new model nikajua ninayo mwenyewe kwenye huu mji.

Nikasema hapana kuna wageni wangu naenda kuwapokea hapo nje, akasema sawa ni vema tukaongozana.

ITOSHE KUSEMA JUZI NDIO SIKU NIMEONDOKA KWENYE SHEREHE BILA KULA.

Nikaenda Kibozone Pub nikaagiza Maji madogo ya buku nikawa nakunywa huku nalia, jamaa yangu Dwella Weston akaniuliza nini kimenikuta nikamwambia wee acha tu🤣

Basi akaishia kunipa pole tu!!!!
 
Inaonekana shemeji yako ndio alikupa kadi ya harusi.
 
Shida hujakaa mjini sana, hayo mbona matatizo madogo ya kusolve tit-for-tat kisha at the end of the road 🛣️ ungetoka na mtoto mmoja wa kishua wa bariiiiidi kwenda kukata kiu? 😂🤣
 
Back
Top Bottom