TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,747
"Meya wa Kinondoni amkaribisha Benard Membe Chadema". Hicho ni kichwa cha habari katika gazeti la Mwananchi ambapo Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob amenukuliwa akimshauri aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje katika awamu ya nne, Benard Membe ahamie UKAWA kwa kile alichokisema hoja alizozitoa Waziri huyo wa Zamani ni za msingi na zilipaswa kutolewa na mpinzani.
Sina haja ya kurudia nini Membea amesema, kama sote tunafuatilia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii tunajua.
Pamoja na Meya Jacob kuziita hoja za Membe ni za msingi, . Nanukuu "Nadhani hakuwa mtu sahihi kusema hayo, alipaswa kwanza kumtafuta mtu mwingine aseme halafu yeye afuate baadaye, lakini kuanza kusema yeye moja kwa moja wakati alikuwa ananufaika na anachokipinga Rais, anaonekana anamuonea wivu na mgongano wa maslahi. Sasa anapoanza kujibu yeye inashangaza kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, iliyokuwa inafanya matumizi makubwa halafu unakosoa unaonekana kabisa unaonesha kuna mgongano wa maslahi". Mwisho wa kunukuu.
Wanachadema na UKAWA kwa ujumla muulizeni;
1. Mbona anakuwa kigeugeu? Anaziona hoja za Membe za msingi wakati huohuo anasema Membe anamuonea wivu Dr. Magufuli kupiga marufuku safari za nje na kwamba ana mgongano wa kimaslahi kwa sababu yeye alinufaika nazo
2. Kwanini anataka Membe ahamie UKAWA wakati amekiri wazi kuwa alinufaika na safari nje wakati akiwa Waziri wa Nje jambo lililoliingizia taifa hasara kubwa? Au ndo kuwaaminisha Watanzania kuwa ni halali wachafu wote kufuata mkondo wa LOWASSA?