Habari za Kapunga zimeandikwa sana na waandishi wa habari Mbeya, hata hii ya milioni 95 imeshandikwa kwenye Raia Tanzania, tatizo haliko kwa waandishi wa habari bali nyinyi wenyewe mnaomchagua na madiwani wenu wenye kumpa umeya kwa ajili ya chips kuku anazowapa.
Suala lake lilifika kwa JK akawatolea nje akiwaambia hilo ni suala lao wenyewe mliomchagua.
Sakata la safari ya awali ilikuwa sh 5m/ nalo liliandikwa sana, la sasa mbali ya fedha kuwa kubwa pia hazikuwemo kwenye bajeti ya mwaka ya jiji hilo, zimekombwa kutoka mafungu mengine, ndipo Chadema wanahoji aliyewapa hayo mamlaka.
Wanambeya huo mzigo wenu wenyewe mlioulea, mmeletewa Mkurugenzi, aliyeleta nidhamu na ufani wa kazi, akapandisha makusanyo toka bilioni mbili hadi 15, lakini alipotengezewa majungu na huyo meya wenu na DC Sigala hakuna aliyemtetea mlikaa kimya, leo mnapiga domo hapa.
Simamieni jiji lenu, msiwaachie hao vijana wachache wa Chadema wawatatulie matatizo yenu, waungeni mkono kwa kuingia barabarani. Mbunge wenu Sugu hana nguvu yoyote yupo bize na kunfu bungeni, madiwani wa Chadema hapo Mbeya ni vifaa kinachotakiwa ni kuwaunga mkono kwa wananchi kuingia barabarani hadi Kapunga ang'oke, mkisimama pamoja CCM wataogopa, watamtoa
Ndugu zangu habari za mwaka mpya.
Ni wazi shahiri kuwa meya huyu kauanza mwaka vibaya sana.
Ni ktk kikao cha WDC ambacho huwa cha wazi ilimbidi avunje kikao ili kuruhusu wananchi kutolewa nje.
Agenda ilokuwa inafuatia ni ya matumizi ya tshs 95 ml alizotumia kwenda China kama nauli ilihali nauli halisi ni tshs 3.ml go and return.
Ni madiwani wa chadema wapatao 16 walouwasha moto hadi kufikia na wa ccm kuungana pamoja kuwa arejeshe haraka pesa hizo.
Meya huyu wa STD 7 aligoma akidai zilitumika zote kwenye matumizi ya maradhi.... hapa akaamsha hasira za madiwani walioamka kwa pamoja na kumwagia maji mwili mzima.
Kapunga kwa wanaomfahau vizuri hajaanza wizi leo. Ufisadi ameuanza muda mrefu yeye na Kabwe ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na ndiyo maana kila mkurugenzi mzuri anayepelekwa Mbeya ni lazima amjengee fitina aondoke ili aendelee kufanya ufisadi.Anapenda kuwa na mkurugenzi ambaye anachotaka yeye iwe hivyo.Pia tatizo lipo kwa wanahabari je wanaweza wakaandika habari hiyo ya meya.Namkumbuka mwandishi mmoja wa NIPASHE anaitwa Thobias Mwanakatwe angekuwepo mbeya angeliandika. Huyu meya ni fisadi wa kutupa ana madepo ya kuuza bia kila kona katika jiji la mbeya na mjini mbalizi fedha zote za kifisadi. madiwani chadema kazeni butu hadi ang'oke huyo fisadi.amenunua viongozi wote wa CCM wa wilaya na mkoa hawawezi kukohoa kwake hata akijamba wanasema ndiyo mheshimiwa unasemaje.