Meya wa jiji la Dar Isaya Mwita pole na changamoto unazopitia

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
757
842
Mwita ukiambiwa kuwa CCM haina urafiki na mtu kwenye maslahi yake uwe unaelewa!

Naomba nikukumbushe kidogo, unakumbuka maelekezo mangapi umekuwa ukipewa utekeleze ukawa unatekeleza kwa kificho ili kuwafurahisha hao wanaCCM na mengine ukawa unasitasita kuyatekeleza?

Imefika zamu sasa kutekeleza agizo la kuachia nafasi yako ili mambo ya watu yaweze kuenda kwani umekuwa kikwazo maana sasa hivi umekuwa unachagua maelekezo ya kutekeleza.

Juzi umeelekezwa uchague kupokea mlungula uachie nafasi au ukose kila kitu. Ndugu yangu fanya maamzi sahihi sasa maana yaliyoko mbele yako ni mazito kwa kuwa upo peke yako umejiweka kando kidogo na Chama chako sijui kama utastahimili.

Juzi ulipoambiwa kachungulie kilichopo kwenye account yako kupitia ATM iliyoko karibu na ofisi yako nafikili hutokuja kusahau kilichokukuta, ulishitukia unapandishwa magari tofauti tofauti ndani ya masekunde na kupelekwa ulikopelekwa bila kutegemea, ukirudi naomba utusimulie uliyokutana nayo ili iwe fundisho kwa wanasiasa wengine kama wewe.

Kwenye siasa hakuna mpambano wa kipeke pekee mtu anaweza kushinda, kunahitaji mshikamano, kujitoa nafsi na mali, uzalendo, n.k, lakini pia kushika dola si kazi lelemama maana aliyeishikilia atatumia kila mbinu ya hila na uovu ili aweze kuendelea kushikilia dola.

Nasisitiza ukirudi ulikopelekwa ile juzi utusimulie yalikukuta yote kwa maslahi ya Taifa letu na wanasiasa wenzako ili watu wapate kujifunza!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema mtinika alikuwa kijana mzur sana toka anasoma Mbalizi sekondar mbeya sijui nini kimembadilisha baada ya kujiunga ccm
 
Politicians are people who have chosen their careers Just like accountant the only difference is that Politicians when they under perform firing them will depend on the influence of their followers and party leaders.

They can also be fired even when their are performing very well for reasons mentioned above.

I hate politics and politicians.
 
Since 1995, Ihate politics and politicians, dont ask me why!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Ungeandika Tu Kiswahili mkuu
Politicians are people who have chosen their careers Just like accountant the only difference is that Politicians when they under perform firing them will depend on the influence of their followers and party leaders.

They can also be fired even when their are performing very well for reasons mentioned above.

I hate politics and politicians.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom