Meya wa jiji la Dar, Isaya Mwita ashindwa kuingia ofisini kwake baada ya kubadilishiwa nywila ya mlango

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,215
7,906
Katika kile ambacho hakukitarajia Meya wa Jiji la DSM, Isaya Mwita amejikuta akisota nje ya Ofisi yake katika Jengo la Karimjee baada ya kufika Ofisini hapo leo asubuhi na kukuta mlango wa Ofisi yake umebadilishwa Password za kuingilia.

Isaya Mwita amesema, "Wamebadilisha Pasword za mlango wa Ofisi yangu ili jambo sio la kawaida sana lakini naendelea na nitaendelea kuwa Meya wa Jiji hili, nimeamua lolote litakalonikuta litanikuta niliapa kuulinda Umeya kwa maslahi ya Watu wa DSM sitoogopa chochote, yeyote na sina hofu yoyote"

Pia soma
i. Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Meya anyang’anywa gari, ofisi yafungwa. Adai kuwa yeye bado ni Meya halali
ii. Meya Issaya Mwita atinga ofisini kuendelea na kazi

EOJRAT0X4AEiJ-1.jpg
 
Katika kile ambacho hakukitarajia Meya wa Jiji la DSM, Isaya Mwita amejikuta akisota nje ya Ofisi yake katika Jengo la Karimjee baada ya kufika Ofisini hapo leo asubuhi na kukuta mlango wa Ofisi yake umebadilishwa Password za kuingilia.

Sent using Jamii Forums mobile app
hureeeeeeee!!! baada ya hapo serikali ya CCM itagawa million 50 kwa kila kijiji.
 
Sexer,

Na sasa ajikite zaidi katika Kujiimarisha zaidi Kiusalama kwani kwa aina ya Ushujaa wake wa Kikurya sidhani kama anaopambana nao watamuacha salama hata kama siyo leo au kesho.

Ushauri wangu mkubwa Kwake ni kwamba kuanzia sasa awe makini na tena hao hao ambao sasa wanamuunga mkono na kumtia Moyo ndiyo hao hao watakaofanikisha tukio zima Kumtokea kwa Unafiki wao uliozoeleka halafu baadae utawaona wanakuja Mitandaoni kupiga Makelele ya Utetezi na Kumlilia.

Bado nasisitiza Mpendwa wetu huyu na Mkurya Mbishi kwa mwendo wake huu anaokwenda nao sasa awe makini kidogo na ikiwezekana bado abadilishe Mbinu na Mikakati ila binafsi nikikumbuka yaliyowatokea wengine naanza taratibu kuingiwa na wasiwasi.
 
Yani wamefikia hatua ya kumuondoa madarakani kwa lazima? wakati kuna sheria na kanuni zinazo regulate hilo suala, kumbe CCM wakibanwa hawaoni aibu kuvunja sheria!, halafu kuna wazembe wana support hili, hii nchi imejaa mizigo tu, sasa ni jukumu la wananchi kufanya kitu, this must stop kwa namna yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom