Meya wa Jiji la Dar akanusha taarifa zinazoenea mitandao ya kijamii

Chademakwanza

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
6,346
1,871
Screenshot_2016-07-16-11-44-09.png


Ameyasema haya kwenye Ukurasa wake wa Twitter.
 
NAOMBA Moderator Invisible Mod 4 Mod 2 NA Paw MMTENDEE HAKI ALIYE LETA TAARIFA YA MEYA KUPINGA AGIZO LA MKUU WA MKOA.

HAKIKA ISAYA NI TOFAUTI NA BAVICHA NA CHADEMA. NINGESHANGAA MEYA ANAPATA WAPI MAMLAKA YA KUINGILIA KAZI ZA MKUU WA MKOA
 
Meya huyu ni wa tofauti kidogo yupo kulinda maslahi ya watu wake na maendeleo ya wananchi ndo mana raisi alimwambia wakimfukuza chadema atampatia kazi yupo vizuri sana huyu
 
Kama kskanusha taarifa ya Makonda basi aliyeleta taarifa ile apate haki yake, na kama tasrifa hii ya kukanusha sio sahihi basi na huyu apate haki yake.
 
Taarifa za uhakika zilizonifikia hivi punde, kutoka chanzo chenye mamlaka katika ofisi ya Meya wa jiji la Dar es salaam, ni kwamba.

Taarifa kwa umma iliyoanza kusambaa tangu jana na inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, si taarifa rasmi iliyotolewa na mstahiki meya au katibu wake au mtu mwingine yoyote kwa maelekezo ya meya.

Aidha chanzo hicho kina sema taarifa hiyo inayosambazwa kuhusu kupingana na Makonda, ni ya kupuuzwa, kwa sababu

1:Si jukumu lake la kisheria kujibizana na kiongozi yeyote au kufanya malumbano kupitia njia yoyote ya mawasiliano

2:Bila kujali uzuri au ubaya wa tamko hilo ambalo hakulitoa yeye (Meya wa Jiji) Lakini hapaswi kuiacha jamii ikatambua kuwa ni tamko lake ili hali si lake, na kwa sababu hiyo basi anapaswa kukanusha ili tabia hii ya kutolewa kwa matamko ambayo chanzo chake si ofisi yake yasiendelee na wala haihitaji kusemewa na mtu mwingine ambae hajamtuma.

3:Lakini pia chanzo cha taarifa hiyo kusambazwa ni baada ya gazeti la Uhuru linalomilikiwa na ccm kuandika story ya Makonda kuanzisha msako, na ni gazeti pekee lililoripoti taarifa hiyo, sasa kwa kuwa utaratibu wa Meya si kutumia muda wake kujibizana na kiongozi wa aina yoyote, anawaomba wananchi wawe na utulivu pale ambapo kuna jambo atatoa taarifa rasmi.

My take tusiwe na utamaduni wa kusambaza taarifa ambazo chanzo chake si sahihi, hasa kwa viongozi wa ukawa ambao sidhani kama wajibu wao ni kujibizana na viongozi wa upinzani katika jiji la Dar es salaam na manispaa zake mbili ambazo ziko chini ya Ukawa, hawajawahi kukurupuka na hawatawahi kukurupuka.
 
Kuna kitengo Fulani chadema kazi yake kutunga uongo na kupotosha kila aina ya habari inayohusu viongozi kisha wanasambaza kwenye mitandao ya kijamii
..


Baada ya kutunga mafuriko feki ya lowasa na kutupiliwa mbali na wananchi sasa wanahaha kila kona kutunga uongo mwingine.
 
Taarifa kwa umma iliyoanza kusambaa tangu jana na inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, si taarifa rasmi iliyotolewa na mstahiki meya au katibu wake au mtu mwingine yoyote kwa maelekezo ya meya.

Kuna huyo mtu humu jamiiforums anayeanzisha taarifa nyingi za CHADEMA ikiwemo hiyo ya meya anaitwa MWANAHABARI HURU huyu alinifanya hadi nikaanzisha maada kuuliza

CHADEMA kuna mapinduzi? Mbona kila mtu ni msemaji wa CHAMA?

Huyu mwanahabari huru amekuwa kutwa akizusha taarifa za CHADEMA zisizo za ukweli akijifanya ni za viongozi wa CHADEMA.Moderators mpeni haki yake
 
Back
Top Bottom