Meya wa Jiji la Dar akanusha taarifa zinazoenea mitandao ya kijamii

Taarifa za uhakika zilizonifikia hivi punde, kutoka chanzo chenye mamlaka katika ofisi ya Meya wa jiji la Dar es salaam, ni kwamba.

Taarifa kwa umma iliyoanza kusambaa tangu jana na inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, si taarifa rasmi iliyotolewa na mstahiki meya au katibu wake au mtu mwingine yoyote kwa maelekezo ya meya.

Aidha chanzo hicho kina sema taarifa hiyo inayosambazwa kuhusu kupingana na Makonda, ni ya kupuuzwa, kwa sababu

1:Si jukumu lake la kisheria kujibizana na kiongozi yeyote au kufanya malumbano kupitia njia yoyote ya mawasiliano

2:Bila kujali uzuri au ubaya wa tamko hilo ambalo hakulitoa yeye (Meya wa Jiji) Lakini hapaswi kuiacha jamii ikatambua kuwa ni tamko lake ili hali si lake, na kwa sababu hiyo basi anapaswa kukanusha ili tabia hii ya kutolewa kwa matamko ambayo chanzo chake si ofisi yake yasiendelee na wala haihitaji kusemewa na mtu mwingine ambae hajamtuma.

3:Lakini pia chanzo cha taarifa hiyo kusambazwa ni baada ya gazeti la Uhuru linalomilikiwa na ccm kuandika story ya Makonda kuanzisha msako, na ni gazeti pekee lililoripoti taarifa hiyo, sasa kwa kuwa utaratibu wa Meya si kutumia muda wake kujibizana na kiongozi wa aina yoyote, anawaomba wananchi wawe na utulivu pale ambapo kuna jambo atatoa taarifa rasmi.

My take tusiwe na utamaduni wa kusambaza taarifa ambazo chanzo chake si sahihi, hasa kwa viongozi wa ukawa ambao sidhani kama wajibu wao ni kujibizana na viongozi wa upinzani katika jiji la Dar es salaam na manispaa zake mbili ambazo ziko chini ya Ukawa, hawajawahi kukurupuka na hawatawahi kukurupuka.
Eti iliyo nifikia rasmi!!!!!!yeye meya anashindwa nini kujitokeza akasema?mnalo hilo maana tayari wananchi tumeshafahamu nini cha kufanya
 
Kuna huyo mtu humu jamiiforums anayeanzisha taarifa nyingi za CHADEMA ikiwemo hiyo ya meya anaitwa MWANAHABARI HURU huyu alinifanya hadi nikaanzisha maada kuuliza

CHADEMA kuna mapinduzi? Mbona kila mtu ni msemaji wa CHAMA?

Huyu mwanahabari huru amekuwa kutwa akizusha taarifa za CHADEMA zisizo za ukweli akijifanya ni za viongozi wa CHADEMA.Moderators mpeni haki yake
Mbona hujauliza taarifa ya lizaboni juu ya ku mtuhumu naibu katibu mkuu wenu?
 
awe amesema au hakusema,jibu ni moja tu mhe.makonda jiji limeanza kukutupa mkono,rudi nyuma jitathimini huko unapoelekea..........
 
Taarifa ni nyingi zinazosambaa kwenye mitandao, ajaribu kuwa specific ni taarifa gani anazokanusha kuhusika nazo la sivyo naye ni JIPU
 
Kuna kitengo Fulani chadema kazi yake kutunga uongo na kupotosha kila aina ya habari inayohusu viongozi kisha wanasambaza kwenye mitandao ya kijamii
..


Baada ya kutunga mafuriko feki ya lowasa na kutupiliwa mbali na wananchi sasa wanahaha kila kona kutunga uongo mwingine.
mkuu,sema tu ukweli. hata lumumba kitengo hicho kipo na mambo yake tunayaona mengi humu jf.na kiutendaji kiko juu zaidi ya hicho cha chadema.
 
Back
Top Bottom