Wasalaam wanabodi,
Nimekuwa nikifuatilia hotuba mbalimbali za Mh. Mayor wa Jiji la Arusha ndugu Kalisti. Nitatoa hotuba mbili za hivi karibuni. Kwanza, nilimsikiliza katika mkutano wa Tacine ( Tanzanian Cities Network) kilichofanyika Jijini Arusha na jana nimemsikiliza akitoa hotuba fupi kwenye mkutano wa wadau wa Master Plan ya Arusha pale Lush Garden.
Huyu mheshimiwa ni mtu mwenye maono sana na Jiji hili kwa ujumla wake. Sina ugomvi binafsi na Mh. Lema lakini naona kuwa kwa aina ya maendeleo yanayotakiwa ndani ya Jiji hili, Mh. Lema anapwaya sana.
Niwaombe CHADEMA kwenye uchaguzi ujao 2020 tumpate mgombea mwingine wa aina ya huyu Mayor ndugu Kalisti. Mtu anayeona maendeleo ni zaidi ya kuwahamasisha vijana kuondoa uwoga kwenye maandamano.
Ni hayo tu wadau.