Meya wa Dar Mafuriko hayo tutatulie changamoto hiyo!!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,076
29,632
Hii imfikie meya wa jiji la Dar...ajionee mwenyewe na ninajua keshajionea MAFURIKO YA UKWELI na sio yale ya kisanii...

Nataka kuona Meya wa jiji na madiwani wake kutoka UKAWA wakisaidiana na vichwa vya elimu ya hapa na pale wanakuja na maazimio na utetekezaji wa kuhakikisha jiji la Dar halifuriki...!

Najua RC Makonda ameshaanza na kampeni ya usafi...sasa nasubiri think tanks wa UKAWA KANDA YA DAR wakija na utatuzi wa hili dogo la Mafuriko...Kuhusu majipu wamuachie super surgion JPJM!!
 
Una tabia za kike,kama ni mwanaume pole!Huwezi jenga hoja bila kuweka umbea umbea,udaku,fitna na majungu?shame
 
swala liko jikoni ccm walishindwa hata kutengeneza njia za maji yanabaki kuiba mali za umma na kuacha kuwatumikia wananchi kila kitu na miundo m mbinu yamebolonga kazi ni kuiba na kutojari wananchi.subiri Ukawa wawaonyeshe jinsi watu walivyowatuma.jingalao sana ccm.

swissme
 
Utamu wa ngoma uingie ucheze na sio kutoa maelekezo ungechea hivi. Muda wa kuwaonesha wananchi na watanzania kwa ujumla pumba zipi na mchele upi au hata kama zote ni pumba umewadia! Tusubiri tuone. Tupongeze panastahili na tukosoe inapobidi
 
Kwenye mambo ya hovyo wako haraka sana kwenye media,sasa kuna mafuriko kila mahali jijini wameingia mitini
 
Hii imfikie meya wa jiji la Dar...ajionee mwenyewe na ninajua keshajionea MAFURIKO YA UKWELI na sio yale ya kisanii...

Nataka kuona Meya wa jiji na madiwani wake kutoka UKAWA wakisaidiana na vichwa vya elimu ya hapa na pale wanakuja na maazimio na utetekezaji wa kuhakikisha jiji la Dar halifuriki...!

Najua RC Makonda ameshaanza na kampeni ya usafi...sasa nasubiri think tanks wa UKAWA KANDA YA DAR wakija na utatuzi wa hili dogo la Mafuriko...Kuhusu majipu wamuachie super surgion JPJM!!
mimi nilijua kwamba vile mlivyowabomolea wakazi wa mabondeni labda maji yangetiririka kwenda baharini , kumbe hamna kitu ! sasa ni faida gani mlipata kwa unyama ule ?
 
Una tabia za kike,kama ni mwanaume pole!Huwezi jenga hoja bila kuweka umbea umbea,udaku,fitna na majungu?shame
Ha ha ha ha. Mkuu umeua kila kitu. Hata hivyo changamoto ya mafuriko siyo ndogo kama unavyofikiria. Na kwa Manispaa ya Kinondoni ni lower point, lazima maji ya kutoka Ila, Kisarawe, Mbezi, Kimara yaende huko!
 
Mmmekuwa viongozi kwa miaka 54 mkashindwa sembuse hawa walioshika kwa miezi 6! Kumbe jina lako linaakisi akili yako
 
Back
Top Bottom