Meya wa Dar es salaam Isaya Mwita asubiri masaa tu kuondolewa kwenye nafasi yake

jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,756
4,842
Kutokana na kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuchunguza tuhuma zinazomkabili Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (CHADEMA) kuwa tayari imeshakamilisha ripoti yake na kilichobaki ni kuiwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa ajili ya hatua zaidi.

Haswa ikizingatiwa kwamba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndiye mwenye mamlaka ya kuunda kamati ya kuchunguza tuhuma, na kuchagua wajumbe wa hiyo kamati anaowataka yeye, wengi wanaona Meya wa jiji la Dar es salaam ataondolewa kwenye nafasi yake kutokana na wingi unaowapa nafasi madiwani wa CCM kumpigia kura za kutokuwa na imani nae.

CCM ina madiwani 9, na upinzani wana madiwani 7, na ikidhaniwa mmoja wa madiwani wa CUF yupo upande wa CCM.

Hili lilijidhihirisha zaidi baada ya Meya wa Ubungo Boniface Jacob na diwani wa Tabata (CHADEMA) Patrick Asenga kutokwenda kwenye mahojiano wakiamini CCM wamedhamiria kumuondoa Meya wa CHADEMA kwa kuwa hawataki kuongozwa na upinzani.

Kutokana na muda mfupi uliobaki, nafasi ya Meya itazibwa na Naibu Meya kutoka CCM, baadhi ya tuhuma zinazomkabili ni pamoja na matumizi mabaya ya gari ya ofisi yaliyopelekea Meya kupata ajali, kitotumia sh bilioni 5.8 za shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na kusababisha Meya wa Ubungo na Temeke (Abdala Chaurembo) wasielewane. Tuhuma ambazo Meya wa Dar es salaam amekuwa akizipinga vikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
daudi bashite sijui amempa nini yule jamaa yetu yaan hata hawezi furukuta na dogo anatamba tu nigepata tunguru alilotumia bashite walahi na mimi ningekuwa wa pili nyuma yake

HAIWEZEKANI KUDTUDANGANYA SISI, WAKATI TULKUBALINA CCM ITAMPA MILLION 700 AKAWA AEKUBALI LAKINI BAADAYE AMETULIA TU,SASA LAZIMA KAMA CCM TUMUONDOE
 
Meya kachaguliwa kwa kura za wanachi, kwa nini aundiwe.kamati ya kumuondoa na mtu aliyekuwa.hand picked tu. Haiingii akilini. Atabakia kuwa ni meya halali.tu ndani ya sheria ya haki!
Meya huchaguliwa na wajumbe(madiwani wenzake),hivyo yeye kama diwani ndio huchaguliwa na wananchi. Hapo ataondolewa umeya na sio udiwani kama tume imemtia hatiani. Nakubali kurekebishwa kama nimekosea.

macson
 
Back
Top Bottom