Method Mwanjali: Mchezaji wa Nguli wa Mamelodi Sundowns

Method Mwanjali: Mchezaji wa Nguli wa Mamelodi Sundowns

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Posts
4,582
Reaction score
2,783
WanaJF forum za Leo!

Leo katika pitapita zangu mitandaoni nime kutana na jina la mchezi wa mlinzi wa timu ya Mamelodi Sundowns ya A. Kusini. Jina lake linaandikwa kama Method mwanjali au mwanjale mwenye uraia wa nchi ya Zimbabwe. Nikavuta pumzi na kuona sili ya mchezaji huyu itakuwa Unyakyusani kule Mbeya.

Hebu tujiulize wakuu kama TFF pengine ingekuwa na taarifa zuri za wachezaji wenye asili ya TZ na kuweza kuwatumia tungekuwa wapi kisoka?

Kuna wachezaji wengi pengine wa namna hii ila hatujawatambua.

 
Usemacho chaweza kuwa kweli kuwatumia
waxhezaji kama hao ikiwa wana asili ya hapa
Nyumbani.

Tatizo wakija hapa watacheza nini zaidi ya
majukumu kila kukicha.
Ona Simba & Yanga wamejaza makomandoo
pamoja na wazee wanaoamkia Klabuni bila
hata kupiga mswaki asubuhi.

Ona wale Wazee wa Yanga walitaka kuichukuKlabu na kulipa mishahara
wachezaji wakati wenyewe hawana hata
viatu miguuni.

Watu wanatumia wachache kwa maslahi
yao.
 
Mkuu Gaza and Islael, hayo majina yenye "Mwa" sio ya mbeya pekeyake bali ni ya ukanda karibu wote wa kusini unaozijumuisha Zambia, Malawi na Zimbabwe, na huyo sio mchezaji wa kwanza kutoka Zimbabwe mwenye hilo jina yupo pia Benjani Mwaluwali
 
Last edited by a moderator:
Kweli kuna kitu kama hicho nadhani kwa Malawi zaidi, Zambai zaidi tunafanana kwnye majina kama Si-Sikala, Simbeye, nk. Hasa hawa ni wale wa Mbozi na Rukwa.

Nilichoshangaa ni jinsi majina yanavyotumika-Mwanjali au Mwanjale ambayo yapo Mbeya kwa wingi wala si ya kutafuta.
 
Nasikia kuna wabongo wengi tu ulaya sana scandinavian countries,wanapiga mpira,ukiwatajia TZ awataki kusikia kabisa.
 
Back
Top Bottom