mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,191
- 19,117
Goli la messi leo ni tamu kuliko magoli 3 ya cr7, linawanyanyua wapenzi wote wa Baca dunia nzima kuupokea UBINGWA, angekuwa anajua huyo cr7wenu angejua kufunga magoli yenye kubadili matokeo, sasa yeye amefunga magoli mengi halafu timu aliyoifungia hayo magoli mengi siyo bingwa.
Inaonyesha cr7 ni mbinafsi kupindukia, hawezi kuwachezesha wenzake ili ushindi wa jumla upatikane.
Cr7 Atachungulia sana kwenye tv wakati wenzie wanajitwika ndoo msimu huu.
Nyie ndio wale wale msiojua mpira wa miguu. Nani kakuambia kigezo ni magoli peke yake. Tunaojua mpira tunakushangaa.
Kwaa akili zako ndogo hiz za mpira, basi Zidane, Gaucho, na hata The real Ronaldo sio wachezaji bora mana hawakuwa wakifunga mara nyng km anavyofunga CR7.
Mbona Guard Muller alikuwa anafunga sn mpk record yake imevunjwa mwaka jana na Messi na wala hy Muller hyupo ktk list ya wachezaj bora hatar waliowah kuwepo? Naamin hata huyo Muller humjui, we unamjua Thomas Muller tu.
Ngoja niishie hapa, ww kwny mpira bado sanaaaaa.....
Hivi ina maana messi naye ni mchovu kwa assistHuwezi kumlinganisha Zidane na Messi au Ronaldo kwa kutumia kigezo cha magoli kwa sababu nafasi zao ni tofauti na majukumu yao ni tofauti! Zidane ni kiungo wakati Messi na Ronaldo ni washambuliaji! Viungo wanalinganishwa kwa pass accuracy, stability & ball control, assists, ball holding capacity and the like! Kwa vigezo hivyo vya Viungo Zidane ni kiungo bora wa muda wote! Lakini Messi na Ronaldo wote ni washambuliaji, Hivyo kuwalinganisha kwa kigezo cha magoli ni sahihi maana ndiyo majukumu yao ya msingi kwenye timu. Kama ukitaka kutumia kigezo cha assists, wote wawili inabidi wakae pembeni wawe watazamaji! Huo ni uwanja wa akina Fabrigas, Hazard, Xavi, Iniesta, chini ya mtemi wao Zidane!
Mkuu so unazungumzia mfungaji na mchezaji bora au? Maana leo nikikuambia unipe record ya Zidane kama alishawah chukua kiati cha dhahabu ila kwann alichukua uchezaji bora?
Mess magori anayofunga yana akil kuliko anayofunga Ronaldo, Ronaldo anafunga magori easy kabisa ambayo ata Sergio Ramos ila angalia anavochukua mpira Mess na kwenda kiweka kimiani utaona utofauti wa Mess na Ronaldo.
Jana nilikuwa na angalia mpira na mshabiki mkubwa wa Ronaldo lakin alikubali kuwa Mess ni zaid ya Ronaldo huku akitumia neno la utani (Mess kweli yule jamaa Zombie) na kunalizia kuwa Ronaldo amepata bahati ya kufunga tu lakin kimsingi hamfikii Ronaldo
Huwezi kumlinganisha Zidane na Messi au Ronaldo kwa kutumia kigezo cha magoli kwa sababu nafasi zao ni tofauti na majukumu yao ni tofauti! Zidane ni kiungo wakati Messi na Ronaldo ni washambuliaji! Viungo wanalinganishwa kwa pass accuracy, stability & ball control, assists, ball holding capacity and the like! Kwa vigezo hivyo vya Viungo Zidane ni kiungo bora wa muda wote! Lakini Messi na Ronaldo wote ni washambuliaji, Hivyo kuwalinganisha kwa kigezo cha magoli ni sahihi maana ndiyo majukumu yao ya msingi kwenye timu. Kama ukitaka kutumia kigezo cha assists, wote wawili inabidi wakae pembeni wawe watazamaji! Huo ni uwanja wa akina Fabrigas, Hazard, Xavi, Iniesta, chini ya mtemi wao Zidane!
Umeishiwa hoja! Ronaldo na messi wote ni washambuliaji, jukumu lao la msingi ni kufunga magoli. Hivyo kigezo kizuri cha kuwalinganisha ni kwa Kiasi gani kila mmoja ametimiza jukumu hilo. Hivyo wingi wa magoli waliyofunga katika mazingira sawa ndio kigezo cha kisayansi cha kuwalinganisha! Mpaka sasa kwenye la liga Messi amecheza mechi 37 na amefunga magoli 41, na kasi yake ya kufunga magoli ni magoli 1.108 kwa mechi moja. Ronaldo amecheza mechi 34 na amefunga magoli 45, na kasi yake ya kufunga magoli ni magoli 1.324 kwa mechi moja. Hivyo ni dhahiri kabisa Ronaldo yuko JUU. Messi atasubiri sana!
Kama ni hivyo mbona msimu uliopita timu ya messi iliambulia patupu la liga? Hapa hatulinganishi timu, bali tunawalinganisha strikers wawili wanavyotimiza majukumu yao yanayofanana! Jukumu la mshambuliaji ni kufunga magoli na si vinginevyo! Akifanya vingine ni ziada. Kwa majukumu yao ya msingi kama washambuliaji ni kufunga magoli! Na katika hilo hakuna ubishi takwimu ziko wazi, Messi magoli 41 katika mechi 37 na Ronaldo ana magoli 45 katika mechi 34! Mwenye macho haambiwi Tazama! Ukitaka kulinganisha timu zao anzisha uzi mwingine!
Kama ni hivyo mbona msimu uliopita timu ya messi iliambulia patupu la liga? Hapa hatulinganishi timu, bali tunawalinganisha strikers wawili wanavyotimiza majukumu yao yanayofanana! Jukumu la mshambuliaji ni kufunga magoli na si vinginevyo! Akifanya vingine ni ziada. Kwa majukumu yao ya msingi kama washambuliaji ni kufunga magoli! Na katika hilo hakuna ubishi takwimu ziko wazi, Messi magoli 41 katika mechi 37 na Ronaldo ana magoli 45 katika mechi 34! Mwenye macho haambiwi Tazama! Ukitaka kulinganisha timu zao anzisha uzi mwingine!
ronardo ni moto wa kuotea mbali sana, mess amecheza barca tu hata nongekuwa mimi nangeshine tu kwani ukishazoeana na wachezaji wengine, lakini ronaldo kama unavyoona mwenyewe amecheza ligi tatu kubwa na nado anatesa tu,
messi better than ronaldo - cole
chelsea's joe cole says barcelona's lionel messi is ahead of manchester united star cristiano ronaldo as the best player in the world.
source: Bbc sport|football
mimi binafsi nakubaliana kabisa na maneno ya joe cole hapo juu, messi anatisha!
ronardo ni moto wa kuotea mbali sana, mess amecheza barca tu hata nongekuwa mimi nangeshine tu kwani ukishazoeana na wachezaji wengine, lakini ronaldo kama unavyoona mwenyewe amecheza ligi tatu kubwa na nado anatesa tu,
~ Ronaldo ni mfungaji bora sana sana saaaaaana wa wakati huu.
~ Messi ni mchezaji bora wa wakati wote, genius kutoka sayari nyingine.
kuwachanganya watu hao ni udhaifu tu wa kibinadamu.
Kwa maandishi haya, nalazimika kuhoji juu ya uzima wa akili yako!
Certified insane! Lol!
Acha ushabiki mkubwa toka kwenye ako kajela upate uhuru wa kufurahia soka..inachukua miaka mingi sana Dunia kupata watu wa kariba ya messi, umepata nafasi usijinyongee..wewe furahia rhythim ya soka ya Messiah wa soka..Messi!
CR7 nampa pongezi inataka ujasiri mkubwa kujaribu kupambana na Messi..
Unapolinganisha wachezaji wawili lazima kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Utumie kigezo kinachopimika ili kuondoa subjectivity!
2. Wachezaji wawe na majukumu yanayolingana.
3. Wachezaji wawe katika mazingira yanayofanana kwa Kiasi kikubwa.
Ni halali kuwalinganisha Messi na Ronaldo kwa kutumia magoli kwa sababu ndicho kigezo pekee kinachopimika na ndiyo majukumu ya wote wawili kama washambuliaji ambayo ni kufunga magoli! Na pia wako katika mazingira yanayofanana kwa Kiasi kikubwa maana wote wanacheza ligi moja (la liga), na magoli yao wanayapata kwa kucheza na timu zile zile, wakipambana na mabeki wale wale!
Zaidi ya kutumia magoli huwezi kupata kigezo kingine ambacho ni objective! Vinginevyo watu tunatofautiana kuhusu ladha tunayopenda, usipotumia objective criteria kila mtu atakuja na hisia zake anazoziamini yeye!
Ndiyo maana timu inayoondoka na pointi tatu muhimu ni ile iliyopata magoli mengi kuliko timu pinzani na hakuna ubishi katika hilo maana kila timu iliingia uwanjani ikiwa na jukumu moja la msingi ni Ushindi kwa kigezo cha magoli. Vigezo vingine vyote havipimiki hivyo havina msaada katika kumpata mshindi pasipo ubishi!
Kwa hiyo kwa sasa Ronaldo ni bora kuliko Messi, Messi ana magoli 41 katika mechi 37, wakati Ronaldo ana magoli 45 katika mechi 34!
Habari ingekuwa nyingine kabisa kama Ronaldo angefanikiwa kucheza mechi zote!
Ndio maana mashabiki wa Messi kwa kuzidiwa hoja na vigezo vya kitaalam wanaishia kutoa kejeli na matusi!
Kuhusu
Kuhusu Zidane si haki kumlinganisha Zidane na hawa wengine maana majukumu yao ni tofauti, na hawajacheza katika mazingira sawa, Hivyo huwezi Kupata kigezo kinachopimika kitakachowatendea haki wote.
Ndiyo maana hakuna mchezaji wa dunia aliyewahi kuchaguliwa kwa asilimia inayofikia asilimia 50%. Kwa maneno mengine dunia haijawahi kukubaliana ni nani aliye mchezaji bora wa dunia maana wanatumia kura hivyo zoezi zima kuingiliwa na subjectivity! Huwezi kuwalinganisha kwa haki golikipa, defender, midfielder, na strikers!
Ndiyo maana mtu akichukua kiatu cha dhahabu kama anavyotarajia Ronaldo mwaka huu ni wa kuheshimiwa maana kigezo kinachotumika kinapimika (magoli), na kinawahusisha wachezaji wenye majukumu yanayolingana (strikers)! Ukilikataa hili huwezi kubisha kuwa vigezo unavyotumia havipimiki hivyo kutumia hoja ya nguvu (kulazimisha interest zako binafsi), Badala ya nguvu ya hoja (objectivity).