Nakushukuruni nyote mlochangia mjadala ule. Wameufunga lakini ujumbe umefika. Walopashwa wamepashika mwanamke kupashwa ndo jadi asiposemwa hajifunzi. Kusutwa sunna si mnajua. Mipasho ndo elimu yenyewe, ya vitabuni haitoshi wenyewe mnajua.
Tuwaelimishe wanetu jamani wapate elimu zote kuanzia ya dini, masomo mengine na taaluma mbalimbali lakini tusisahau kuwapa elimu ya maisha wakaja wakajiona kuwa midhali wanaongea kizungu ndio wamemaliza kila kitu, hapana, maisha ni zaidi ya kuongea kizungu. Wanangu nimewapeleka shule ya medium lakini japo wadogo najitahid kuwafundisha kuwa maisha yanahitaji elimu zaidi ya hiyo ya medium, lazima wajue na yale mengine ambayo watoto wengine wanayajua, yalo mabaya waepuke na yale mema wayafatishe. Bakhti mbaya sikujaaliwa wa kike lakini ningekuwa naye ningehakikisha anapata maarifa yote niliyo nayo na yale yanayopatikana katika digirii yote achanganye hapo ndipo atakamilika.
Narudia kukutakieni heri ya mwaka mpya Allah akujazeni yote yaliyo ya kheri na mabaya akuepushieni inshaallah.