Message Memory Full: Sumsung Duos

Message Memory Full: Sumsung Duos

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,863
Habari zenu wanabodi.

Natumia Sumsung Duos, Tatizo ni kwamba, napata alert ya "message memory full".

Nimeangalia available space (SD card) ni 3.68GB, ila system storage ni 17MB.

Nime install app chache sana.

Je! Nawezaje kulitatua hili tatizo?

Je! Nawezaje kuhamisha app kutoka kwenye system storage kwenda SD card.

NB
Nimefuta meseji zote, bado tatizo linaendelea.

Natanguliza shukrani.
 
Mimi pia natumia simu hio hio na tatizo ni hilo hilo mwenye kujua atujuze please
 
Samsung Galaxy Tab 2 (mini tablet) tatizo ni hilo hilo.Nasubiria wataalamu watuelekeze chakufanya.
 
Labda nikuulize mdoa mada, ni Dous ipi manake ziko nyingi, Dous pocket, S duos, Neo Duos n.k

Ila kwa ninavyojua mimi simu nyingi za bajeti (budget phones) zina low internal memory,
mfano Samsung Galaxy Y Duos ina 160 MB as internal memory, hii haitoshi kuinstall apps nyingi.
Fanya hivi:
1. Jaribu ku-clear CASHE MEMORY, BROWSER SEARCH HISTORY na COOKIES ya zile apps unazotumiia mara kwa mara, hii itasaidia kupunguza nafasi kwenye internal memory.
2. Kuna apps zinakubali kuwa installed kwenye SD Card, jaribu kuzihamisha pia, utapata angalau nafasi...

Wengine watatatoa options zingine.
 
Eli79
Asante sana.

Natumia Galaxy Y Duos. Nili clear cache. Tatizo bado liliendelea.

Naomba muongozo wa kuhamisha App kwenda kwenye SD card.
 
Last edited by a moderator:
Hizo simu feki.. me pia nilipatwa na hilo tatzo, nikafanya kila njia lakini wapi. Find another phone.
 
Eli79
Asante sana.

Natumia Galaxy Y Duos. Nili clear cache. Tatizo bado liliendelea.

Naomba muongozo wa kuhamisha App kwenda kwenye SD card.

Ili kuhamisha apps toka Internal storage kwenda SD Card jaribu kufanya hivi;

Kwanza unatakiwa kuifanya SD Card as a Primary Storage ya device yako..ili kufanya hivyo
Nenda Menu -> Settings -> Storage -> Primary Storage, alafu bonyeza pale then chagua kati ya SD na Internal
Ukishafanya hivyo device yako ita-restart kuruhusu SD Card ku-function as a primary storage

Baada ya hapo nenda tena Settings ->Apps -> then angalia apps moja moja,
mfano: bonyeza skype, utaona options za Force stop, Uninstall, Clear Data au Move to Sd Card
Then bonyeza , move to SD Card na mchezo umeisha
Kama option ya Move to SD Card haifunction, manake hiyo app huwezi kuihamisha.

Jaribu mkuu!
 
Back
Top Bottom