Message from Juma Mwapachu

Hivi anadhani sisi wapiga kura hiyo lugha yake tunaielewa, katusomesha?

Lowassa ni Fisadi na hatakaa aache ufisadi.

Ili uaminike naomba angalau kidogo tu uniwekee hapa Ufisadi wa Lowassa na amelitia hasara Taifa la Tanzania kwa upotevu wa fedha kiasi gani, maana tulishuhudia Basil Mramba na Yona wakihukumiwa kwa kosa la kulisababishia hasara Taifa sasa kwa Lowassa naona mnajikalilisha tu kuwa ni fisadi lakini sijawahi kuona sehemu yeyote mkiorodhesha ni nini alichokifisadi.
 
Huna adabu wewe..kwani kizungu ndio kusomaa?CCM imewashika pabaya sana...mtakunya hadharani sasa


#Kama wewe ni msomi Tanzania, ni LAZIMA ujue kiingereza. Ila kujua kiingereza tu pekeake hakukufanyi uwe msomi.

Kwa Tanzania, elimu ya msingi pekeake ndio hutolewa kwa kiswahili isipokuwa kwa somo moja tu la kiingereza. Kwanzia sekondari mpaka chuo kikuu, elimu hutolewa kiingereza!

Kwahio basi kama wewe ni msomi Tanzania, ni LAZIMA ujue kiingereza. Ila kujua kiingereza hakukufanyi wewe uwe msomi.
 
he is a fat cat writing to fat cats. can he be another old wieldbeast seeking green pastures? may be but he seems to be in perpetual green grasses. hiyo kizungu yake wala hakuna atakayemuelewa.
 
To hell with your idea dude, ila RAIS ana inspire mfumo, that is simple and clear regardless of sijui manifesto!
It is not my IDEA it is the reality. Rais anaingia ameshaandaliwa manifesto. Kazi ya Rais tu ni kufanya management ili kuhakikisha yaliyomo kwenye manifesto yanatimizwa. Kwa taarifa yako, jua pia kwamba kuichagua CCM ni kuendelea na katiba mbovu iliyopitishwa na CCM, ambayo itaiongoza nchi hii for the next 50-100yrs. So this election is not really about Lowassa or Magufuli for me and every other sane Tanzanian, its about the bigger picture, the future of our beloved Tanzania!
 
he is a fat cat writing to fat cats. can he be another old wieldbeast seeking green pastures? may be but he seems to be in perpetual green grasses.

He used to be in perpetual green grasses then but not now sir.
 
Sure, kinachoumiza kwetu ni kwamba yanakuwa maumivu ya upande mmoja, tunazuga kulalamika wote ila wengine wanalalamika kinafiki. Wakiwa ndani mwao wanatucheka jinsi wanavyotutumia kujineemesha wao.

Ila hamna jinsi; hatuwezi ishi bila kuwa na viongozi. Swala la kuwapa nafasi za kujineemesha, hilo halikwepeki. Kwahio pamoja na kujineemesha kwao, wafanye kazi zionekane kwa taifa kusonga mbele. Sio kujimeemesha tu halafu tunapiga marktime!
 

Huhitaji kuamini kutokana na mimi ninachokwambia, Lowassa alipokuwa CCM tulishuhudia wapinzani maarufu wanamwita fisadi, akawekwa kwenye list of shame, ambayo mwanasheria wa chama alikiri kwamba alihusika kuiandaa na hawajakosea. Dr Slaa amewahi kufunua taarifa nyingi sana za ufisadi wa Lowassa kwenye kampeni za ubunge wa Nasari, sisi wenyewe humu tumeongea sana juu ya mali za Lowassa zisizo na majibu ya mahali zilikotoka.

Lowassa alikuwa CCM, CCM haina taratibu za kuwawajibisha mafisadi kwa sababu utajikuta unawajibisha chama kizima, Lowassa kutoshtakiwa haimaanishi eti siyo fisadi, tumeona kesi za EPA, Escrow, Ndege ya Chenge etc, kuna watu kibao walibainika kuneemeka na hawakuchukuliwa sheria, je tutasema ile siyo rushwa wala ufisadi?

Sikukatazi kumpenda Lowassa, lakini pia nakushauri tu kwamba pamoja na mapenzi uliyonayo kwake bado Lowassa ni mwizi, ni fisadi na hatakaa aache, hili liko wazi.
 
Andika kiswahili basi; umekula pesa zetu za nchi bure leo unakuja na swa-english yako. Tunakusihi utupishe. You are too old to learn new tricks of today's politics!
 
Asante kwa kumpa elimu huyo. Halafu ndo huyu anashabikia Mafisiem tena kwa mapovu!!
Yaani mwaka huu its now or never.
Ukiangalia supporters wa CCM either wamelishwa na mfumo au ni maskini wasio na elimu wanashawishika kirahisi sana.
Tizama hata mikoa inayoongoza kusupport CCM, the poorest regions of Tanzania!
 

Mkuu mimi najua nitampa kura yangu Lowassa kwa vile tu sina pa kuipeleka, siwezi kuwapa CCM kamwe, hata maiti yangu haitawapa CCM kura.

Lakini pamoja na yote, Lowassa nampa nikiwa najua jamaa ni fisadi, hajaokoka na hataokoka, nawapa UKAWA nikiwa najua Mbowe ni mpigaji, hana uchungu wowote na hii nchi.

The main hope niliyonayo ni kwamba kama CCM itaondoka, kuna siku tutakuja kupata chama kitakachotuondoa kwenye huu umaskini, tutakuja kupata mtu mwenye mapenzi ya kweli kutuvusha hapo baadae, lakini siyo huyu Lowassa.

Hivi tuulizane maswali, kama Lowassa angesimamishwa na CCM, je sisi wapinzani tungeweza kukubali utetezi wa Richmond ni ya Kikwete? Tungeweza kukubali eti ugonjwa wake siyo tatizo? Tungeweza kusema Lowassa siyo fisadi na kumwondoa kwelye list of shame?

Tukiweza kuishi na upinzani tutaweza kuishi na upinzani huko mbeleni; hii ndo point pekee inayonisukuma kuwapa upinzani, ila upinzani huu hauendi kuleta mabadiliko yoyote kiuchumi na kiutawala, isipokuwa mabadiliko ya vyama na viongozi tu.
 
Ila hamna jinsi; hatuwezi ishi bila kuwa na viongozi. Swala la kuwapa nafasi za kujineemesha, hilo halikwepeki. Kwahio pamoja na kujineemesha kwao, wafanye kazi zionekane kwa taifa kusonga mbele. Sio kujimeemesha tu halafu tunapiga marktime!

Mkuu matatizo tuliyonayo ni sawa sawa na matatizo waliyonayo mataifa mengine mengi yaliyo chini ya jangwa la Sahara, viongozi wetu ni wabinafsi, ni wachoyo na ni watu wasiojali kamwe.

Leo anaingia uongozi tukiwa tunasema ni msafi, kesho anachafuka.

Sasa ukiangalia uchaguzi tulionao kipindi hiki, wagombea tayari wamechafuka kabla ya kupewa madaraka, unadhani watasafishika wakiingia madarakani?
 
Kama ambavyo hujui maana ya ufisadi wa kutenda na kusadikishwa..

Mkuu elimu haina mwisho, ni muhimu kufundishana vitu kama hivi kwa sababu vinasaidia kufanya maamuzi makini.

Unaweza kunijulisha hizo tofauti?
 
Kwani huyu baba Mwapachu hajui kiswahili, kila siku anaandika kiinglish

Mwapachu ana watu anao walenga katika jumbe zake. Kwahiyo amechagua hadhira ya kuwasiliana nayo.
Kabla hujafungua Uzi na kuutolea maoni usome halafu jiulize kama wewe ni mhusika ama la. Kujua kama wewe ni mhusika jitathimini kama umeelewa lugha na maudhui ya ujumbe husika
 

Mkuu, kupata kiongozi msafi ni ngumu sana.. mimi huwa naamini: as far as tunaowachagua ni binadamu tu, basi hamna kiongozi msafi.. hawa tunaowaona wasafi (kma wapo) ni kwamba tu hatujui their other sides. Hatuchagui malaika.

Kujaribu ni sayansi. kujaribu mabadiliko ni sayansi ya maendeleo. By Horace Byatt.
 

Mimi ni bodaboda na mke wangu ni mama ntilie umeandika kimasai au nisaidie ni lugha gani umetumia kwasiliana na sisi wana UKAWA wenzako? Lakini nimeona neno moja umeandika neno stupid maana yake wewe ni mpumbavu au?
 

Mkuu wangu ikiwa tangu enzi ya Mwl...Nyerere huyu ndg alikuwa anaiba imekuwaje akaachwa bila kupelekwa Mahakamani manake unaungana na wanaoikataa CCM kwamba inaelea WEZI nahawastahili kupewa muhula mwingine sini afadhali huyu 1alietoka manake anakuja kusimamia Sera ya CDM sio CCM khs SLAA mkuu wangu zamani tulipokuwa tunatoka mishipa ya Shingo kuwaaminisha watu kwamba Slaa angeweza kushinda uchaguzi nilikuwa sielewi kwanini tulikuwa tunachekwa ila baada ya EL kuja UKAWA ndio nimeelewa kung'oa Utawala uliodhani kuwa unahatimiliki nahii NCHI sio kazi nyepesi hebu nambie jinsi hii Game ilivyotaiti na CCM wanavyopambana kutumia hadi senti yao ya Mwisho nivipi Slaa au Lipumba angeweza kushinda uchaguzi....Ila Mara hii mshindi wa uRAIS atapatikana kwa KURA sio kwa BEI yake nahii ndio inawaliza CCM cz El aliitaka hiyo nafasi miaka mingi nahana njaa watampa nini ili akubali so mkuu ndio maana JK anahangaika....so nikwambie jambo 1 tu ndg Lowasa akishinda NCHI hii itasogea sana kuliko akishinda Magufuli...watu wanamsifia kwa Jazba zake lkn uRAIS nizaidi yakukariri km za Barabara mbovu alizojenga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…