Nimesoma mawazo ya wengi kwenye thread hii,nabaki katikati.
Binafsi siwezi kuwa-support westerners (hasa Wamarekani) kwa kuwa lengo la kumtoa Gaddafi ni sahihi kwa some extent lakini means wanazotumia za kutumia military approach siyo sahihi.
Pili,nakubali kweli Gaddafi ameisaidia nchi yake kama mwananchi yeyote anavyopaswa kutoa mchango kwa nchi yake.Nampongeza kwa kutimiza wajibu wake
Nakataa anaposema amewapa wananchi nyumba,huduma za afya na vitu vingine bure,hapana hakuwapa na wala hakuna mtu anayeweza kuwapa wananchi vitu kama hivyo bure kama source ni income kutoka kwenye nchi yao,ni vyao!
Lakini unaposoma speech yake ndani kuna maneno ambayo kweli yana-touch,yanaumiza na kutia huruma kama binadamu.Lakini,nayafananisha na ndoano ambayo huwa imezungukwa na chambo kinachoonekana kizuri ila dhamira ya ndoano ni mbaya tu siku zote..Amejinasibu na dini anapozungumzia suala la Libya kama Nchi,wajiweke wapi Walibya ambao siyo dini yake??Haiwezi kuingia akilini mtu anapong'ang'ania kukaa madarakani zaidi ya miaka 40,aliitoa nchi toka sehemu moja akaifikisha sehemu nyingine nzuri-kwa nini ang'ang'anie kuendelea kuwa madarakani?Lakini anapofanya mapato ya Nchi yatumike kwa manufaa ya familia yake si haki kwa Walibya hata kama kuna vitu wanapata bure toka serikalini,tendo zuri haliwezi kulifanya tendo baya lisionekane kwa ubaya wake!!
Kama Waafrika tuna vingi vinavyotugawa na kamwe hatuwezi kuwa na umoja lakini kubwa kuliko yote ni Dini ambazo tumerithi toka kwa wageni-wenye asili ya dini hizo wamezitumia kwa maslahi yao binafsi wakikaa juu ya migongo ya dini hizo,nasi tumekubali kumeza hadaa hiyo!
.