Uko sahihi Abdulhalm, kuwapa wananchi vitu bure, ambovyo actually siyo vyake yeye kama anavyotaka tuamini hivyo, wakati huku akifanya familia yake ndiyo watawala wa nchi ya Libya ni kosa lake kubwa sana. Kuwanyima watu uhuru wa kuongea, kuwaita wenye mawazo tofauti na yeye kuwa ni vibaraka wa nchi za ulaya na USA, kuwatusi kwa kila aina ya matusi anayo yajua siyo halali yake.
Kumpindua mfalme wa nchi hiyo na yeye kutaka kuongoza kama mfale mpaka afe na kumkabidhi mmoja wa watoto wake uongozi wa nchi ni dharau kwa wananchi wengine wote wa Libya. Alikwa na opportunity kwa miaka kadhaa ya kubadirisha style ya uongozi wake kutoka huu wa kiimla na kuleta uongozi shirikishi/kidemokrasia lakini ameeishia kulewa madaraka na kujiita The King of Kings.
Awe tayari kuvuna aliyopanda