Meseji ya mauaji ya Barlow yanaswa

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kutoa taarifa ya awali ya uchunguzi wa mauaji ya kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa ajili ya kutekeleza mauaji hayo imenaswa.

Kamanda Barlow aliuawa usiku wa manane alipokuwa akitoka kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake. Alifikwa na mauti hayo baada ya kupigwa risasi akimsindikiza Mwalimu Doroth Moses.

Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya makachero jijini Mwanza zinaeleza kuwa, ukweli wa mauaji hayo umebainika na kwamba watuhumiwa waliokamatwa wanahusika moja kwa moja na mpango kamili wa mauaji hayo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa Kamanda aliuawa baada ya mmoja wa wahalifu aliyekuwa akikabiliwa na kesi nzito (jina tunalihifadhi) kutoa kiasi cha fedha kupitia kwa mtu wake wa karibu ili kutekeleza mpango wa mauaji ya kulipiza kisasi.

Kupatikana kwa wauaji hao, kumetokana na simu ya Mwalimu Dorothy Moses kupitia ujumbe wa simu aliokuwa akiwasiliana na wahusika.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lilian Matola alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema taarifa siyo za kweli na kusisitiza kwamba taarifa aliyoitoa DCI Robert Manumba ndiyo sahihi
 
Nyie mnazungumzia polisi na wahalifu?yule mama hamjamwona nini jamani?mi mawazo yote ni jinsi ya kumpata yule lulu wa kamanda barlow ili ikibidi nimuwekee ndani,fanya mchezo na ile jicho?
 
Tanzania kuanzia kura mapaka mswala muhumu yote ni uchakachuaji, so hakuna ninachoweza kuamini siku hizi. ile riport naona kama kuna kitu kinafichwa. Wale walikuwa wanamsubiria kamanda pale bana. Mchongo mzima ushafichwa Mtanzania ameshapumbazwa.

haya tusubirini mengine tusahau hili kama tulivyosahau ya Ulimboka. Hii ndo bongo bana
 
Inamaana hao wauwaji walikuwa wakiwasiliana na Doroth kwa ujumbe mfupi kwenye simu yake ili kutekeleza mpango wa mauaji.
 
Polisi kama hawajamaliza upelelezi wao si wakae kimya mbona kila siku habari ni mpya.Nasikitika wanavyojita makachero wakati taarifa zao zinavuja kabla hawajazifanyia kazi.
 
Tusubiri tuone mwisho. Walivyoapa kulipiza kisasi, watanaswa hata wasiokuwemo. Hiyo ndiyo polisi ya bongo bwana, inachagua mambo ya kuyashughulikia.
 
Inamaana hao wauwaji walikuwa wakiwasiliana na Doroth kwa ujumbe mfupi kwenye simu yake ili kutekeleza mpango wa mauaji.

kwa hiyo mwalimu dorothy nae anahusika?

Hapana hausiki anaposema kupitia simu ya dorothy wanamaanisha ni Handset tu kumbuka wale so called majambazi walimnyang;anya simu wakatupa line kwahyo walichomeka line yao(hapo ndio walipokosea) so kupitia line yao iliyochomekwa kwenye simu ya mwalimu dorothy ndio ikawa rahisi kufatilia hyo namba(iliyochomekwa kwenye simu ya mwalimu dorothy) ndio wakagundua hizo message,umeelewa?
 
huu ni usanii mtupu sidhani kama hizi taarifa ni kweli maana polisi ndio wanajua ukweli wa hili jambo vizuri sana na wala sio huu uvumi
 
Hapana hausiki anaposema kupitia simu ya dorothy wanamaanisha ni Handset tu kumbuka wale so called majambazi walimnyang;anya simu wakatupa line kwahyo walichomeka line yao(hapo ndio walipokosea) so kupitia line yao iliyochomekwa kwenye simu ya mwalimu dorothy ndio ikawa rahisi kufatilia hyo namba(iliyochomekwa kwenye simu ya mwalimu dorothy) ndio wakagundua hizo message,umeelewa?

Naomba unieleweshe... Hivi kuna uwezekano wa kufatilia handset ya mtu bila Kujua IMEI ya handset yake? Na Kama sivyo, Inamaana polisi walikuwa na IMEI ya handset ya Mwalimu Dorothy b4? kama walikuwa nayo huoni kulikuwa na dalili ya kumtilia mashaka ndo mana wakamfatilia?
 
acha kudanganya umma kwa kubuni vihabari visivyokuwa na ukweli.mmekwisha danganya watu sana kuhusu tukio hili nadhani ungepeleka habari hii kwenye magazeti ya udaku.
 
kisa cha mapenzi anabambikwa mtu kesi zisizo muhusu, wanaesema amekamatwa dar (lamada hotel) ni baba nyumba (hawara) wa mwalimu dorothy, inshort ndio aliyekuwa anamtunza dorothy. sasa wameamua kumbambika kesi zote za ujambazi mwanza. wakubali tu yale yalikuwa malipizi as hakuna kitu kinachoboa kama kumuhudumia mwanamke alafu mwingine anajifanya yeye ndio kidume.
 
Naomba unieleweshe... Hivi kuna uwezekano wa kufatilia handset ya mtu bila Kujua IMEI ya handset yake? Na Kama sivyo, Inamaana polisi walikuwa na IMEI ya handset ya Mwalimu Dorothy b4? kama walikuwa nayo huoni kulikuwa na dalili ya kumtilia mashaka ndo mana wakamfatilia?

kukuelewesha tu IMEI unayotumia wewe ipo kwenye database ya mtandao wako unaoutumia,kuipata imei yako wanatumia namba yako kuangalia kwenye system na kupata informations zako,swala la kwanza katika upelelezi wowote ni simu,mtu yeyote akipata matatizo kama hayo swala la kwanza kuangalia ni cm,kwakuwa wale wezi waliiba simu so ilikua rahisi sana kuwapata,IMEI ya Mwalimu hawakuwa nayo maaskari b4 bali waliifatilia kwenye kampuni husika ili kupata imei hili iwe rahisi kuwakamata hao majambazi.....
 
Naomba unieleweshe... Hivi kuna uwezekano wa kufatilia handset ya mtu bila Kujua IMEI ya handset yake? Na Kama sivyo, Inamaana polisi walikuwa na IMEI ya handset ya Mwalimu Dorothy b4? kama walikuwa nayo huoni kulikuwa na dalili ya kumtilia mashaka ndo mana wakamfatilia?
uwezekano wa kujua imei upo, napopiga simu au kutuma message kuna info zinakuwa captured from my handset including imei na mnara unaonipa mawasiliano. so baadaye hata mtu akitupa line yangu na wakasearch mawasiliano yangu watajua imei yangu, watatumia imei hiyo kujua ni nani anatumia hiyo handset kwa sasa.
 
Duh! Kwa hali ilivyokuwa na ushahidi wa awali wa kimazingira ilionekana kuna mkono wa polisi ktk mauaji ya Barlow.

Ila naona wamekwisha chagua mbuzi wao wa kafara......lazima watu waumie. Kila mtu na Mungu wake sasa
 
Back
Top Bottom