VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Siwezi kuamini.Kweli Tume iliyosheheni Wasomi wa Sheria wabobezi inaweza kucheza mchezo mchafu kama huu?! Ni hivi,leo asubuhi nimepokea ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi. Ujumbe ( ingawa siwezi kuukumbuka neno hadi neno kwakuwa niliufuta haraka kwa woga mkuu) unanifahamisha kuwa nijiandae kwenda Mafia kutetea msimamo wa Tume juu ya Maoni ya Katiba. Sehemu ya Ujumbe huo unasema ifuatavyo : 'tuna taarifa kuwa wewe ni mzaliwa wa Mkoa wa Pwani'.
Ujumbe ukaendelea:'Wilaya yako ya Kibaha haipo kwenye orodha ya Wilaya za mwanzo kukusanyiwa maoni yako ya Katiba. Kwa kuzingatia umuhimu na weredi wako wa kisheria,tunakualika uambatane nasi kwenda Mafia kwa ajili ya kushiriki kwenye Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba Mpya. Utafanya hivyo tena Wilayani Kibaha. Tutakuwa na Kikao cha uelekezi tarehe....' Nilipofika hapo nikaufuta na kuanza kulia. Nikachanganyikiwa hadi kusahau kuitunza nambari ya aliyenitumia ujumbe.Wakinikumbusha,nitaiweka nambari hapa jamvini. Nisameheni kwa 'kupanic' kwangu...
Nashindwa kuamini na kuendelea kuandika habari hii. Kwakweli nimelia sana asubuhi ya leo. Kumbe watoa maoni wa Katiba Mpya ni Mamluki? Maoni yenyewe kumbe sio huru na ya haki.Hapa tulikofikia,inahitajika v... au? Sina imani na chochote juu ya lolote la Serikali na Tume.Kamwe...

Ndio kwa maswali yote mawiliJe ni kweli wewe ni mzaliwa wa Pwani? je wewe umesomea sheria? tuanzie hapo kwanza
Utaendelea na msimamo wako nikija na ushahidi Mkuu?Kahawadithie watoto wenzako huko !!! Wacha kuipaka matope Tume ya Katiba, sio kila kitu ni cha kupinga. Yaani utaelekezwaje kwenda kutoa maoini Mafia ilihali wewe sio mzaliwa wa hapo Mafia ? Watu wa Mafia hawatakuona kuwa wewe sio mkazi wala mwenye asili ya huko. Halafu kwa nini umelia, kwani kuna vitisho vya kukudhuru hapo ? Kama unapewa ajira ya muda, mbona ungeenda halafu uje usaidie kufichua hiyo hujuma. Sasa ni-PM namba yako niangalie kwenye server kama umetumiwa sms ya namna hiyo !!!
Ndio kwa maswali yote mawili