Meseji hii kwa mume au kwa mke... Ungefanyaje?

Meseji hii kwa mume au kwa mke... Ungefanyaje?

Mommadou Keita

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
230
Reaction score
238
Jana nilikuwa kazini, nikiwa bize na shughuli zangu ghafla ikaingia meseji katika simu yangu, bila ya kuwa na wasiwasi nikaifungua na kuanza kusoma: kwanza namba ilikuwa ngeni kwangu, pili maneno yaliyoandikwa yalikuwa makali sana yalisomeka hivi:

" Plz naomba unisaidie kwani kesho ndiyo nafanya field, niko chini ya miguu yako na hayo makalio unayotaka nitakupa ingawaje mwenzio sijazoea, kwani sijawahi kufanya hivyo hata mara moja, kumbuka miye ni yatima na hatima yangu iko mikononi mwako, naomba nisaidie tafadhali..."

Nilishtushwa sana na ujumbe huo, karibu yangu alikuwepo rafiki yangu aitwaye Bitilanga, nikamwonesha ujumbe huo akaonekana kudharau na kuniambia kuwa hata yeye alishawahi kutumiwa ujumbe kama huo. Mfanyakazi mwingine wa kiume akasikia maongezi yetu na Bitilanga akasogea, naye nikamwonesha.

Huyu mfanyakazi ananishauri kitu, akaniambia nimpigie huyo aliyetuma labda nilikuwa nikimfahamu na inawezekana kuwa nimepoteza namba yake . Pamoja na kukubali hoja yake ya kumpigia lakini nilimwambia binafsi sina tabia hizo za kishenzi kwamba siwezi kumsaidia mtu mpaka anipe 0713.

Nikamtoka nje ya ofisi na kumpigia muhusika, akapokea na maongezi yetu yalikuwa hivi:
Mimi: Nami mwenzangu?
Yeye: Wewe si ndiye uliyepiga simu unamtaka nani?
Mimi: Samahani dada yangu umenitumia ujumbe ambao umenishangaza sana.
Yeye: Miye sijakutumia ujumbe wowote.
Mimi: Sikia basi, ujumbe ulionitumia una maneno mengi lakini miye nitakukumbusha machache.... umesema kesho unataka kwenda field na kunitaka nikutumie fedha...
Yeye: Ayaaaa!
Miye: Maneno mengine katika ujumbe huo siwezi kukutamkia.
Yeye: Samahani kaka Yangu
Miye: Hebu fikiria kama ujumbe huo ungeonwa na mke wangu unadhani angenichukuliaje?
Yeye: Nisamehe kaka yangu
Miye: Nakuomba uwe makini katika matumizi ya simu
Yeye: sawa
Miye: Tena jitahidi kutafuta njia nyingine ya kuweza kumaliza tatizo lako siyo kumkubalia huyo mwanaume hicho anachokitaka.
Yeye: Sawa kaka'angu.
MY TAKE: Wanajamvi hebu niambiieni laiti mke wangu ambaye siku nyingine huwa namwachia simu yangu angekutana na ujumbe huo ingekuwaje, kama hamtakia kunifikria miye hebu jifikirieni na nyie wanaume wenzangu, au wanawake hebu fikirieni kwamba ujumbe kama huyo ndiyo mngeukuta kwa waume zenu, ingekuwaje?
 
Dah kaka pole sana, hata mimi hapa nimebaki midomo wazi hata la kusema sina, ila shukrani kwa kutoa ushauri mzuri kwa uyu dada, ila kama ingewezekana ungemsaidia ili jamaa asije kumla 0713
 
Dah kaka pole sana, hata mimi hapa nimebaki midomo wazi hata la kusema sina, ila shukrani kwa kutoa ushauri mzuri kwa uyu dada, ila kama ingewezekana ungemsaidia ili jamaa asije kumla 0713
Ni kweli na hiyo field alikuwa aende leo, mbaya zaidi sikuwa na fedha za kuweza kumpa nina namba yake sijui nimuulize kama alikutana na jamaa au...?
 
Hebu nitumie mimi hizo namba. Mi mke wangu hana mamlaka na simu yangu. Na akijifanya kuivizia anakumbana na mipasiwedi kibawa.
 
Kweli waswahili walikuwa imara kusema "Dunia hadaa Ulimwengu Shujaa" Dada anauza 0713 kwa matatizo yake...Ndio maana Machangu wengi wanajitetea wamefika pale kutokana na ugumu wa maisha. Na sisi wanaume tuache tabia ya kutumia uwezo tuliojaliwa na mungu kuwadhalilisha binadamu wenzetu wanawake kwa wanaume.... Plz, plz please tunajizolea laana
 
Ni kweli na hiyo field alikuwa aende leo, mbaya zaidi sikuwa na fedha za kuweza kumpa nina namba yake sijui nimuulize kama alikutana na jamaa au...?

aisee! Pole sana mkuu! Lait mkeo angeona pasingekalika hapo!bora ulikuwa kw ofisi! Aisee ila namuonea huruma huyo binti yupo mashakani!
 
Hebu nitumie mimi hizo namba. Mi mke wangu hana mamlaka na simu yangu. Na akijifanya kuivizia anakumbana na mipasiwedi kibawa.
Kwa nini uweke 'mipasiwedi' katika simu yako, unaonekana si mwaminifu kwa mkeo na kwa nini nikutumie uanitaka kwa ajili ya kupata hiyo 0713? hebu nijuze kwanza.
 
Sijui kwanini mimi ni mtu wa mwisho kuamini kama ushenzi huu upo duniani.
 
Siku hizi tabia za 0713 zinasikika sana ..mungu angetakiwa alete ugonjwa special kwa wafoasi 0713
 
Kwa nini uweke 'mipasiwedi' katika simu yako, unaonekana si mwaminifu kwa mkeo na kwa nini nikutumie uanitaka kwa ajili ya kupata hiyo 0713? hebu nijuze kwanza.
Dah! kweli dunia imebadilika, mwezake anaeleza tatizo, mwingine anataka naye apate 0713 hapo hapo....
 
Sijui kwanini mimi ni mtu wa mwisho kuamini kama ushenzi huu upo duniani.
sitaki kukulazimisha kwamba hilo tukio limetokea kweli. ila huo ni ukweli ila sasa sijajua kama huyu mwanamke alikuwa akinitega au alikuwa na tatizo kweli, sina haja ya kuapa kuhusu hilo.
 
Mmmh... Heri yangu mie ambaye sina muda wa kufukunyua simu ya mpenzi/mume..!
 
Dah kaka pole sana, hata mimi hapa nimebaki midomo wazi hata la kusema sina, ila shukrani kwa kutoa ushauri mzuri kwa uyu dada, ila kama ingewezekana ungemsaidia ili jamaa asije kumla 0713
Na hata kama ni mwanachama wa 0713, hawezi kusema na atajifanya hajawahi liwa hiyo ndogo kumbe ni mzoefu....

 
Hayo ni mambo ya utandawazi na utundu wake...
 
Huyo mshamba mpaka anaandika makalio! Kwa taarifa yako sms nyingi za kishenzi kama hizo zinaingia during the day na ukiipata kama huijui no lazima uipige umkanye ama sivyo itatumwa hata usiku na hamna atakayeelewa kuwa ni bahati mbaya ukizingatia maisha yanavyopiga unajikuta nyumbani hujaomba na mnagombanagombana mara kwa mara
 
tabia mbaya tu
hakutakiwi kuwe na siri baina ya wana ndoa
Hebu nitumie mimi hizo
namba. Mi mke wangu hana mamlaka na simu yangu. Na akijifanya kuivizia
anakumbana na mipasiwedi kibawa.
 
Huyo mshamba mpaka anaandika makalio! Kwa taarifa yako sms nyingi za kishenzi kama hizo zinaingia during the day na ukiipata kama huijui no lazima uipige umkanye ama sivyo itatumwa hata usiku na hamna atakayeelewa kuwa ni bahati mbaya ukizingatia maisha yanavyopiga unajikuta nyumbani hujaomba na mnagombanagombana mara kwa mara
Mkuu socialife hapo nimeediti miye maana analiandika neno kama linavyotamkwa mata....
 
Last edited by a moderator:
Nimesikitishwa sana na huyo dada..kama vp naomb unitumie namba zake nimsaidie.
 
Back
Top Bottom