siyoi koroi
Senior Member
- Sep 6, 2016
- 177
- 214
Ni jambo la kusikitisha sana kwa mteule huyu wa Rais kufunga ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya meru.
Leo tarehe 20 february 2017 ilikuwa ni siku ya kikao cha kawaida cha baraza la halmashauri la madiwani wa halmashauri ya meru kikao cha pili baada ya kikao cha kwanza kufanyika tarehe 17 february siku ya ijumaa iliyopita. Kwa mshangao mkubwa baada ya madiwani kufika na wahudumu kuweka majoho tayari ukumbini mkurugenzi aliamuru majoho yaondolewe na ukumbi ufungwe bila Diwani yeyote kupewa taarifa ya kuahirisha kikao.
Huu ni muendelezo wa mambo ya ajabu yanayofanywa na mkurugenzi wa halmashauri ya meru katika kuvunja kanuni za uendeshaji wa halmashauri. Naambatanisha picha na barua ya wito wa kikao cha leo.
Hapa madiwani wamefika ukumbini wakakuta ukumbi umefungwa bila taarifa.