Merkel ashinda tuzo ya Time ya mwaka 2015

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,470
Reaction score
5,144



Jarida la Time limemtaja Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa "Mtu mashuhuri wa Mwaka 2015.

Jarida hilo limetaja mchango wake katika kutatua mzozo kuhusu wahamiaji Ulaya pamoja na mgogoro wa madeni wa Ugiriki kama moja ya mambo yaliyochangia kutawazwa kwake.

Kadhalika, jarida hilo limetaja kuingia kwa Urusi nchini Ukraine.

Bi Merkel ametoa uongozi wa busara katika ulimwengu ambao umepungukiwa, mhariri wa jarida hilo Nancy Gibbs ameandika.

Kiongozi wa kundi la wapiganaji linalojiita Islamic State Abu Bakr al-Baghdadi ametajwa kuwa wa pili, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Donald Trump, anayesaka tiketi ya kuwania urais Marekani kupitia chama cha Republican.
 

Attachments

  • CVyOW2wW4AADdBS.jpg
    50.2 KB · Views: 44
Kilichonishangaza ni huyo mkuu wa IS naye kuwa mashuhuri kwa kushika nafasi ya pili. Dunia ina mambo! Kama ni Bongo ningeamini huyo wa IS ndio wa kwanza., ila kachakachuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…