Mengi atoa mbinu za biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mengi atoa mbinu za biashara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Candid Scope, Mar 25, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amesema kuwa wajasiriamali wanapaswa kuwa na wazo la biashara kabla ya kukopa fedha.
  Alisema hali hiyo huwafanya wajasiriamali hao kushindwa kuendelea kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali.

  Mengi alitoa kauli hiyo jana alipotembelea kampuni ya Mr. Oil Skuvi 141 Ltd, iliyoko Kawe jijini Dar es Salaam ambapo pia alizindua tovuti ya kampuni hiyo.
  “Tatizo la wajasiriamali wengi ni elimu ya biashara. Wengi wanasaka pesa kwanza kabla ya kuwa na wazo la biashara. Ukiwa na pesa, ukakosa wazo la matumizi, pesa hizo zitatafuta matumizi zenyewe. Hapo utaona zinaishia kwenye bia na mambo mengine kwa sababu hukuwa na wazo la jinsi ya kuzitumia,” alisema.

  Source: Tanzania daima
  Mengi alitaja sababu nyingine kuwa ni ubunifu ambapo alisema kuwa wengi hawana ubunifu na ndio maana wanashindwa kuendelea. Kadhalika, Mengi ameiomba serikali kutenga sehemu ya eneo la Tanganyika Packers Kawe, kuwa la viwanda vidogo ili kuwawezesha wabunifu wadogo kuendeleza ujuzi wao.

  Kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1995, inatengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia vyumba kama samani yakiwemo madawati, meza, vitanda, mageti pamoja na kunyoosha magari. Kuhusu kudhibiti mapato, alisema, “Watu wengi hawajui ni wakati gani wa kudhibiti biashara, wanajibana wakati mapato yanaposhuka…lakini wakati mzuri wa kudhibiti biashara ni wakati pato linapokuwa zuri, mapato yakiwa juu ukaweza kudhibiti biashara hata ikiyumba hautatetereka.

  “Ningeomba mdhibiti matumizi wakati biashara inapaa,” alisema.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mr. Oil (141) Ltd, Laibai Kallaghe, alisema lengo la kuanzisha kampuni hiyo ni kuhamasisha vijana kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi na biashara mbalimbali.

  Kallaghe alifafanua kwamba kampuni hiyo imekuwa ikiwafundisha vijana kazi za ufundi, elimu ya ujasiriamali, elimu ya biashara, utunzaji wa kumbukumbu, upangaji wa bei na utafutaji wa masoko.
   
 2. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Thank you Sir!.
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nice info nimepata elimu kuwa na wazo la biashara kabla ujakopa na kubana matumizi wakati biashara inapaa
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,266
  Likes Received: 19,396
  Trophy Points: 280
  business plan first
   
 5. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Je na pesa hiyo inapatikana au ndo unaelezwa lete Plan yako ukiiwakirisha uatasikia lete wadhamini,ukiwafikisha,onyesha Fixed asset,
  SASA HAPO JE.?
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  business idea first
   
Loading...