sokolaboro
JF-Expert Member
- Dec 1, 2011
- 313
- 54
Mweyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP amewataka viongozi wa dini ya kikristo kuacha malumbano ya nani achinje.
Ili tuendelee na amani tuliyokuwa nayo..amewataka kuacha utaratibu uliokuwepo ili kuendelea kuwa wa moja kama kawaida..
Breaking news Eatv..
Kwa nini amani iondoke mkristo akijichinjia kitoweo chake anachokula yeye na watoto wake na wakristo wenzake? Nani anaiondoa amani mkristo akijichinjia kitoweo chake, je, ni serikali au Waislamu au Wakristo wenyewe, ndio wanaiondoa amani hapa Tanzania wanapojichinjia vitoweo vyao?
Mengi sio msemaji wa wakristo , amezungumza mawazo yake ; Maaskofu wa Wakristo wote T anzania wameshasema, wameshatoa Matamko yao juu ya kuchinja. Wao ndio wanaoijua dini yao, wamesomaTheology, wanayajua yale wanayosema na wanayasimamia. Mengi hakuzungumzia Biblia inasemaje, wala ukristo unasemaje ; yeye amezungumzia utamaduni. kuna tamaduni ambazo kwa sasa zinaachwa ingawa tulizizoea, kama vile kukeketa, na chama kimoja cha siasa.
Katika hili waislamu hawana haki yoyote kisheria wala kikatiba katika nchi hii ya wao ku monopolize uchinjaji wa wanyama kwa ajili ya kitoweo. kama kuna mtu yeyote anaijua sheria ya uchinjaji aiweke hapa.
Sheria ya uchinjaji hapa kwetu Tanzania inaruhusu mifugo kuchinjwa kwa imani za dini za walaji. Kwa hiyo Viongozi wa kitaifa wasimamie katiba waliyoapa kuilinda, na kuwaacha watu wajichinjie wanavyotaka kwa imani zao.
Waislamu wamedai kwamba wao wanapokuwa wanachinja huwa wanafanya ibada kwa Mungu wao.
Wakristo wamekataa kushirikishwa kwenye ibada ya waislamu. kwa kuwa sheria inawaruhusu kujichinjia, serikali isiwe na kigugumizi cha kutamka sheria na katiba kwamba inawaruhusu watu wote kujichinjia vitoweo. Inaruhusu Wakristo, Wapagani na waislamu na wengine wa dini zingine.
Kila mtu asimwingilie mwenzake anapojichinjia, kama kachinja mkristo nawe muislamu hauli vilivyochinjwa na mkristo usile haulazimishwi, WAACHENI WAKRISTO WAJICHINJIE KAMA MNATAKA AMANI KAMA HAMTAKI ENDELEENI KUWAZUIA NA WAO WATAENDELEA KUJICHINJIA KAMA WANAVYOFANYA SASA HIVI.
Amani haiondolewi na kuchinja au kutokuchinja, amani inaondolewa na serikali inapoacha kusimamia sheria zake na watu wanapoacha kutii sheria za nchi.
Kwa nini mnataka mkristo ndiye awe mvumilivu kuchinjiwa na wengine wasiwe na uvumilivu huo. Na kwa nini ulazimishe kumchinjia mwenzio kitoweo chake?