Mengi ataka wakristo waache waislam wachinje!

Mengi ataka wakristo waache waislam wachinje!

Status
Not open for further replies.

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
5,597
Reaction score
1,016
Mweyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP amewataka viongozi wa dini ya kikristo kuacha malumbano ya nani achinje.

Ili tuendelee na amani tuliyokuwa nayo..amewataka kuacha utaratibu uliokuwepo ili kuendelea kuwa wa moja kama kawaida..

Breaking news Eatv..

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mgogoro wa kidini uliozuka nchini kuhusu ya hoja ya kuchinja wanyama ambapo kwa maoni yake alisema hakuna haja ya kuchochea suala hilo kwa kuwa ni miaka mingi tumeishi kwa amani na utulivu na kupendana.

Mwenyekiti wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amewaomba viongozi wa Kikristo kuwaambia waumini wao wenye haki ya kuchinja wanyama ni Waislam na kwamba utaratibu huo usibadilishwe kwa kuwa umekuwapo kwa miaka mingi.

Kadhalika, Dk. Mengi amesema taifa linakabiliwa na mataizo makubwa yakiwamo ya uchumi na elimu na kwamba watu kuzungumzia nani anastahili kuchinja na nani hastahili ni jambo la aibu kwa wakati huu.

Dk. Mengi alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuhoji kwamba ni shetani wa aina gani anayenyemelea Tanzania hadi kusababisha watu kuanza kupigana hadi kuuana kwa ajili ya kugombea kuchinja.

"Anayechinja wanyama kwa matumizi ya umma ni Muislam na hali hiyo imekuwapo miaka mingi iliyopita na hapajawahi kutokea tatizo lolote la uvunjifu wa amani na mtu anayetaka leo kubadilisha utaratibu huu analitia aibu taifa," alisema Dk. Mengi.

Aliwaomba viongozi wa dini ya Kikristo kuwaambia waumini wao juu ya suala la nani ana haki ya kuchinja na kwamba asitokee mtu wa kubadilisha utaratibu huo.

"Huyu shetani katoka wapi na kama siyo shetani hili ni dudu gani ambalo limekumba nchi mpaka kusababisha watu kuanza kupigana kwa sababu ya kugombea kuchinja wanyama?" alihoji Mengi.

Alisema Waislamu wana matatizo yao na Wakristo pia wanayo ya kwao na kwamba hayo ndiyo yasemwe ili yaweze kutafutiwa ufumbuzi wake, lakini siyo suala la kuchinja wanyama ambalo linataka kuota mizizi hapa nchini.

Alisisitiza kuwa suala la nani anachinja lisiingizwe kuwa miongoni mwa malalamiko ya Watanzania na kwamba kuna mambo muhimu yanayowakabili ambayo wanahitaji kuyazungumza.

"Jambo hili siyo la kuzungumza kati ya Waislamu na Wakristo na kubadili jambo ambalo wamelikuta, ni aibu na ni bora liachwe liendelee kama lilivyokuwa awali," alisema.

Kuhusu udini ambao umeanza kujitokeza hapa nchini, Dk. Mengi alisema suala la umaskini wa kipato na uelewa mdogo ni moja ya sababu zinazochangia watu kuyumbishwa na wanasiasa ama viongozi wa dini.

"Maskini ambaye ana njaa na wakati huo huo uelewa wake wa akili ni mdogo ni rahisi kuyumbishwa na kutumiwa bila kufahamu," alisema.

"Udini umeingia Tanzania, tukatae tusikatae, lakini mizizi yake bado haijawa na nguvu kiasi cha kushindwa kuiong'oa na bado kuna nafasi ya kurudisha hali ya amani na utulivu," alisema.

Alisema dhambi ya udini ni mbaya sana kuliko dhambi ya mauti na viongozi wote watakaoshiriki masuala ya kuleta vurugu kupitia dini hawatasamehewa.

Aliomba Mwenyezi Mungu aepushe aina zozote za vurugu zinazoweza kutokea kwa sababu ya masuala ya dini na kwamba ikitokea vita Watanzania hawana pa kukimbilia.


CHANZO: NIPASHE
 
Huyu mzee ni genious..... mimi namkubali.....

Anaelewa kwamba mnyama aliyechinjwa na mwislamu dunia nzima humla lakini madhehebu mengine yakichinja watakula wao tu. Anaelewa universal law ya kuchinja inamwangukia mwislamu. Mzee huyu msomi sana anajua. Acha wale wenye chuki na uislamu waponde lakini ndo kashasema hivyo.
 
Kwani chuki ya nani kuchinja si wamaepandikiza wanasiasa wenyewe? wengine toka kitambo tukiandaa kashughuri, tunamuomba Juma au hasani watusaidi

Umeonae, politicians r dangerous people
 
kwetu mwendo wa kunyoga tu hayo ya kuchinja familia yetu hatuyajuagi
 
Huyu mzee ni genious..... mimi namkubali....

Anaelewa kwamba mnyama aliyechinjwa na mwislamu dunia nzima humla lakini madhehebu mengine yakichinja watakula wao tu. Anaelewa universal law ya kuchinja inamwangukia mwislamu. Mzee huyu msomi sana anajua. Acha wale wenye chuki na uislamu waponde lakini ndo kashasema hivyo.

Basi akiibuka mkristu mmoja kuwasemeav waislamu mnafuraaaahiiii utadhani mmeona biriani na nyama. Mengi is just one person, na sisi hatuwakatazi waislamu kuchinja bali tunachokataa ni kuwa 'ETI NI HAKI YA MWISLAMU KUCHINJA. Mengi angesema tuwaachie waislamu kuchinja japo sio haki yao pekee ningemwelewa!
 
nakuunga mkono mzee Mengi ila waislam naomba watuchinjie na kiti moto ili tuwakabidhi rasim hiyo shughuli.
ilikuwa poa sana kununua kiti moto na nyama ngombe same bucha!

Kwa nini tunapenda sana utani hata kwenye mada nzuri kama hizi jamani?
 
Mweyekiti mtendaji wa makampuni ya Ipp amewataka viongozi wa dini ya kikristo kuacha malumbano ya
nani achinje..
Ili tuendelee na amani tuliyokuwa nayo..amewataka kuacha utaratibu uliokuwepo ili kuendelea kuwa wa moja kama kawaida..

Breaking news Eatv..

Mungu akubariki mzee wangu Mengi maana hekima yako imewazidi wanaojiita maaskofu,hakuna wokovu ktk kuchinja hatujaitwa kuja kulumbana kuchinja Bali kuwaita mataifa kwa Mwokozi Yesu na kutangaza hukumu na msamaha ktk Bwana
 
Kukubali kumaliza malumbano kwa style hii sidhani kama ni sahihi. Style haitatupa nafasi ya kujadili na kutafuta na hatimaye kumaliza kabisa kiini cha mizozo ya kidini hapa nchini. Bado tuna nafasi ya kumaliza mizozo ya aina hii kwa njia ambazo tulijiwekea wenyewe kama Taifa,KATIBA YA NCHI,!

Viongozi walioapa kuitetea na kuilinda katiba yetu wameshindwa kuitumia kumaliza mgogoro huu, na hii ni dalili ya udhaifu. Kushindwa kwao huko hakupaswi kusawazishwa kwa WAKRISTO kukubali yaishe! Kwa kufanya hivyo kutaleta mwanya ya wale wenye nia mbaya ya kutugawa kama Taifa kuja na issue nyingine nyeti zaidi ya kidini, ambayo huenda ikauangamiza kabisa umoja wetu kama WATANZANIA.

Siungi mkono ushauri huo, cha kufanya ni kuishinikiza serikali kusimamia sheria za nchi na kumaliza kadhia hii yenyewe, ili istoe mwanya wa kuchezewa tena huko mbeleni.
 
Basi akiibuka mkristu mmoja kuwasemeav waislamu mnafuraaaahiiii utadhani mmeona biriani na nyama. Mengi is just one person, na sisi hatuwakatazi waislamu kuchinja bali tunachokataa ni kuwa 'ETI NI HAKI YA MWISLAMU KUCHINJA. Mengi angesema tuwaachie waislamu kuchinja japo sio haki yao pekee ningemwelewa!

Huna maana yoyote wewe, penda shari sana wewe, Mimi ni Augustine lakini niko na Mengi 100%
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom