Menejimenti MOI yapigwa msasa utekelezaji Bajeti 2025/26

Menejimenti MOI yapigwa msasa utekelezaji Bajeti 2025/26

Joined
Apr 15, 2025
Posts
91
Reaction score
174
Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepatiwa mafunzo ya utekelezaji bora wa bajeti ya maendeleo ya Taasisi hiyo ya mwaka wa fedha 2025/26 ili kuendelea kuboresha huduma kufikia dira ya taifa ya 2050.

Hayo yalibainishwa Agosti 26, 2025 na Meneja Mipango, Ufuatiliji & Tathimini wa MOI, Bw. Elisha James Sibale wakati wa mafunzo ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 kwa wajumbe wa menejimenti ya MOI.

Bw. Sibale alisema taasisi imejipanga kuhakikisha rasilimali zilizotengwa zinatumika kwa ufanisi mkubwa

“Bajeti ya MOI kwa mwaka wa fedha 2025/2026 imejikita katika uwekezaji wa huduma za kibingwa, tafiti na matumizi ya teknolojia ya kisasa. Hatua hii inalenga kuhakikisha tunachangia moja kwa moja kufikia azma ya Taifa iliyoainishwa kwenye Mpango wa Taifa wa miaka mitano pamoja na kujipanga vema kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 kupitia Mpango na Bajeti utakao andaliwa kwa mwaka wa fedha 2026/2027” alisema Bw. Sibale

Kwa upande wake, Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Bw.Mintanga Milulu, alisema kuwa wizara itaendelea kusimamia na kuhakikisha taasisi za afya zinatekeleza bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa.

“MOI ni moja ya nguzo muhimu katika sekta ya afya, hivyo utekelezaji wake wa mpango na bajeti lazima uendane na dira ya taifa. Wizara itaendelea kutoa usimamizi wa karibu na msaada wa kitaalamu,” alisema Bw. Milulu

Aidha, Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bi. Mary Mshangila, alisema kwamba serikali imeweka mkazo kwenye matumizi sahihi ya fedha za umma, kuhakikisha taasisi zinabaki na uendelevu wa kifedha

“Ofisi ya Msajili wa Hazina itaendelea kuhakikisha taasisi kama MOI zinapata usimamizi bora wa kifedha. Tunataka kila shilingi inayotolewa ichangie moja kwa moja katika kufikia malengo ya maendeleo ya taifa ifikapo mwaka 2050,” alisema Bi. Mary

IMG-20250828-WA0009.jpg
IMG-20250828-WA0010.jpg
IMG-20250828-WA0012.jpg
 
Rais wetu mpendwa, bila kuzungumza uongo au unafiki, huduma za kiafya zimekuwa aghali mno, kuanzia kwenye uzazi wa kina mama, Ile discipline ya wahudumu aliyoiacha mwenda zake yote imekwisha, kazia ufanisi na uone gharama za matibabu zitapunguzwaje, hapa ndiyo chanzo cha kina mama wengi wa hali ya chini aka wanyonge kutokubaliana nawe!,
Pili akina mama Hawa wanyonge, ndani ya shule za msingi wanachoshwa na uchangiaji wa lazima wa shs 1000 kila siku, mtoto akikosa ni viboko vya hasira kali, (kosa la mzazi kukosa fedha adhabu inamuangukia mwanafunzi) inafika mahala mtoto akikosa fedha anaogopa kwenda shule, ni bora abakie nyumbani kuepuka kipigo!, kwa afrika yetu ulezi mkubwa hufanya mama zetu, kwa suala hilo huwachosha akina mama kiasi huo ngeza chuki dhidi yako, kibaya kachakula wapewacho ni vijiko vitatu tu, pia baadhi ya watoto walapo huumwa matumbo kutokana na wakati mwingine chakula kuwa kibichi!,
Mh. Rais wetu, tatua kero hizi za kijamii zinazoumiza zaidi akina mama!.....
OCTOBER TUNA TIKI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom