Meneja EATV kortini kuhifadhi raia wa nje

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WATU wawili akiwemo Meneja Vipindi wa kituo cha televisheni cha East Africa (EATV), Lidya Igarabuza (37) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kuishi nchini bila kibali.

Igarabuza ambaye ni mtanzania na raia wa Kenya, David Wachila (36), ambaye anadaiwa kuwa ni DJ wa muziki katika kituo hicho cha televisheni, walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi, Kwey Rusema.

Wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji, Khadija Masoud alidai kuwa Februari 25, mwaka huu katika maeneo ya Mikocheni A, Wachila akiwa raia wa Kenya, alikutwa akiishi nchini bila kibali jambo ambalo ni kinyume cha Sheria za Uhamiaji. Katika mashitaka yanayomkabili, Igarabuza anadaiwa kumhifadhi Wachila jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Inadaiwa Februari 25, mwaka huu huko maeneo ya Mikocheni, Igarabuza alikutwa amemhifadhi Wachila huku akijua jambo hilo ni kinyume cha sheria. Washitakiwa walikiri kutenda makosa hayo.

Wakili Masoud aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali. Hakimu Rusema aliahirisha kesi hiyo hadi Machi Mosi, mwaka huu. Igarabuza aliachiwa kwa dhamana wakati mshitakiwa Wachila akirudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.

habari leo
 
Kwa mini asipelekwe mahakamani mkurugenzi wa EATV bibi Regina mengi au wanamuogopa maana yeye ndio mwajiri wao! Kama walivyofanya makampuni mengine CEO ndio anakuwa responsible
Wanasema alihuhifadhi kwa hiyo sio kampuni ni yéyé binafsi na kumbuka ni meneger wa vipindi na sio GM au CEO navyoona na maswala binafsi.To be corrected
 
Tena uhamiaji wafanye raid ya kushtukiza tripple 7, Masters club,silver pipe,Kruz inn,escape one, cine club,mbalamwezi na mabaa yote ya mikocheni watakutana nabrai wengi wasio na vibali vya kuishi nchini. Na pale kwa wahindi kwenye disco lao mikocheni kwa nyerere karibu na mohans
 
Naona kumeanza witch hunting Tanzania. Hiyo itatupeleka kubaya. Tayari kuna kiasi kikubwa cha phobia dhidi ya wageni hasa Wakenya. Tatizo hili katika nchi zenye ustaarabu mtu hupewa mwezi hivi arekebishe hali yake ya kuishi nchini. Wala hakuna haja ya yote haya. Nahofia Wakenya wataanza ku-retaliate. Mnaturudisha miaka ya 70 na 80 na hali tuko karne nyingine. Mambo haya yamepitwa na wakati.
 
Kuna jamaa namjua ni mkenya anapiga kazi mahali na bila shaka hada kibali yule, sijui nimchome.....ushauri wadau.
 
Naona kumeanza witch hunting Tanzania. Hiyo itatupeleka kubaya. Tayari kuna kiasi kikubwa cha phobia dhidi ya wageni hasa Wakenya. Tatizo hili katika nchi zenye ustaarabu mtu hupewa mwezi hivi arekebishe hali yake ya kuishi nchini. Wala hakuna haja ya yote haya. Nahofia Wakenya wataanza ku-retaliate. Mnaturudisha miaka ya 70 na 80 na hali tuko karne nyingine. Mambo haya yamepitwa na wakati.
Unapoishi Tz bila kibali two things happen
1.Unaikosesha serikali mapato yake
2.Unemploying the locals maana usikute unafanya kazi ambayo wabongo wanamudu.
 
Kwenye hiyo habari, wanasema washtakiwa wamekiri makosa. Kisha wanataja preliminary hearing. Wanasheria msaada. Nilidhani hukumu I tafuta.
 
Naona kumeanza witch hunting Tanzania. Hiyo itatupeleka kubaya. Tayari kuna kiasi kikubwa cha phobia dhidi ya wageni hasa Wakenya. Tatizo hili katika nchi zenye ustaarabu mtu hupewa mwezi hivi arekebishe hali yake ya kuishi nchini. Wala hakuna haja ya yote haya. Nahofia Wakenya wataanza ku-retaliate. Mnaturudisha miaka ya 70 na 80 na hali tuko karne nyingine. Mambo haya yamepitwa na wakati.

Hivi wewe unadhani ukifumwa huko Kenya unaishi bila kibali utaachiwa? Nenda ujaribu uone kilichomnyoa kanga manyoya.
 
Hivi wewe unadhani ukifumwa huko Kenya unaishi bila kibali utaachiwa? Nenda ujaribu uone kilichomnyoa kanga manyoya.
Kenya wameraisisha uhamiaji kwa raia wa afrika mashariki work permit hulipii kabisa. Afrika moja.
 
Jamani hivi umoja wa Africa Mashariki ndo upo hivi? Mimi ni mtanzania nashauri busara itumike sana
 
wawakamate ndio maana wanataja sehemu za Tanzania ziko kwao lini ulisikia mtanzania anadai sehemu za kenya ziko Tanzania
 
Kenya wameraisisha uhamiaji kwa raia wa afrika mashariki work permit hulipii kabisa. Afrika moja.
mtego huo,wa nipe nikupe,yaani kama kumuhonga demu peremende,akikukubali anakuzalia watoto rundo na shamba analima,wao(kenya) ndo wanashida na tz si kinyume chake
 
Kenya wameraisisha uhamiaji kwa raia wa afrika mashariki work permit hulipii kabisa. Afrika moja.
Wamejirahisishia wao ili waweze kuja kwetu siyo sisi kwenda kwao kwa sababu wao ndiyo wenye kutaka kuja kwetu zaidi ya sisi kwenda kwao.

Wako kwenye uwoga mwingi sana kwa sasa kama tukiweza kusimama kwao itakuwa ni shida kwa sababu sisi ndiyo walaji wakuu wa bidhaa zao nyingi
 
Naona kumeanza witch hunting Tanzania. Hiyo itatupeleka kubaya. Tayari kuna kiasi kikubwa cha phobia dhidi ya wageni hasa Wakenya. Tatizo hili katika nchi zenye ustaarabu mtu hupewa mwezi hivi arekebishe hali yake ya kuishi nchini. Wala hakuna haja ya yote haya. Nahofia Wakenya wataanza ku-retaliate. Mnaturudisha miaka ya 70 na 80 na hali tuko karne nyingine. Mambo haya yamepitwa na wakati.
Haujaelewa mkuu , wana vibali?Nchi inaendeshwa na taratibu
 
Back
Top Bottom