Mene mene tekeli na pelesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mene mene tekeli na pelesi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shenkalwa, Nov 1, 2011.

 1. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tawala nyingi zilizoanguka katika dunia hii toka enzi za mababu ziliangushwa baada ya dalili nyingi kujitokeza zikiwa ni pamoja na watawala kutoshaurika, kujiona wao ni miungu zaidi ya Mungu na kuwanyima watu wao yale wanayoyastahili na badala yake watawala kujipenda wenyewe na familia zao, na marafiki zao na jamaa wa koo zao na kuwaacha wengine wakihangaika na maisha.

  Zaidi sana kuwanyanyasa kwa kuwabambikia makosa ambayo ni ya kutengenezwa ili mradi tu mkubwa mmoja amemchukia mtu fulani. Haya pamoja na mengine mengi ndiyo yanayotokea katika Tanzania ya leo. utawala uliopo madarakani kwa kupitia ccm hebu someni maneno haya: Mene mene tekeli na pelesi
   
 2. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Swadaktaaaaaaaaaa. Mungu ameuhesabu utawala wao umekwisha. Umepimwa kwa mizani nao umepungua kwa sababu wamewatesa watu wa mungu na kuwaongoza ndivyo sivyo. Wameyakumbuka matumbo yao tu. Wamewaibia wajane na wamekula mali za watoto yatima. Elimu na maisha bora ni kwa watu wa nyumbani kwao tu, wananchi wanateseka. Siku zao zinahesabika. Mwisho wao umefika.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,426
  Likes Received: 22,341
  Trophy Points: 280
  CCM ina shingo ya chuma, haisomi wala haielewi alama za nyakati.
  Soon lishingo la chuma litavunjika
   
Loading...