Dear boys dear men... Ni sisi wasichana kina dada mabinti na mama zenu, tunaongea kutoka upande wa chini upande wa pili upande wa mbali kutoka usawa wenu
Upande nilipo msichana kuna hitilafu, so sikio lako thabiti ndio ushindi kwangu
Ninayotaka kusema hapa sio siri katu, ili ujue nina vingi vya kufa kabla ya mwili wangu
Kwa miaka mingi nimeishi gizani, gizani kwenye baridi na miba mingi nyikani
Eneo unalotaka niishi ni eneo kandamizi, na bahati mbaya we ndio mchoraji wa hii ramani
Ramani inayomuonesha binti kama chombo cha mapenzi, msindikizaji na mtoto tegemezi
Ramani isiyojua vituo, isyojua kua tunaweza kuwa marafiki bila kuvuana nguo
Dear boys dear men mngeelewa mngeiweka fikra sahihi, kama sanaa inavyo zalisha fasihi
Mi ni mlezi ukinivika mi umeivika jamii
U gentlemen sio kulipa mgahawani, umeshapitwa na wakati...
hainisaidii kunifungulia mlango nikifika kwenye gari, nifungulie fikra nitafakari...
Dear boys dear men tumekuwa tegemezi maana mmeficha mbegu, nani wakuipigana vita yetu?
Umbali kati yetu utakua mkubwa milele, maana si ni wahanga wa mifumo mliyoiunda wenyewe
Mkijaribu kusoma nabaki bure, maana unaujali mwili wangu ndomana sitaki shule
Kila nikienda popote wanaomba ngono, labda niwe changudoa to the fullest at least i will get paid
Hata sisi tuna life tu, in the world that does revolve around you
Nipo tofauti sikupenda na tena, unaponichezea fahamu kua nazeeka mapema
Shujaa unakumbukwa mzazi sikumbukwi, na kwanini kuwa msafi sio haja kwako?
Au kutembea kifua wazi kwako ni kujiamini, nikitembea mimi ni nusu uchi
I wish ungejua pride yako nayo sumu, i wish ungejua uanaume sio nguvu
I wish ungejua binadamu hajakamilika mwanaume aliyekamilika anatimiza majukumu
I wish ungejua na mimba sio haya, i wish ungejua mwanamke kua kichwa si vibaya
I wish ungejua nao upendo una nguvu mwanamke akimtongoza mwanaume si malaya
I wish ungejua kwenye shafia sometimes haitokei, its okay kulia sometimes
I wish ungejua uongozi hauoni jinsia, si tatizo mwanamke kuongoza njia sometimes
Mifumo mliyoianzisha ina maisha, na chenye maisha kinazikwa
Kwa hiyo kuna siku mwanamke atasimama na vita tunayopigana ipo siku tutashinda
Inasikitisha hamkui kihisia, japo mnakua kiakili
natamani ungejua inauma kuwa namba mbili kwenye kila nyanja
Eagle ni power ila iogope, maana ni upanga unaokata pande zote
Ngome nzuri ngome nzuri haitavuma milele, ukitumia ubabe vibaya utakuvunja mwenyewe
Hadithi ya mwanamke alimshawishi adamu kula tunda iliamdikwa na wewe, sijui delila alichukua nguvu za mumewe akaziuza iliandikwa na wewe
Upande wangu wa hadithi hujaskilizwa pengine hautasikilizwa hasilani, maana ulianzisha shule akasoma mwanaume mwanamke nikabaki nyumbani
Dear boys dear men hamtakaa kwenye kilele, maana kilele ni kuwa mama
Mimi ni kichwa sio wewe, ungekua kichwa mtaani kusingekua na single mothers
Lini mtaacha kutuita mademu? Au labda umuite demu mama yako
Ukiona huwezi naomba uniheshimu maana heshima inaanza kwako, Na haja ya maelewano iko hapo
Amin ipi salama ya kichwa cha familia bila mkono wa kuosha macho
Najua tupo tofauti na tofauti ibataki, itabakia hivyo milele...ila naomba usinichukie nielewe
Dear boys dear men ni sisi wasichana kina dada mabinti na mama zenu, tunawasilisha kutoka upande wa chini, upande wa pili upande wa mbali, kutoka usawa wenu...
Credits: dizasta vina