Men only (inahusu wanaume)

Haya lala atakuletea hapo kitandani.

Kusema hivo sikumaanisha mtu ndo abweteke akisubiria riziki!
Anapaswa kuchacharika na vile vile kumuomba Mungu!

KAMA IPO IPO TU!
 
Ushauri mzuri sana huu kwa wanaume.
Koromeo udumu milele.
Wanaume wa siku hizi baadhi yao wamesahau wajibu wao.
 
Last edited by a moderator:
Itakua umezodolewa wewe roho inauma.

Hapana, sijazodolewa kama ulivyosema. Huu ushauri unawahusu wanafunzi wa vyuoni wenye boom na wahitimu wa vyuo wanaotafta kazi. Imenilazimu kusoma ili nijue inahusu nini kabbla sijakujibu, nimejua inawahusu hao.

Mimi sio mwanafunzi wa chuo kwa hiyo sipati boom wala sihusiki,vile vile mimi sitafti kazi na bahasha na kuchagua kazi. Lakini hii akili ya kwamba usichague kazi niliipinga sana miaka ile namaliza chuo, kwa kweli nilikua nachagua kazi, kazi za kibwege ----- sikutaka hadi nilipokuja kupata kazi niliokua naitaka na sehemu niliyokua naitaka.

Nadhani umenielewa, sijazodolewa kama ulivyosema kiongozi.
 

Mmh haya ni makavu live najua fika kuna watu wanapita kimyakimya na kuachia misonyo mireefu kama utelezi wa bamia lakini habari ndio hiyo
Quinine ni chungu lakini inatibu maralia
 
Wanaume na wasikie, wavulana endeleeni kupiga selfie na majumba na magari ya wanaume, mkikua mje msome hapa.

na kupost picha insta ndo kazi za wavulana..............wao mda wote kiba na domo nan mkali lol..............
 
mada yako ni nzuri ila naona mentality tulio nayo wakati tunasoma ndiohua inatunyima kuthubutu. kila mtu anawaza akitoka chuoni atapata kazi tena nzuri na derva wa kumuendesha. kwa kifup chuoni tunakua hatujajua kitaa kukoje baada ya kusambaza bahasha mwaka bila mafanikio ndo mtu unapata picha ya hali halisi

psychologia ya mtu aliyekosa kazi nadhani anakua anaishi kupitia ndoto kwamba one day yes ndo maana wangi wanashindwa kufikiri nje ya box.

sijawahi kuishi maisha maisha ya kukosa kazi ila nahisi yanachanganya sna. inabid uwe mstahamilivu sana ili kuanza kufanya kazi ambazo wengi wanaamini si za staha. hata hivyo hamna jinsi ili maisha yaende ni lazima ujitoe kupigana kiume haswaaaa tusijali kazi ila tunapozifanya tutumie akili illi kuonesha tofauti kati yako na yule ambaye hakupiga umande

halaf kazi nyingine hata hazihitaji mitaji mikubwa. unakuta mtu anaishi mjini kwa biashara ya chai tu. kazi yake ni kununua mikate na kuipaka blue band usiku asubuhi anabandka sufuria la chai kubwa akiuza mpaka ikiisha ana faida ya kutosha tu. ni wangapi wako tayari kuzunguka na thermos sokoni? inataka moyo sana
 
Tatizo mtoa mada hajatuambia nn cha kufanya....!! Njia za kupitia anatupa lawama tu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…