Men only (inahusu wanaume)

Mkuu umenena watu wanabaki kuilaumu serikali wakati mtaji wameukalia
 
Umeeandika point zenye GB 500 big up bro wambie watoto wazembe wafanye kazi. Sio kudownlord movie mpya na kucheza play station..
 
Shukrani mkuu....
But umewasahau wanaotafuta pesa then wanaishia kuhonga viwanawake...
 
Uzi makini sana huu,kwa mwenye akili ya kujiongeza atapata chochote, sio ku criticize hata hoja za msingi
 
Nikiwa Kama Mchungaji Iyo Imekaa Vzr, Mungu Alipomuumba Adamu Kazi Ya Kwnz Kumpa Ni Kuilima Na Kuitunza Bustani (Mwanzo 2:15). Na Sifa Ya Kwnz Ya Mwanamume Anaestahili Kuwa Mume Ni Uwezo Wa Kufanya Kazi, Nina Libariki Neno Hilo Kwa Jina La Yesu Kristo.Amen
 
Hapo kwenye red mkuu ni ukweli ulio uchi. Jamaa wa aina hiyo kazi ya ni kutumwa na mke(shemeji) wa kaka yake maandazi asubuhi na mchana kutumwa nyanya gengeni vinginevyo hakuna kupewa chai asubuhi wala ugali mchana.
 
Eeeh watu kama wewe mnapaswa muishi maisha marefu ili muendlee kutoa busara zenu kwetu sisi vijana,nmejifunza kitu pia hata kutegemea mshahara wa laki 7 mwisho wa mwez kwa mwanaume nao na uzembe...
 
Safiii! Huu Uzi umetulia,umetugusa vijana wengi wa Leo. Wengi wetu tunajiaminisha ufahari kuajiriwa maofisini, lakini kumbe kujiajiri ni bora zaid! Waweza kupata riziki kwa akili, nguvu na kwa muda wako mwenyewe. Kufanikiwa au kufeli ni utashi wako mwenyewe.
 

Amen...
 

USHUHUDA:

Nikiwa mwaka wa mwaka mwishoni kulitangazwa kuuzwa kwa viwanja vya SALASALA. Enzi hizo unajiona bado mdogo. Unaojiona una mengi ya kufanya kuponda maisha.

Sikuona umuhimu wa hata kufikiria kununua viwanja. Niliwaza kwanza mimi ninataka kuwa na kiwanja kwenye maeneo ya 'low-density' sio vile vya salasala. Nikapuuzia.

Nilikuwa na rafiki yangu aliniambia kuhusu vile viwanja na kuwa yeye alikuwa na mpango wa kununua na alinishawishi na mimi ninunue pia. Mimi sikununua. Yeye alinunua...kwa boom!!!!!!!!!!!!!

Matokeo yake, mwenzangu ameoa mwaka jana...akahamia kwenye nyumba yake. Juu ya hapo, ana mradi wake unamuingizia fedha za kutosha pembeni ya kazi ya kuajiriwa. Mimi ndio kwanza ninahangaika na kununua viwanja na kukusanya pesa za ujenzi...!

Kijana uliyeko chuo sasa hivi, jitahidi kuwekeza. Hata kama sio kwenye ardhi, jitahidi kuwa na mradi yaani hilo boom (au fedha unayopewa na mzazi) hiyo hiyo kidogo itumie izae. Usikae ukafikiri maisha bado. Ulianza kuishi tangu ulipozaliwa, na maisha hayakusubiri ufuje pesa kwanza ndo uanze kujipanga baada ya kumaliza chuo.

Wakati sisi tunamaliza chuo tunasambaza CV kama hatuna akili nzuri, rafiki yangu huyu alikuwa kwenye mradi wake anapiga pesa taratibu. Kazi ilimfuata. Sasa hivi anaweza kusema haishi kwa kutegemea mshahara. Yani kwake mshahara ni kitu tu cha kumwezesha kuchukulia mikopo kukuza biashara zake zaidi.

Ni maisha ambayo kila kijana anaweza kuwa nayo kama tusiposubiri kujifunza kama mimi nilivyojifunza. Usisubiri ukosee wewe ndo ujifunze (Wise is he who learns from others' mistakes).

Amka...jishughulishe! wekeza...anzisha miradi...IT IS NEVER TOO EARLY...!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…