Kumbukumbu nzuri sana...
kulingana na wimbo huo inawezekana miaka hiyo hiyo kabla raia hawajasanuka.
Kuna mwaka mikoa mingine haikupata Mchele sana tulisomba hapo mchele kwa kilo tsh 800/= japo barabara ilitutoa jasho tulipiga pesa....
shukrani kwenu leo sumbawanga mpaka mbeya kuna lami.
Genz zungukeni africa kuna pesa nyingi sana.
Sahihi kabisa.....
Vyakula bei ilikuwa chini sana,,,,Mchele wengi waliufuata mpaka kwenye bonde la Ziwa Rukwa.
Sasa umenikumbusha kipindi tunajenga barabara ya Nzega...Tinde...then Tinde....Maganzo...na Tinde...Isaka,,,Mchele ulikuwa Jelojelo kwa kilo,,nyama ya kondoo tunanunua kwa mapande siku ya jumanne mnadani nayo ni Jelojelo,,,,,na pande lilikuwa linakaribia kilo.
Kambi ilikuwa ni hapo hapo Tinde ingawa kulikuwa na kambi nyingine Maganzo.
Sasa wazungu walikuwa wananunua kondoo kwa wingi...ghafla bei ya kondoo ikawa juu kushinda mbuzi,,,kwa hiyo dili la nyama ya jelo jelo ikapotea....Kampuni ilikuwa ya makaburu Grinaker LTA...
Hapa nimemkumbuka mzee mwenzangu Nyakunga alikuwa Dereva wa Benz Powerliner..mwingine alikuwa Sir Edward au Edward mpalestina naye alikuwa akiendesha Benz poweliner Tiper,,,daah...mwingine alikuwa kijana aliitwa Frank Kamando naye... Benz,,mwingine aliitwa Wabongo RIP huyu alikuwa na sifa ya kukimbia na magari,,,,baada ya mradi alipata ajali mbaya sana,,,akakatika kichwa ....kikapatikana baada ya siku nyingi,,,na siku zote alikuwa akijitamkia kwamba kama akipata ajali hataki kupona anataka kupotea mazima (maneno huumba)...pia nimemkumbuka Major Magere RIP huyu alikuwa Security Oficer wa Kampuni ya Grinaker,,,,kila jioni tulikuwa tunapata naye kikombe chini ya mti kwenye Bar ya dada mmoja (Ester)
Daah,,,nimekumbuka mengi sana Ofisini kulikuwa na kina Bruno dada KHadija( muarabu wa Tinde)...Walter Mhasibu toka sauzi,,nk nk,,,
Kuna kichekesho kilitokea mapolisi walikamata diesel za wizi pamoja na nondo na Cement wakaleta ripoti ofisini na kumtaka project manager Mr.Frank Swift aende kutambua mali hizo za wizi,
Project Manager mwenyewe Zungu la sauzi naye muhuni tu,,,,akawaambia polisi zile mali si za kampuni ingawa diesel ya kampuni ilitambulika kwa kutiwa rangi nyekundu.... lakini mzungu aliikataa katakata....akadai diesel ya kampuni ipo kwenye matank na ndani ya mitambo......pia kwenye magari hiyo nyingine ni ya kwao waichukue,,,,,,,