Membe: Wizi ulipangwa Hazina

ingekuwa ni fedha za shule, maji, barabara....
.
Mkuu Mzee Mwanakijiji malizia basi ... mbona unatupa shida kujua unachotaka kusema? ... Anyway ngoja nimalizie ...

ingekuwa ni fedha za shule, maji, barabara.... wala isingekuwa issue

...... ILA kwa sababu ni fedha za safari! - wameamua kuipa uzito na ku-act haraka na mapema ili bwana mkubwa (Vasco Da Gama) mpenda safari aweze kuendelea na utalii wake! ...

Mambo muhimu na ya msingi hayapewi kipaumbele katika nchi hii ..... Inasikitisha sana! ...
 
Membe ameongea ukweli, wizi ulipangwa na yeye mwenyewe akiwa mmoja wa wahusika, bahati mbaya maofisa usalama wa wizara hawakuhusishwa ndio maana baada ya kuchukua fedha watuhumiwa walikamatwa, hiyo tume iliyoundwa kuchunguza hakuna lolote zaidi ya kuvuta muda tu ili watu wasahau, hakukua na sababu ya kuunda tume kwani watuhumiwa walikatwa, ilitakiwa watiwe ndani halafu upelelezi uendelee. Membe anajaribu kujisafisha, yeye ni muhusika namba moja.
 
re. wizi ulipangwa hazina.
ni hatari kuona kiasi kikubwa kama hicho cha fedha kinatoeka ktk mazingira ambayo maofisa wa serikali wanahusika. ni vyema wangehifadhiwa kwanza(jela) then uchunguzi ikaendelea.
Hivi neno kukaimu naona limemchanganya membe? Sijui unapokaimu majukumu ni yapi na ukomo ni upi? Membe labda ufafanue hili
 
..sasa Membe anahalalisha vipi matumizi ya 3.5 billion kwa ajili ya safari za Brazil,Geneva,na Arusha??

..kwa nchi yenye umasikini kama yetu, viongozi kufuja pesa zote hizo kwa ajili ya safari za nje ni sawa na mtu anayekunywa uji wa mgonjwa.
 
UCHAGUZI UJAO NAGOMBEA URAIS. 3.5 BIL. KWA SAFARI TU? TENA INAWEZEKANA HIZO NI ZA MWEZI MMOJA TU! KWANI WASINGEJARIBU KUCHOTA BILA WOGA WA KUSHTUKIWA. MUNGU WANGU! WAVUJA JASHO TUNAIBIWA BILA HATA CHEMBE YA HURUMA!!!! JAMANI MUOGOPENI MUNGU.
picture-9.jpg

Na Alfred Lucas - Imechapwa 20 June 2012

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema njama za kuiba mabilioni ya shilingi ya safari za Rais Jakaya Kikwete, zilifanikishwa na maofisa wa Hazina.

Amesema maofisa wa Hazina walikiuka taratibu za kutoa fedha kwa wizara yake.


Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jijini Dar es Salaam juzi, Membe amesema anatuhumu watendaji wa Hazina kwa kuhusika na njama hizo “…hawa wanajua taratibu za kutoa fedha kwa wizara yetu.”


Waziri Membe amesema kwa mujibu wa taratibu, mwenye mamlaka ya kuomba fedha Hazina ni waziri husika, naibu waziri, katibu mkuu, na naibu katibu mkuu.


Amesema hata baada ya viongozi hao kuomba fedha, lazima maofisa wa Hazina waende kwa mhasibu mkuu wa wizara husika ambaye atathibitisha iwapo kiasi cha fedha ambacho waziri anaomba, kipo na katika akaunti ipi.


“Sasa kilichofanyika hapa, ni kwamba waliokuwa wanakaimu nafasi walifanikiwa kutoa fedha hizo benki. Jambo tunalojiuliza ni nani aliidhinisha fedha hizo kutolewa Hazina?” alihoji Membe.


Membe amehoji, “Waziri wanamfahamu, naibu waziri, katibu mkuu na naibu katibu mkuu wote wanawafahamu. Wao ndio wataalamu wa fedha, wanafahamu taratibu za utoaji fedha; ilikuwaje wakatoa fedha kiasi kikubwa kama hicho bila idhini ya wale wanaowafahamu kuwa ndio wenye mamlaka?”


Amesema wakati fedha hizo zinachotwa, hakuwapo. Naibu Waziri, Mahadhi Juma Maalim hakuwapo; pia Katibu Mkuu John Haule na hata naibu wake, Balozi Rajabu Gamaha, hakuwapo.


“Ilikuwaje basi Hazina watoe fedha zote hizo kwa viongozi wanaokaimu nafasi zetu? Hilo ndilo linalochunguzwa,” anasema waziri Membe.


Membe alikuwa anatoa ufafanuzi wa habari kwamba maofisa watano wa wizara yake wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa “kwa ajili ya safari za rais.”


MwanaHALISI lilikariri taarifa za wizara na ikulu katika toleo lililopita zikisema kwamba maofisa hao, akiwemo Mkuu wa Itifaki, walifanikiwa kuchota Sh. 3.5 bilioni “kutoka benki moja nchini.”


Ilielezwa kuwa fedha hizo zilikuwa sehemu ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi katika safari za rais kwa ziara za Geneva, Uswisi; Rio de Janeiro, Brazil; Addis Ababa, Ethiopia na safari ya ndani ya nchi – kwenda Arusha.


Maofisa waliosimamishwa ni pamoja na Mkuu wa Itifaki aliyetajwa kuwa ni Anthony Itatiro. Wengine ni ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfan; Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer; Mhasibu aitwaye Deltha Mafie na karani wa fedha Shabani Kesi.


Membe alisema, “…wizi huu umefanywa kwa ujanja wa hali ya juu na kuna mtandao mkubwa ambao Tume iliyoundwa itauweka wazi. Matokeo ya uchunguzi hayatakuwa siri.”


Waziri Membe amefafanua kuwa mtandao huo ulifanikiwa kuchukua kiasi hicho cha fedha, 8 Machi 2012 kutoka Benki ya NMB, tawi la Bank House lililoko Barabara ya Samora, katikati ya jiji la Dar es Salaam.


Amesema pamoja na kufanikiwa kuchota fedha hizo, hawakuweza kugawana kwa sababu walinaswa na fedha taslimu walipokuwa wanataka kugawana. Maofisa usalama wa wizara ndio waliowafuma na kuwakamata.


“Kwa hiyo, hata senti moja haikupotea, fedha zote zilirudishwa,” amesema.


Katika suala hilo, Membe amesema, “…sisi tumeshika mkia na sasa tunatafuta kichwa. Kinachotafutwa hapa ni kichwa. Na hicho kichwa kitapatikana.”



[/QUOTE]
 
Hili ni changa la macho, watu wamekamatwa wanagawana pesa, hawapelekwi gerezani au kufungiliwa mashitaka badala yake wanasimamishwa kazi wanaendelea kulipwa nusu mshahara,Inaundwa tume kuchunguza nayo itumie pesa, waziri anasema wao wameshika mkia, wanakitafuta kichwa, hii ni dhahili serikali ni dhaifu. Huyo Membe inakuwaje yeye, naibu wake , katibu mkuu na naibu wake wote kuwa safari kwa wakati mmoja, na nafasi zao kukaimiwa?? Au hii ni njama yao pamoja na waliowakaimu ili wachote hizo pesa.


Sijui unachjaribu kusema hapa ni nini? Hivi kusafiri kikazi ni kosa au ndiyo tiketi ya watu kufanya wizi wao? Huna namna ya kufikiria kama mtu ambaye hana disease of the mind?
 
Hivi Membe haoni aibu katika nchi ambayo madaktari na walimu wanataka kugoma kwasababu ya malipo duni wao wanatumia mabilioni kusafiria?...it is a shame

Aibu ya nini? Unadhani hizi hela zisingebajetiwa kwa safari na matumizi hayo muhimu zingeenda kwa hao watu wako wenye tamaa ya kulipwa kuliko wanavyolipwa kokote Africa?
 
huyu membe naye ni janga la taifa waziri gani anajichanganya namna hii.? Juzi amesema hazijaibiwa leo anasema wamewafuma wakati wanagawana kwa hiyo walikua wanagawania wapi.?
 
kama safari chache hizo zinatakiwa kugharamiwa na billion 3.5 , tangu jamaa aingie ikulu ametugharimu sh ngapi?
Kuna umuhimu wa wabunge(vyama vya upinzani)
kuhoji umuhimu wa safari za rais. Sasa wizi huu is an eye opener
 
Ama kweli Tanzania shamba la Bibi!
Nina wasiwasi na maelezo. Sidhani kama inawezekana Benki kutoa fedha yote hiyo kuwapa watu MKONONI!
Ila ilitakiwa ihamishiwe kinyemela kwenye akaunti ya Chama sasa walipoona kuna wajanja wameshatoa kumbukumbu kwa MwanaHalisi wakaona wawatoe kafara wenzao.
Haya ndiyo yale yaliyotokea EPA, maandalizi ya matumizi ya uchaguzi yanataka kuanza mapema!!!!!!! Huenda ni pamoja na maandalizi ya chaguzi ndogo??

SITAKI KUDANGANYWA MIMI!
 
Hili ni changa la macho, watu wamekamatwa wanagawana pesa, hawapelekwi gerezani au kufungiliwa mashitaka badala yake wanasimamishwa kazi wanaendelea kulipwa nusu mshahara,Inaundwa tume kuchunguza nayo itumie pesa, waziri anasema wao wameshika mkia, wanakitafuta kichwa, hii ni dhahili serikali ni dhaifu. Huyo Membe inakuwaje yeye, naibu wake , katibu mkuu na naibu wake wote kuwa safari kwa wakati mmoja, na nafasi zao kukaimiwa?? Au hii ni njama yao pamoja na waliowakaimu ili wachote hizo pesa.
Sio kweli
 
Back
Top Bottom