Membe: Wizi ulipangwa Hazina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: Wizi ulipangwa Hazina

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=1][/h]

  [​IMG]
  Na Alfred Lucas - Imechapwa 20 June 2012

  [​IMG][​IMG]
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema njama za kuiba mabilioni ya shilingi ya safari za Rais Jakaya Kikwete, zilifanikishwa na maofisa wa Hazina.

  Amesema maofisa wa Hazina walikiuka taratibu za kutoa fedha kwa wizara yake.


  Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jijini Dar es Salaam juzi, Membe amesema anatuhumu watendaji wa Hazina kwa kuhusika na njama hizo “…hawa wanajua taratibu za kutoa fedha kwa wizara yetu.”


  Waziri Membe amesema kwa mujibu wa taratibu, mwenye mamlaka ya kuomba fedha Hazina ni waziri husika, naibu waziri, katibu mkuu, na naibu katibu mkuu.


  Amesema hata baada ya viongozi hao kuomba fedha, lazima maofisa wa Hazina waende kwa mhasibu mkuu wa wizara husika ambaye atathibitisha iwapo kiasi cha fedha ambacho waziri anaomba, kipo na katika akaunti ipi.


  “Sasa kilichofanyika hapa, ni kwamba waliokuwa wanakaimu nafasi walifanikiwa kutoa fedha hizo benki. Jambo tunalojiuliza ni nani aliidhinisha fedha hizo kutolewa Hazina?” alihoji Membe.


  Membe amehoji, “Waziri wanamfahamu, naibu waziri, katibu mkuu na naibu katibu mkuu wote wanawafahamu. Wao ndio wataalamu wa fedha, wanafahamu taratibu za utoaji fedha; ilikuwaje wakatoa fedha kiasi kikubwa kama hicho bila idhini ya wale wanaowafahamu kuwa ndio wenye mamlaka?”


  Amesema wakati fedha hizo zinachotwa, hakuwapo. Naibu Waziri, Mahadhi Juma Maalim hakuwapo; pia Katibu Mkuu John Haule na hata naibu wake, Balozi Rajabu Gamaha, hakuwapo.


  “Ilikuwaje basi Hazina watoe fedha zote hizo kwa viongozi wanaokaimu nafasi zetu? Hilo ndilo linalochunguzwa,” anasema waziri Membe.


  Membe alikuwa anatoa ufafanuzi wa habari kwamba maofisa watano wa wizara yake wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa “kwa ajili ya safari za rais.”


  MwanaHALISI lilikariri taarifa za wizara na ikulu katika toleo lililopita zikisema kwamba maofisa hao, akiwemo Mkuu wa Itifaki, walifanikiwa kuchota Sh. 3.5 bilioni “kutoka benki moja nchini.”


  Ilielezwa kuwa fedha hizo zilikuwa sehemu ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi katika safari za rais kwa ziara za Geneva, Uswisi; Rio de Janeiro, Brazil; Addis Ababa, Ethiopia na safari ya ndani ya nchi – kwenda Arusha.


  Maofisa waliosimamishwa ni pamoja na Mkuu wa Itifaki aliyetajwa kuwa ni Anthony Itatiro. Wengine ni ofisa katika Idara ya Itifaki, Shamim Khalfan; Kaimu Mhasibu Mkuu, Kasim Laizer; Mhasibu aitwaye Deltha Mafie na karani wa fedha Shabani Kesi.


  Membe alisema, “…wizi huu umefanywa kwa ujanja wa hali ya juu na kuna mtandao mkubwa ambao Tume iliyoundwa itauweka wazi. Matokeo ya uchunguzi hayatakuwa siri.”


  Waziri Membe amefafanua kuwa mtandao huo ulifanikiwa kuchukua kiasi hicho cha fedha, 8 Machi 2012 kutoka Benki ya NMB, tawi la Bank House lililoko Barabara ya Samora, katikati ya jiji la Dar es Salaam.


  Amesema pamoja na kufanikiwa kuchota fedha hizo, hawakuweza kugawana kwa sababu walinaswa na fedha taslimu walipokuwa wanataka kugawana. Maofisa usalama wa wizara ndio waliowafuma na kuwakamata.


  “Kwa hiyo, hata senti moja haikupotea, fedha zote zilirudishwa,” amesema.


  Katika suala hilo, Membe amesema, “…sisi tumeshika mkia na sasa tunatafuta kichwa. Kinachotafutwa hapa ni kichwa. Na hicho kichwa kitapatikana.”   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni hatari hii serikali kweli inatisha unaweza kuamini eti pesa zilitolewa na kupewa watu wanaokaimu Ukatibu Mkuu, Unaibu

  Waziri Hazina na Mambo ya Nje; na pesa zikapotea na hawajui hao watu ni kina nani?

  Hiyo sio ajabu ya Nchi? Ndio Maana hatuna pesa za Budget... Matumizi na Wizi Mbovu

  Ndio Maana Wazanzibari wanataka Budgeti yao Wao Wataongoza kwa DINI Ufisadi huu wa Kijinga hautakuwepo

  Hii kweli inaonyesha Jinsi Serikali Ilivyo DHAIFU yaani inaendeshwa kama vile ya ki-Mafia
   
 3. d

  dguyana JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inaonyesha yashafanyika mengisana huko nyuma ila hili ni kama bahat mbaya tu. Tatizo raisi mwenyewe anapiga mno perdiem zake kwahiyo hata hawa jamaa wakichomoa yeye hajali. Nakuheshim raisi wangu ila haya unayataka mwenyewe kwa ajili ya udhaifu wako
   
 4. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kama safari chache hizo zinatakiwa kugharamiwa na billion 3.5 , tangu jamaa aingie ikulu ametugharimu sh ngapi?
   
 5. m

  mzee lyandi Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  re. wizi ulipangwa hazina.
  ni hatari kuona kiasi kikubwa kama hicho cha fedha kinatoeka ktk mazingira ambayo maofisa wa serikali wanahusika. ni vyema wangehifadhiwa kwanza(jela) then uchunguzi ikaendelea.
   
 6. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nchi yangu TZ this is possible kwako tu. 3.5 kwa tusafari huto tuchache, udhaifu wa baba RIZ maskini jamaa nao wanachota kupitia mgongo wake. Weit and see mambo ya kina jairo yatajirudia watu watarudishwa kazini kwa vishindo. Ndio maana maghorofa yanaibuka kama uyoga bila kujua matumizi yake cause ndio njia pekee ya kusafishia hizo pesa chafu. Ole wenu tunarecord maovu hayo
   
 7. O

  Ome Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  hayo ndio matokeo ya kukumbatia mafisadi na wezi, wezi wa EPA wangeshughurikiwa ipasavyo kuna ambaye angepata uthubutu wa kuiba tena, i hate those people who called a politicians in my lovely country, the whole system is already corrupted we need to have a brand new system instead of using an old used one.

  yani mtu haogopi kula pesa ya mlipa kodi this is not fare watu tunakatwa kila mwezi kodi then somebody just doing nothing illegal fill his/her pocket with 3.5b for single day it real pain.
   
 8. J

  JR LEO Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :lol:
  serikali yote nyinyiem iko corupted je ni nani atamfunga paka kengele? ******** zao
   
 9. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hili ni changa la macho, watu wamekamatwa wanagawana pesa, hawapelekwi gerezani au kufungiliwa mashitaka badala yake wanasimamishwa kazi wanaendelea kulipwa nusu mshahara,Inaundwa tume kuchunguza nayo itumie pesa, waziri anasema wao wameshika mkia, wanakitafuta kichwa, hii ni dhahili serikali ni dhaifu. Huyo Membe inakuwaje yeye, naibu wake , katibu mkuu na naibu wake wote kuwa safari kwa wakati mmoja, na nafasi zao kukaimiwa?? Au hii ni njama yao pamoja na waliowakaimu ili wachote hizo pesa.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ingekuwa ni fedha za shule, maji, barabara....
   
 11. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  upepo tu utapita, lakini tuachieni tupumue zanzibar ufisadi kama huu haujawahi kutokea na wala hautotokea ile ni nchi na ina dini.
   
 12. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huu ni uwongo benki gani itakayo kupa bil 3.5 cash kwa madafu yetu utayabebea wapi jamani??? Wasitupige changa la macho kijinga hivi
   
 13. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wangehamishiwa wizara nyingine, unapogusa pesa ya safari ni sawa ni kugusa moyo wa Mzee wa Magogoni, lazima ushughulikiwe swiftly.
   
 14. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Hivi Membe haoni aibu katika nchi ambayo madaktari na walimu wanataka kugoma kwasababu ya malipo duni wao wanatumia mabilioni kusafiria?...it is a shame
   
 15. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umeonaee, yaani ukikaa nje miaka 2 au mitatu tu ukirejea bongo unashangaa hivyo vikwangua namna vinavyoota. Ukiwa angani utasema nchi inaendelea sana lakini nenda uwanja wa fisi uone maisha yalivyo, hii inaonyesha wazi kuwa maghorofa hayo hayatokani na mzunguko sahihi wa fedha bali ni njia za kusafisha hizo fedha chafu.
   
 16. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Duh, nii kweli nchi hii inaibiwa, lakini inapofika kupigia dili pesa za Safari za Mkuu wa nchi mwenyewe! Maana yake ni kwamba huu wizi umeshakuwa sugu na kuonekana kama ibada tu. Ukichung kwa undani ni kwamba hawa watu walianza kidogo kidogo, kwa kuanzia kuiba pesa za kuwasaidia Wamachinga, Mama Lishe, Waathirika n.' Na wakawa hawachukuliwi hatua yoyote! Wakaingia kuiba pesa za Makatibu wakuu, Mawaziri, wakaona kimya! Sasa wakaingia za rais. Mpaka wamekamatwa watakuwa wameshaiba pesa nyingi sana za Mh. "Dhaifu".
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Walewale walio kunywa uji wa mgonjwa.
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Na jana wamepitisha mlo mwingine kupitia silly session.

  At least Membe has come open and he seem to care a little bit unlike dhaifu Kikwete and the rest of ccm.
   
 19. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,314
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Kama wanene wanathubutu hata kuiba fedha za safari za mkuu wa nchi basi serekali ya jk haina mtu msafi wa kumnyoshea mwenzake vidole. Hivyo wananchi wachini ni maumivu tu.
   
 20. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Dah! Kodi zetu hizo!
   
Loading...