Membe Ubalozi karibia utafungwa kule Brussels

swali liko palepale je balozi ambazo hazipati waombaji wa visa wa kutosha zinajiendeshaje?Manake Mkuu umetaja hizo nchi giant na naweza kukubali kuwa zinaleta wataalii wengi bongo sasa je zile balozi ambazo ziko kwa 'wachovu' au wasiopenda kufanya utalii tanzania vipi huko nako wanaishi kwa hela ya visa?

- Mkuu nchi nilizozitaja nimewahi kuishi na kama kawa very close na watu wa hizo ofisi, ndio maana ninafahamu vyema jinsi system zetu za balozi financially zinavyofanya kazi, maofisa wanaweza kosa mishahara, lakini sio the locals au bills za ofisi ni lazima zilipwe ontime na wakati mwingi hutegemea hela za viza kunapokosekana hela toka serikalini.

- Pia nimewahi kuishi katika nchi za ki-Africa pia, kama Zambia, Burundi, Rwanda, Kenya na zaire sikuwahi kusikia kwamba ofisi za balozi zina matatizo ya hela hata siku moja, matatizo ya hela mara kwa mara huwa ni kwa balozi zetu za West.
 
kuna mtu ananiuma sikio kwamba si kwamba umeishi bali kuna mtu wako ubaloizini hapo ambaye nadhani ni jamaa yako wa karibu sana usibishe tusije mtaja jina hapa maana jf bwana ,ndiyo anakupa hizi habari na namna balozi ziendavyo , maana kama umekaa us miaka kibao ni wazi kwamba walio kuwa katika nchi hizi walisha ondoka labda ubaki kuwasiliana nao na kuuliza lakini kubali na wenzako mwanavyo sema ukweli wa leo hii si wa jana
 
1.
Kaka makusanyo ya visa yanatofautiana nchi na nchi. Siamini kama Brussles kuna flow ya wageni kiasi cha kuweza kuwezesha kukusanya kiasi cha kutosha kwa matumizi kama hayo. Wengi wanaoingia na KLM ni wa connctions kutoka US/CANADA/germany/Nordic/Scandnavian countries ambazo kuna balozi tofauti. Vilevile kama sijakosea mapato yote huwa yanaingizwa kwenye account halafu kupelekwa Hazina. Hazina ndio wanaotoa fedha/idhini za matumizi kufuatana na bajeti.

- Mkuu habari yako ambayo hoja yake ya msingi ni "huamini" haina ukweli wowote, infact iko mbali sana na ukweli Belgium inatuletea watalii wengi sana na wageni wa kiserikali kutokea EU na mashirika mbali mbali ya kimtataifa yaliyoko Brussels, nimewahi kusoma shule pale Antwerpen, na pia nimewahi kuishi Brussels na kufanya kazi tena Antwerpen, kwa hiyo nimesafiri sana kati ya Dar na Brussels back and forth, toka enzi hizo za Air Sabena na Lufthansa, sijui kama bado zinatua bongo lakini najua KLM inakuja bongo, bado tunapata wageni wengi sana kutoka Belgium, kwa hiyo ubalozi wetu pale unatakiwa kuwa na hela za kutosha kutokana na malipo ya viza ili kujiendesha bila kusubiri hela toka serikali.

- Kama hujakosea, hapana umekosea hakuna ofisa mjinga aliyeko ubalozi kama wa Brussels anayeweza kupeleka hela hazina, huku ana permission ya wizara kuzitumia kwa matumizi ya kiofisi inapobidi, sasa kwa ofisi zetu kama huko sio tu inapobidi ila huwa ni kawaida Hazina huwa wanakuja kukagua mahesabu mwisho wa mwaka, lakini kwamba eti kuna hela wanapokea toka ofisi zetu za ubalozi labda kutoka Africa, lakini sio West na the day ikitokea kama unavyosema basi ofisi hizo zitafungwa mpaka mgawo wa hela za serikali uende huko, kwa hiyo sio tu kama hujakosea ila umekosea sana!

Huenda kuamini kwako ndivyo inavyosema kwenye karatasi za serikali, lakini huo sio ukweli kabisa wa the real financial operations za balozi zetu, hasa za West, bila hela za viza nyingi zingekua zimeshafungwa kabisaa!
 
kuna mtu ananiuma sikio kwamba si kwamba umeishi bali kuna mtu wako ubaloizini hapo ambaye nadhani ni jamaa yako wa karibu sana usibishe tusije mtaja jina hapa maana jf bwana ,ndiyo anakupa hizi habari na namna balozi ziendavyo , maana kama umekaa us miaka kibao ni wazi kwamba walio kuwa katika nchi hizi walisha ondoka labda ubaki kuwasiliana nao na kuuliza lakini kubali na wenzako mwanavyo sema ukweli wa leo hii si wa jana

- Kwanza hukuwa na sababu ya kutumia jina hili kusema haya maana unaishia kujishusha hadhi bure kwangu wewe ni mtu ninaamini tunaheshimiana sana kwa jina lako la kawaida, halafu mbona unataka kutumia nguvu kunilazimisha nikubali hoja? Wewe ni kuweka mawazo yako na mimi kuweka yangu ndio njia ya kuelimishana mkuu sio kutumia nguvu na vitisho, eti utamtaja anayeniambia what is that? Na wewe anayekuambia ni nani mkuu?

- Kuhusu watu kunihusu katika serikali ya bongo na balozi zetu, mkuu ninao washikaji wengi sana na hata ndugu wa karibu, na kama ni habari au dataz sidhani kama una maana hawa ndio wananipa dataz za serikali na CCM! Infact mzazi wangu mmoja amewahi kuwa balozi mara nyingi sana, sasa kweli unaamini kwamba ninabahatisha na this infos? Halafu si nimewahi kusema wazi hapa kwamba mkuu mmoja wa ukaguzi wa mahesabu ya serikali wa zamani ni rafiki yangu wa karibu sana, sasa mkuu kweli una amini ninabahatisha haya?
Nikiwa ninasoma Antwerpen kwenye scholarship nilikuwa ninachukua posho toka ubalozini hivi umeshawahi kupitia hiyo process ya kuchukua hela ubalozini mkuu? sasa kweli mkuu unaamini ninabahatisha haya au ninahitaji watu wa karibu kujua haya ya balozi zetu na system zake za pesa?

- Wewe mwenyewe unasema nina watu ninawajua huko kwenye mabalozi yetu halafu tena unasema nikubali ukweli wa leo na sio wa jana unaona mkuu unavyojichanganya, anyways naona nikuachie mjadala wako mkuu maana sasa sio hoja tena ila vitisho vya kunitishia kuwataja wanaohusu walioko ubalozini, hivi kweli hii ndio spirit ya JF ya kuhabarishana na kuelimishana, kwamba ni lazima ukubali tu ama sivyo ni vitisho, kweli Tanzania tuna safari ndefu sana tuendako!

Haya mkuu naomba nikuachie mjadala maana usije ukawataja wanaonihusu huko ubalozini. Bwa! ha! ha! ha!
 
Mzee ES nimesha shuhudi wageni wengi sana wana chukulia VISA hapa hapa Dar .Kuna shida ya Balozi ama ofisi za balozi kukaa majumbani mwa wa watu.Kwa mgano kule Holland jamaa mzungu ni rafiki yake JK for the last 14yrs wanajuana na hata JK akipita pale lazima wanaitana na wanadanya shopping wote , leo ofisi yake iko porini hjata Public transport ni shida hadi uchukue taxi.Wa Dutch they got no time for that wanachukulia airport Dar wanamaliza fitina .Unasemaje ?

Mkuu Lunyungu,

- Wewe tunaheshimiana kwa hiyo nitakujibu, uliyosema hapa ni kweli 100% na kama unakumbuka hii ishu niliwahi kuisukuma mbele kwa wakuu wakapata kigugumizi kwa sababu ya ushikaji wa huyo mkulu na muungwana, sawa sawa kabisa,

ila tu uliyosema hayana anything to do na ubalozi wetu Brussels kukosa heat, tena wakati huu wa winter, najua for a fact kwamba Brussels tunao ubalozi kamili, maana mimi nilipokuwa pale Karume ndiye alikuwa full balozi.
 
ni makosa kwa balozi zetu kuishi kwa kutegemea viza. wizara ya mambo ya ndani nayo huwa wanapigia hesabu mapato ya viza na hata wakaguzi wa mahesabu wanapopita ubalozini huulizia na kuonya juu ya matumizi ya pesa za viza. zaidi ya hayo mapato ya viza siyo "constant" kwani yanategemea misimu ya watalii hivyo hata balozi zetu haziwezi kupanga matumizi yao kutokana na mapato ya viza.

balozi zina gharama nyingi hususan serikali inaposhindwa kuzipatia pesa balozi zetu basi hayo mapato ya viza ndio yanatarajiwa kutosheleza sio malipo ya umeme, simu, pango la ubalozi na maafisa bali pia mishahara ya "local staff" sasa hiyo pesa ya viza kweli itatosheleza haya!

naamini imefika wakati watendaji serikali kuu waache kufikiria kwamba balozi zinaweza kuendeshwa kwa pesa za viza hivyo hata pesa zipopelekwa balozi zetu zinaweza kukidhi mahitaji yake.

wakuu maafisa wetu wanawekwa kwenye hali mbaya utakuta balozi nyingine zinakatiwa hata simu!
 
Mkuu Lunyungu,

- Wewe tunaheshimiana kwa hiyo nitakujibu, uliyosema hapa ni kweli 100% na kama unakumbuka hii ishu niliwahi kuisukuma mbele kwa wakuu wakapata kigugumizi kwa sababu ya ushikaji wa huyo mkulu na muungwana, sawa sawa kabisa,

ila tu uliyosema hayana anything to do na ubalozi wetu Brussels kukosa heat, tena wakati huu wa winter, najua for a fact kwamba Brussels tunao ubalozi kamili, maana mimi nilipokuwa pale Karume ndiye alikuwa full balozi.

Mkuu ES
Samahani umeni quote kwenye mahojiano yako .Mkuu mimi ni real hapa na maomba majadiliano haya uniache nje mie nikitaka kukupinga napinga hapa .Mkuu kwa hili unanikosea haki kabisa .

Masahihisho mkuu .

Kwa data tu nilizo nazo ni kwamba Ubelgiji inaweza kuwa inaleta wageni wengi wa kiserikali na mashirika ya Umma Serikalini lakini kwa Utalii mkuu Ujerumani na Holland ndizo hasa .Wabelgiji hawaijui Tanzania vilivyo na hili ndilo naweza kukupinga bila kuzunguka .Nina data za kutosha .

Again mkuu mimi na wewe tuna heshimiana sana na hata kupingana kwangu mimi na wewe ni kwa hoja mkuu .
 
- Sawa sawa mkuu, nimekupata sana check PM.
 
Nadhani hili ni suala zaidi la kiutawala wa ndani ya ubalozi wenyewe. Kama wanashindwa ku keep up na bills za gas kazi kweli kweli....

Hili linatokea ndugu yangu. Balozi zetu nyingi huwa hawapelekewi pesa ikiwamo mishahara yao on time na hata kusababisha wafanyakazi wa balozi hizo kulazimika kununua mahitaji yao muhimu kwa mkopo kutoka masupermarkets ambayo balozi zimeomba kuwepo kwa utaratibu huo na pesa zikifika basi wafanyakazi hao hulipa malimbikizo ya madeni yao. Ni hali ya kusikitisha lakini lipo, ingawaje siku hizi limepungua ukilinganisha na miaka michache ya nyuma.

Hivyo mimi sishangai kusikia ubalozi pale Brussels wameshindwa kufanyia matengenezo heating system yao ili kujikinga na hali ya baridi hapo ofisini.
 
Barafu yamkimbiza ofisini balozi wa Tanzania Ubelgiji

Mwananchi newspaper
Leon Bahati

BALOZI wa Tanzania nchini Ubelgiji, Simon Mlay, amesimamisha shughuli za ubalozi tangu Desemba 5, mwaka huu kutokana na baridi kali katika ofisi za ubalozi huo.

Taarifa iliyopatikana katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeeleza kuwa huduma pekee ambazo zitaendelea kutolewa na ofisi hiyo iliyopo mjini Brussels, ni za viza.

Hali hii imeelezwa kuwa imetokana na mtambo wa kupasha joto kwenye ubalozi huo kuharibika vibaya na sasa serikali imeamua kununua mwingine.

Juhudi za kuuweka mwingine nazo zimeshindikana kutokana na mafundi wengi nchini Ubelgiji kuwa kwenye mapumziko ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

"Hiki ni kipindi cha baridi, ubalozi umelazimika kufunga shughuli zake hadi hapo mtambo huo utakapofungwa na kuanza kufanya kazi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ikibainisha kuwa, uwezekano wa ofisi kurejesha huduma zake kikamilifu ni Januari 20, mwakani.

Ilielezwa kuwa tayari serikali imetuma fedha za manunuzi ya mtambo huo wa kuongeza joto na taratibu za kupata mwingine zimekamilika.
 
sasa hii si fedheha! hata hivyo ni bora balozi ameamua kusitisha shughuli kuliko kuwalazimisha watendaji wapige mzigo kwenye baridi kali na hivyo kuhatarisha maisha yao.
 
Haya mambo ya kutegemea hela za viza ni kama vile baba mwenye nyumba kuacha hela pungufu na kutegemea mama atafanya ujanja ili kitoweo kipatikane. Serikali inatakiwa iendeshwe kwa kufuata taratibu. Kuruhusu wahasibu na mabalozi kupindisha taratibu ili kukidhi mahitaji yaliyotakiwa kuwa yametengewa fedha katika kasma yake ndiyo mwanzo wa kuitana mafisadi. Gharama za uendeshaji za ubalozi zinatakiwa kujulikana mapema na kuwekewa fedha za kutosha. Ubalozi ndiyo kioo cha nchi yetu huko ugenini. Hivi tunategemea mwekezaji wa maana gani atawekeza kwenye nchi ambayo inashindwa hata ku-bajet kwa matumizi muhimu kama joto wakati wa winter katika balozi zake? Unaweza kukuta hata hiyo mashine mpaka iharibike kiasi hicho ina maana hata service ilikuwa haifanyiwi! Kuepuka gharama ndogo za service zitatufanya tununue mashine mpya katika wakati ambao si muafaka! Na hapo ndipo tutakapobambikwa!

Inasikitisha lakini tutafanyaje?

Amandla........
 
sasa hii si fedheha! hata hivyo ni bora balozi ameamua kusitisha shughuli kuliko kuwalazimisha watendaji wapige mzigo kwenye baridi kali na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Nilisema nikaondoka ili nione wabishi wa jf wanasemaje .Sasa haya wamebana na sasa wamechomoa .Tuendelee sasa .Ubalozi umefungwa kuanzia dec 5 lakini hakuna tangazo wala taarifa .Je kuna tatizo gani hapa ?

Es umeona kwamba visa hazitoshi kuendesha ubalozi na kwamba si kweli Ubelgiji wanaongoza kwa watalii ?
 
Taarifa iliyopatikana katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeeleza kuwa huduma pekee ambazo zitaendelea kutolewa na ofisi hiyo iliyopo mjini Brussels, ni za viza.

Es umeona kwamba visa hazitoshi kuendesha ubalozi na kwamba si kweli Ubelgiji wanaongoza kwa watalii ?

Mkuu Kimbembe,

- Heshima mbele sana, ofisi imefungwa lakini viza inaendelea unafikiri ni kwa nini wasiende kuchukulia bongo tu na watalii sio wengi kutoka Belgium anyways? Soma betweeen the lines mkuu maana ndio hasa sifa yetu kubwa hapa JF.

Anyways, Kritsmas njema mkuu wangu na heri ya mwaka mpya.
 
Kila siku wako Ulaya na America; inaelekea wakiwa huko hawafiki ubalozini wanaishia mahotelini tu na ndio maana wakina Karamagi wanasign mikataba nje ya ubalozi!! Inaelekea hawa wanamtandao na Seikali yao kila mtu kivyakevyake tu; hawana common vision.Lumbanga si ndio yuko huko Brussels, inakuwaje balozi yupo lakini ubalozi unakosa central heating system? Mrudisheni aje ajibu maswali ya EPA .

write with facts... u seem to have a problem with some ppl
kukurupuka inamfanya mtu aonekane mpumbavu
 
Last edited:
Mimi ni mtu wa Ottawa, hapa ubalozi wetu umegeuks kuwa wa nyumba kumikumi tu, Sijui huyu Mheshimiwa Kallaghe anafanya Nini. Haishi kwenye nyumba nza watu yeye na mke wake. Mama Balozi anacomment et hakuna mwanamke wa Kitanzania mzuri kama yeye na anayevaa kama yeye. Sisi hatumfahamu kwa undani sana lakini yuko bega kwa bega na Mashangingi mawili Moja toka Moshi Na lingine toka Tanga watu ambao wanajulikana kwa kubeba waume za watu.

Hali ya hapa ianatia aibu..... waziri Membe tunakutaarifu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom