Membe: Sihusiki vurugu za Mtwara...

Membe: Sihusiki vurugu za Mtwara...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Saturday, 25 May 2013 14:44

bernard%20membe%20waziri.jpg


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akifafanua jambo


Dar es Salaam,Tanzania

WAKATI wanasiasa wakipinga hatua ya kuhusika katika vurugu za Mtwara ziliso sababisha vifo vya watu wa wawili na kusababisha uharibifu wa mali, kwa kuijia juu Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kwamba isitafute sababu, bali itafute njia ya kukomesha vurugu na kutatua tatizo la Wana-Mtwara, Wazi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe naye ameibuka nakudai kuwa ahusiki katika vurugu hizo.

Waziri Membe amevunja ukimya na kudai kwamba tuhuma zinazorushwa kwake na wana CCM wenzake kwamba anahusika katika vurugu hizo si za kweli.


Membe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu tuhuma hizo zilipoanza kusambaa sehemu mbalimbali nchini kwamba anahusika katika vurugu za Mtwara zilizo sababisha Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Anne Makinda asitishe vikao vya Bunge la Bajeti kwa siku mbili.


Akizungumza katika Mahojiano maalum na Habarimpya.com Membe alisema kwamba yeye ahusiki kwa namna yoyote ile na vurugu hizo na kwamba watu walioamua kumhusisha na vurugu hizo wana malengo yao yasiyokuwa na tija.


"Si kweli kabisa kwamba ninahusika kwa namna yoyote ile na vurugu za Mtwara, wanaonihusisha wana malengo yao ya kisiasa ambayo hayana tija kwa maslahi ya nchi yetu pamoja na rasilimali zetu"alisema Waziri Membe. Jana tovuti ya Habarimpya.com katika toleo lake namba 2468 iliyokuwa na kichwa cha habari iliyosomeka kwamba Membe atuhumiwa vurugu za Mtwara ilielezea jinsi ambavyo serikali inawatuhumu wanasiasa kuwa wao ndiyo chanzo cha vurugu hizo.

 
Hii ni Pro-Membe. kama kawaida ni siasa tu
 
Watu wengi walitaka tu kujua kama yeye yuko upande gani katika hili suala la gesi maana wenzake wote wamejitambulisha kwa wananchi wa kusini bado yeye tu.

Kama hataki kujijulisha ni vema tu, maana sisi kwa akili za kuzaliwa tu tunajua hawezi kuwa tofauti na boss wake, na hii si hatari kwetu ni kwake. Maana sisi tumekikataa chama hiki cha mafisadi kimetuulia ndugu zetu wengi na kuchoma nyumba zetu moto na kubaka wake zetu order kutoka amiri jeshi mkuu
 
Kwa hiyo ni kweli Hawa Ghasia alimrushia tuhuma nzito Membe.?
 
vurugu zote aulizwe siraha na chadema yake

SIRAHA ndio NANI??? Unaiogopa CUF? Wao Wamefanya MIKUTANO MINGI haswa MTWARA... Unaogopa kusema neno CUF??
Au as USUAL U R BIAS sio kwa kutaka ni kwa kulazimishwa na CHUKI...
 
Mbona uhusika wake hausemwi au ndiyo vita vya panzi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kumbe yule kilaza aliyekuja hapa kumtukana Lowasa eti Membe hakutajwa kwenye hicho kikao chao cha wahuni alikuwa anafunika kombe?! Jamaa kaona maji yamezidi unga kajitokeza kuthibitisha kutajwa kwake.
Wao warukeruke tu, lakini kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake...
 
Kwa hiyo ni kweli Hawa Ghasia alimrushia tuhuma nzito Membe.?
Eti kwa kua mali zake hazijahujumiwa na wananchi kwa hiyo anahusika na ghasia hizo.... Hivi kumbe mtu akibobea sana kwenye ufisadi anapoteza akili ya kawaida ya kufikiri?
 
hapa wanamsingizia membe ila wana mererani na geita nao wataamka kutoka kwenye ukungu sijui hapa watamshutumu nani?
 
Membe anajifanya kama Vile Panya anakutafuna (anakungaka) hafu hapo hapo anakupuliza ili usihisi maumivu .amekuwa na vituko vingi ,vituko vingine avifanyavyo utashangaa kwani nina yakini Rais anavijuwa sasa tujiulize kuna nini kati ya watu wawili hawa?
 
vurugu zote aulizwe siraha na chadema yake
Kweli wewe una akili za panzi, waliomshutumu Membe ni CCM wewe unaiingiza CDM Na Slaa, kwanza kumbuka jana Kigwangala alikanusha kuwa tuhuma hizi ni uzushi na hazikutolewa katika kikao chao leo hii Membe anakanusha kuwa hausiki na tuhuma hizo zilizotolew dhidi yake, TAFAKARI kauli hizi na uone unatakiwa uwe kundi lipi la wajinga kama ulivyo sasa au uhamie kundi la welevu kama sisi.
 
SIRAHA ndio NANI??? Unaiogopa CUF? Wao Wamefanya MIKUTANO MINGI haswa MTWARA... Unaogopa kusema neno CUF??
Au as USUAL U R BIAS sio kwa kutaka ni kwa kulazimishwa na CHUKI...

Bado ndoa ni changa...honey moon itaharibika.Ukizingatia huyu mke ana wivu.Kila siku NCCR anajijenga.
 
Back
Top Bottom