Membe: Niliponea chupuchupu

Membe: Niliponea chupuchupu

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

Na Mkinga Mkinga na Masoud Masasi, Dodoma

Posted Alhamisi,Novemba15 2012 saa 21:49 PM

KWA UFUPI

"Baada ya Mheshimiwa Membe kuondoka kwenda Shinyanga, wapinzani wake ndani ya chama walitumia muda huo kupiga propaganda mbaya dhidi yake na walianza kutangaza hadharani kwamba, hatapata nafasi hiyo ili kumnyong'onyesha," kilisema chanzo chetu ambacho hakikutaka kutajwa gazetini.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Bernard Membe amekiri kuwa haikuwa rahisi kwake kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kupitia kundi la kifo kwa kuwa upepo uligeuka ghafla kinyume na matarajio yake.

Membe ni miongoni mwa makada wa CCM waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Nec kupitia nafasi kumi zilizokuwa zikiwaniwa na vigogo kadhaa wa chama hicho.

Akizungumza na Mwananchi jana, Membe alisema kuwa amefurahishwa na matokeo yote na kwamba ushindi wake wa kupata nafasi kati ya washindi kumi ni salamu kwa waliokuwa wakipiga kampeni chafu dhidi yake.

"Ninawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa kunichagua… Kuchaguliwa kwangu kumetuma ujumbe mzito kwa waliokuwa wakihaha kuhakikisha kwamba, sipati nafasi hiyo kwa gharama zozote," alisema Membe.

Makada wengine waliochaguliwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wasira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Wengine ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Willison Mukama na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenella Mukangara.

Membe alishika nafasi ya sita katika kundi hilo licha ya vitisho kutoka kwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CC, Hussein Bashe ambaye siku moja kabla ya uchaguzi aliapa kuwa atahakikisha waziri huyo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ‘hapiti'.

Baadhi ya watu walio karibu na Membe wanasema kuwa, mambo yalibadilika ghafla mjini Dodoma siku ya Jumamosi baada ya waziri huyo kuongozana na Rais Jakaya Kikwete kwenda mkoani Shinyanga kwenye mazishi ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Hayati Aloysius Balina.

"Baada ya Mheshimiwa Membe kuondoka kwenda Shinyanga, wapinzani wake ndani ya chama walitumia muda huo kupiga propaganda mbaya dhidi yake na walianza kutangaza hadharani kwamba, hatapata nafasi hiyo ili kumnyong'onyesha," kilisema chanzo chetu ambacho hakikutaka kutajwa gazetini.

Membe ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuanza kujijenga kwa ajili ya kuwania urais 2015 kupitia CCM na kundi lake limekuwa likisigana na la kada mwingine anayetajwa kuwania nafasi hiyo, Edward Lowassa.

Aidha, kumekuwa na minong'ono mingi baada ya yeye kushika nafasi ya sita katika kundi la watu kumi kwamba ameanguka kisiasa, lakini yeye anasema amefanikiwa.

Membe alisema kimsingi kila aliyeomba kuchaguliwa kupitia mkutano mkuu alikuwa na matumaini ya kushinda japokuwa wengine hawakufanikiwa.

"Unajua, inabidi yeyote anayetaka kunipima ajue kwamba, sikugombea ili nishike namba moja, la hasha; niligombea kuchaguliwa kuwa mjumbe wa NEC na ninamshukuru Mungu nimepata," alisema Membe.

JK anena
Katika hatua nyingine Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, jana alitoboa siri kuwa, wapo watu waliokuwa wakitambika usiku na mchana ili chama hicho kitoke vipande kwenye Mkutano Mkuu wa nane.

Akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM mkoani Dodoma katika sherehe maalumu iliyoandaliwa na uongozi wa mkoa huo kuwapongeza viongozi wapya, Kikwete alisema mkutano huo umekwisha kwa mafanikio kinyume na matarajio ya wengi.

Alisema CCM sasa kiko imara na tayari kimekwishapanga safu yake kwa ajili ya mapambano na kwamba, uchaguzi huo ni ujumbe tosha kwa wapinzani.

"Nashukuru Mungu mkutano umeisha salama maana kulikuwa na watu walikuwa wakisali na hii si kusali bali ni kutambika usiku na mchana ili kwenye mkutano mkuu kuwe na vipandepande, lakini haikuwa hivyo kabisa mkutano umeisha salama bila ya matatizo yoyote," alisema.

Kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa Mkutanmo Mkuu alisema, watayachambua maazimio na mapendekezo yote na kuyatengenezea mpango utekelezaji ndani ya chama na Serikali.

Aliwatwisha jukumu zito wajumbe wa NEC kuwa mara baada ya mafunzo watatakiwa kutembea nchi nzima kwa ajili ya kueneza sera za chama na kueleza ukweli juu ya CCM kwa Watanzania.

"Ili kufikia malengo niliyoyataja, lazima tuanze na Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ambao wao wakipata mafunzo watakuwa wakufunzi wa wengine," alisema Kikwete.

Sekretarieti kazini
Katika hatua nyingine Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema Sekretarieti mpya iliyoteuliwa juzi imeanza kazi kutekeleza majukumu yake.

Alipoulizwa kama sekretarieti hiyo ina uwezo wa kuendelea kufanya kazi bila ya kuundwa kwa Kamati kuu, Nape alisema hilo siyo jambo la kushangaza.

"Nakwambia Sekretarieti mpya inaendelea na kazi zake na ilianza kazi mara tu baada ya kuteuliwa juzi," alisema Nape.

Alipoulizwa ni kazi zipi zilizokwishafanywa na wajumbe wa kikao hicho, Nape alisema ni kazi za kawaida kama zilivyoainishwa katika katiba ya chama hicho.

"Tunaendelea na kazi za kawaida za chama, nenda kaangalie katika katiba utaona kazi za kila mjumbe zimeainishwa kule," alisema na kukata simu.

Sasa Utakuwa Rais wa NCHI?
 
Sijui ni kitu gani kwa huyu baba sina ubaya nae wala sijatumwa honestly speaking anaonekana ni mnafiki sana hasa fake smile aliyonayo!!!!na misemo yake ndo kabsaaa....!!eti nasubiri kuoteshwa mmh???????:shut-mouth:
 
Membe na mbio za ikulu.Huku nao Chadema wanagombania kupata nafasi wakati wanajua ikulu kwao ni ishu.Zitto mwachie kibabu kikajifie kuzunguka nchi nzima lazima kife
 
Membe na mbio za ikulu.Huku nao Chadema wanagombania kupata nafasi wakati wanajua ikulu kwao ni ishu.Zitto mwachie kibabu kikajifie kuzunguka nchi nzima lazima kife

Kweli JF kuna watu wa kila aina,Zitto na Kibabu wanaingiaje hapa bi.Kopa?
 
Membe na mbio za ikulu.Huku nao Chadema wanagombania kupata nafasi wakati wanajua ikulu kwao ni ishu.Zitto mwachie kibabu kikajifie kuzunguka nchi nzima lazima kife

je wewe unayo kinga ya kifo, huyo unayemuita kibabu anaweza kuapishwa wakati wewe ukiwa maiti
 
Sijui ni kitu gani kwa huyu baba sina ubaya nae wala sijatumwa honestly speaking anaonekana ni mnafiki sana hasa fake smile aliyonayo!!!!na misemo yake ndo kabsaaa....!!eti nasubiri kuoteshwa mmh???????:shut-mouth:

sio tu mnafiki bali uhakika nilionao ni kiongozi wa ushirikina nandi ya ccm na ndio tegemeo lake kubwa, na mara nyingi amekuwa akijisifia kuwa wakwake ni wakurithi na sio wa kununua na ndipo hapo viongozi wengine nandi ya ccm wamekuwa wakimuogopa kama ukoma hata maradhi ya anayetajwatajwa kuitaka ikulu kwa nguvu zote yanausiswa naye na kuna wakati alijigamba kuwa aatammalizia kila akibonyeza kitufe mzee ugonjwa wa kutetemeka unaaanza nasikia huwa wanafanya kumuomba asimmalizie. Na hiyo ndiyo ccm
 
Ninalichokiona baada ya kusoma mara nyingi sana ni kuwa si membe tuu ndiye alipaswa Mtaja Mungu hata katika michezo isiyo na Mungu "Rais Naya anashukuru Mungu kuwa Mkutano umemalizika salama". Si mchezo...Sijui kama wapo salama hivyo.makundi ya tangu 2010 yamekuwa die hard km windows XP ktk biashara ya Microsoft.Sasa hapa ambapo hata yeye mwenyewe anakiri kuwa mambo yangeweza yasiwe salama kabisa.

Na kaahidi kushughulikia hizo kura 3, basi kuna kila dalili bado vita inaendelea.
 
Nachukizwa sana dira na mikakati CCM hawalengi kupambana na UJINGA, UMASIKINI, MARADHI na SHETANI RUSHWA wao wana ONLY ONE BIG COMMON agenda KUSHIDA UCHAGUZI! Kwa hili kweli wameweza kukubaliana kila mwana ccm lengo lake ni kushinda uchaguzi hata kama wananchi wataishi mapangoni, gizani, mlo mmoja wao bora washinde uchaguzi.
 
sio tu mnafiki bali uhakika nilionao ni kiongozi wa ushirikina nandi ya ccm na ndio tegemeo lake kubwa, na mara nyingi amekuwa akijisifia kuwa wakwake ni wakurithi na sio wa kununua na ndipo hapo viongozi wengine nandi ya ccm wamekuwa wakimuogopa kama ukoma hata maradhi ya anayetajwatajwa kuitaka ikulu kwa nguvu zote yanausiswa naye na kuna wakati alijigamba kuwa aatammalizia kila akibonyeza kitufe mzee ugonjwa wa kutetemeka unaaanza nasikia huwa wanafanya kumuomba asimmalizie. Na hiyo ndiyo ccm

Nadhani wewe utakuwa ni yule msomali, hebu tuambie hayo maneno kwenye red yana maana gani kwa Kisomali!?
 
sio tu mnafiki bali uhakika nilionao ni kiongozi wa ushirikina nandi ya ccm na ndio tegemeo lake kubwa, na mara nyingi amekuwa akijisifia kuwa wakwake ni wakurithi na sio wa kununua na ndipo hapo viongozi wengine nandi ya ccm wamekuwa wakimuogopa kama ukoma hata maradhi ya anayetajwatajwa kuitaka ikulu kwa nguvu zote yanausiswa naye na kuna wakati alijigamba kuwa aatammalizia kila akibonyeza kitufe mzee ugonjwa wa kutetemeka unaaanza nasikia huwa wanafanya kumuomba asimmalizie. Na hiyo ndiyo ccm

Nani aloge huyo mzee wenu?Yeye mwenyewe ana ugonjwa wa kukubali kweli.Kila kitu kahujumiwa.
 
HAHAHAHAH JF ina watu wengi, wengine hawajui waandike nini? wengine wanakurupuka utadhani wametoroka toka mirembe kabla hawajamaliza matibabu. hata kama kibabu kinamuhusu? ya kwake yanamshinda, haya utayaweza? Funguka !!
 
Membe na mbio za ikulu.Huku nao Chadema wanagombania kupata nafasi wakati wanajua ikulu kwao ni ishu.Zitto mwachie kibabu kikajifie kuzunguka nchi nzima lazima kife

Kuna watu mnaharibu sifa ya jF mnaleta taarabu...mmmh kumeingiliwa humu
 
Membe na mbio za ikulu.Huku nao Chadema wanagombania kupata nafasi wakati wanajua ikulu kwao ni ishu.Zitto mwachie kibabu kikajifie kuzunguka nchi nzima lazima kife

???Bila shaka haya ni sehemu tu ya mawazo yako mazuri katika ulimwengu wa siasa unayoijua. Bora uliishia hapo vinginevyo..
 
Huyu maembe sijui nyembe anatamba nini wakati mipango yake ilikuwa kuwa wa kwanza kwnye hizo kula katika kundi la bara nakilicho tokea kimemfanya ashindwe bwekea waota njozi za urais wenzake nang'epa namba mmoja mng'emsikia saasa nimeotesha
 
Back
Top Bottom