Maskini Omutwale, chuki na kutumiwa kumekunyima fursa adhimu ya kufanya utafiti wa mambo ambayo ni very basic.
1. Membe amekuwa mbunge wa jimbo la Mtama kuanzia Novemba 2000 na muhula wake wa kwanza ulikwisha mwaka 2005. Katika historia ya jimbo la Mtama hakujawahi kutokea mbunge aliyetekeleza ahadi na kuanzisha miradi ya maendeleo Kama Membe. Kitakwimu, Membe ni kati ya wabunge wachache sana hapa nchini waliowekeza majimboni kwao, labda akitanguliwa na Mh. Nimrod Mkono. Ukiangalia miradi ya maji, afya, elimu na hata miundombinu na masuala ya kiimani utagundua kwamba ulichongea wewe hakina hata chembe ya ukweli kuhusu utendaji wa Membe jimboni kwake. Swali la kujiuliza ni je, ni mgombea yupi, akiwemo Slaa mwenye sifa ya utumishi bora jimboni unaomshinda Membe?
2. Msimamo kuhusu rada ulikuwa ni msimamo wa serikali na Membe Kama waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje. Msimamo wa serikali ulikuwa ni kwamba chenji irejee serikalini, kosa lake Kama mtendaji na mtendaji na mtekelezaji wa maamuzi ya baraza la mawaziri ni nini? Mgombea makini angefanya tofauti na hivyo? Hiyo isingeitwa insubordination? Msimamo wa mgombea wako makini katika hili ni upi?
3. Hakuna siri kwamba Gadaffi alikuwa ni kiongozi wa nchi ambayo ilikuwa na uhusiano na Tanzania. Uhusiano huu haukuanza leo na wala haukuanza wakati wa uwaziri wa Membe. Leo hii hata ICC wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo chake. Hii ni kwa vile kilikuwa cha kikatili na kisichostahili katika mazingira hayo. Msimamo wa serikali wakati wote ni kutatua mgogoro huu kwa amani. Ndiyo ulikuwa msimamo wa AU pia. Mtu anaweza asiupende msimamo huo lakini kwa kutokubaliana nao haumfanyi Membe kuwa mtu asiyefaa kuwa Rais japonica yeye mwenyewe hajawahi kutangaza nia.
4. Suala la mahakama ya kadhi na suala la OIC ambayo ni moja ya kero za muungano lililo chini ya wizara ya nje yalikuwa ni sehemu ya ahadi za CCM kwa wana chi 2005 na walioitunga ilani hiyo wanafahamika na winging leo ndo wapiga debe wa baadhi ya wagombea wanaosifiwa sana. Yeye alijibu kwamba watu waache kuwatia wananchi hofu juu ya OIC na badala yake waachwe wajadili faida na hasara zake na baadae akaliarifu bunge juu ya kusitishwa kwa mchakato kuruhusu mageuzi ndani ya taasisi hiyo. Tatizo liko wapi?
5. Siri za baraza! Kichekesho Kikubwa! Ilibainika kwamba Membe hakuwepo kwenye kikao husika na isingewezekana avujishe siri ambazo alikuwa hazijui na Rais alipogundua kwamba hizo ni adolescent machinations za waliokata tamaa akazipuuza na watuhumu (those who were baying for Membe's blood) wakaaibika sana.
Ninachokiona katika thread hii ni woga na kuweweseka kwa mgombea mmoja ambaye kila mara amekuwa akijigamba kuwa na mtaji wa kimtandao lakini kila siku ushahidi wa kumiss kujiamini kwake kunadhihiri, kwa kupaka matope wenzie, kuwatisha na hata kudiriki kudhuru wenzie. Lakini si ni vyema tukahoji miaka zaidi ya 20 ya ubunge wa jimbo lake ana nini la kujivunia? Na ile ahadi ya ng'ombe kwa kila kaya chini ya "kopa ng'ombe lipa ng'ombe" ya mwaka 2003 kule mikoa ya kusini imeishia wapi?
Hoja yako haina mashiko na haina mnunuzi kwa sababu imekosa chembe chembe muhimu za kuipa sifa ya kujadiliwa kwa mapana. Ndo maana kuna kujihami kwingi. Mradi umeanza, basi utapata haki yako.