Wana JF mimi naomba kuuliza, hivi Tamasha hili la Pasaka liliandaliwa na nani? Madhumuni yake yalikuwa ni nini? Mbona sijamsikia mtu yeyote toka ktk Kamati iliyoandaa Tamasha hili akilalamika kwa namna yeyote? Kila mtu aliyehusika ktk Tamasha hili amefurahia sana, hivi haya maneno yanatoka wapi? Huoni kama uharibu shughuli ya wenzio ambayo ilifanikiwa sana? Ni vizuri zaidi mtoa hoja akatueleza ni wakati gani Membe alizomewa? Maana nimepitia video ya tukio zima toka Membe alipoingia uwanjani hadi alipotoka, sijaona hata sehemu moja alipozomewa, zaidi ya kushangiliwa. Kwa mantiki hii, nina wasi wasi na mtoa hoja huenda ana agenda yake ya siri na Mh. Membe. Na wengi wanaomchukia Membe ni MAFISADI au wale wanaomuona kuwa ni tishio ktk medani za kisiasa.