Membe katika tamasha la Pasaka uwanja wa taifa

kumzomea mtu si heshima,ni dalili za kukosa ubinadamu
When people they have got no other way to show their dissatisfaction they resort to extreme measures, so long as its non violence I don't see any problem (this so called viongozi they don't listen to reason), therefore may this will grab their attention
 
Ukweli niliouona kwenye tamasha la pasaka.



nadhani aliyeleta thread hii aliona aibu baada ya ajenda yake ailiyotaka itokee kwa Membe haijatokea. Mfano sijaona mtu aliyeweka vidole viwili kwa maana ya alama ya Chadema pale Uwanja wa Taifa. hakukuwa na Chembe hata ya Chadema.

nimependa sana style ya Membe kuongea na maskofu karibu wa Makanisa makubwa nchiini akiwemo alinikisa Cheyo wa Kanisa la Moravian, Muadhama Polycarp Pengo, Askofu Dr Alex Malasusa, Askfu Mokiwa wa Anglican, Gamnywa na Maskofu wengine. Kila aliyeongea naye alikuwa na ujumbe kuhusu tamasha.

Membe alianza hotuba yake kwa kueleza maskitiko kwamba tathnia ya sanaa imepata msiba mkubwa kwa kupotelewa na Mwigizaji Steven Kanumba kufuatia kifo cha ghafla kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 8 Aprili,2012. Ameeleza kuskitishwa sana na msiba huo mkubwa. Kanumba alikuwa Balozi wetu mkubwa nje, umasrufu wake ulifika hatankuke ambako nchi yetu haina Ubalozi, na kupitia uigizaje wake, ameweza kuwa mgeni wa familia nyingi kwenye sebule zaokupitia luningani. Naomba tusimame dakika moja tumuombee na kumtakia heri. Bwana ameleta, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana na lihimidiwe!. Aligusia pia suala la kifo cha Rais wa Malawi.

akagusia umuhimu wa Tamasha na Muziki kwamba wa Nyimbo za Injili ni kipimo kizuri cha uvumilivu wa kiimani na dini nchini. Nyimbo hizi zimevuta mashabiki kutoka dini zote na marika yote. Zinaeneza ujumbe ulio mkuu kuliko dini zetu, ujumbe wa upendo, maisha ya uadilifu na utukufu wa Mungu. Ni jambo la kawaida kumpigia simu Ally na kusikia mlio wake wa simu ukiimba wimbo wa injili. Aidha, kwenye maharusi, nyimbo hizi hutumiwa na makundi ya zawadi ambamo ndani yake hujumuisha wakristo na waislamu pia. Huu ndio Utanzania.

Taarifa kamili ya aliyosema Membe nimeinukuu hapa chini kama ifuatavyo.


- Tunayo kila sababu ya kuwashukuru wenzetu wa dini ya kiislamu na imani nyingine kwa uvumilivu wao, ushirikiano wao na uelewa wao. Ni kwa sababu hiyo, wakristo mnapata fursa ya kuendeleza kazi zenu za kiimani na uhuru wa kuabudu. Hivyo, wakristo wanayo kila sababu na wajibu wa kuhakikisha uhuru wao wa kuabudu haukwazi imani na dini nyingine. Tukitambua kuwa hakuna uhuru usio na mipaka, wala haki isiyo na wajibu, daima tutaiepusha nchi yetu dhidi ya shari za kidini, na wote tutakuwa salama.

- Taifa letu linapita katika majaribu makubwa sana ambayo yanatikisa baadhi ya nguzo za umoja na utaifa wetu. Vitendo vya ufisadi, kuporomoka kwa maadili ya viongozi, mfumuko wa bei na kuyumba kwa uchumi wa dunia kumesababisha hali ya kukata tamaa kwa baadhi ya watu; kumepandikiza chuki; na kumechochea ubinafsi kutokana na kukosekana kwa haki na matumaini kwa wananchi walio wengi. Nawashukuru sana viongozi wa dini kwa na wasanii wa nyimbo za injili kwa kuendelea kusisitiza amani, kutoa matumaini na kutuunganisha pamoja. Mungu ana mpango na Taifa hili. Majaribu haya ni mapito na yatapita. Nabii Suleimani alisema, " kila jambo lina wakati wake na sababu yake juu ya nchi, kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna, wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa". Serikali yenu inasikia kilio chenu na machungu yenu, inachukua hatua za muda wa kati na muda mrefu, baadhi ya matokeo mtayaona karibuni, baadhi yatachukua muda. Hakuna machungu yasiyo na mwisho.

-Tunaelekea kwenye mchakato wa Katiba mpya ambalo ni jaribio lingine. Jaribio ambalo tukifanikiwa kulivuka tutakuwa tumefikia nchi ya ahadi, Tanzania tunayoitarajia. Watakuja wengi wenye maelezo mazuri kuhusu Tanzania ya ahadi. Wengine watatumia muda huo kuleta uchochezi, tuwapuuze. Tanzania tunayoitaka ni Tanzania inayomwogopa Mungu, Tanzania inayodumisha upendo, Tanzania inayovumilia imani na dini mbalimbali, Tanzania isiyobaguana na Tanzania yenye neema tele zitokanazo na rasilimali zake, Tanzania ambayo kila mtu ana fursa ya kuchangia maendeleo na kuneemeka na fursa zitokanazo na mchango wake, Tanzania ambayo wasanii, wataalamu, wakulima, wanasiasa, wavuvi, wanawake kwa wanaume, wazee kwa vijana, viongozi na raia, wapinzani na chama tawala wote wana fursa na haki sawa,naam, Tanzania hii inawezekana. Shime tutumie fursa ya mabadiliko ya Katiba kuifikisha nchi yetu huko.
 
Kukuta kwenye blogs sio kigezo mkuu.
Kuna watu kama nyie mlio busy kueneza uongo kwenye mitandao
OTIS

OTIS ndugu yangu usidanganye watu ukidhani siku hizi kuna la kuficha ndo maana tunashindwa kuwambia ukweli hawa viongozi wajirekebishe sijui anakupatia nini ama wewe ndo yeye. Membe kazomewa sana uwanja wa taifa na watu kunyanyua vidole viwili juu. Nilikuwepo hapo na watu walicholalamikia ni hotuba ndefu ndefu ambazo wao wameona kama za kisiasa na kuhusisha na UCCM. Ukweli kama we ni wa kundi lake katika makundi mengi ambapo si kosa lakini usidanganye na kuwadanganya watu. Membe kazomewa hadi mi personally nilifedheheka kuwa kwa nini hawa viongozi hawasomi alama za mahali. Mi nampa pole lakini afanye utafiti ajue chanzo chake lakini msipotoshe na kuwadanganya watu kuwa alishangiliwa. Hata juzi uchaguzi wa Arumeru mlikuwa mnaambiwa hali mbaya mnasema hizo kura za mjini baadaye wengi wenu hamkuonekana hapa hadi tukadhani bp zimewachukua. Tukubali ukweli ili tujirekebishe na kusonga mbele na nasisitiza MEMBE AMEZOMEWA MBAYA
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Naona hata heading imebadilika "Hakuzomewa, kashangiliwa" Kama mnataka hivyo anzisheni thread nyingine. Mimi ni mmoja wapo waliokerwa na hotuba ya Waziri Membe. Nilipoona anaendelea kuniboa nikaenda zangu pale Minazini kuangalia Arsenal vs Man City.
 
Sio kweli kwamba Mh. Membe amezomewa leo. Huyo aliyeleta post hii ni MUONGO MKUBWA. Membe ameshangiliwa saaaana na umati mkubwa uliopo uwanjani. Namshangaa sana

mnafiki na mwongo wewe unayeonekana una tumiwa kama kopo la chooni mtu akishikwa haja analitafuta akimaliza hataki hata kuliangalia
 
OTIS ndugu yangu usidanganye watu ukidhani siku hizi kuna la kuficha ndo maana tunashindwa kuwambia ukweli hawa viongozi wajirekebishe sijui anakupatia nini ama wewe ndo yeye. Membe kazomewa sana uwanja wa taifa na watu kunyanyua vidole viwili juu. Nilikuwepo hapo na watu walicholalamikia ni hotuba ndefu ndefu ambazo wao wameona kama za kisiasa na kuhusisha na UCCM. Ukweli kama we ni wa kundi lake katika makundi mengi ambapo si kosa lakini usidanganye na kuwadanganya watu. Membe kazomewa hadi mi personally nilifedheheka kuwa kwa nini hawa viongozi hawasomi alama za mahali. Mi nampa pole lakini afanye utafiti ajue chanzo chake lakini msipotoshe na kuwadanganya watu kuwa alishangiliwa. Hata juzi uchaguzi wa Arumeru mlikuwa mnaambiwa hali mbaya mnasema hizo kura za mjini baadaye wengi wenu hamkuonekana hapa hadi tukadhani bp zimewachukua. Tukubali ukweli ili tujirekebishe na kusonga mbele na nasisitiza MEMBE AMEZOMEWA MBAYA
Laingwanani's activist at work.........
 
nimependa sana style ya Membe kuongea na maskofu karibu wa Makanisa makubwa nchiini akiwemo alinikisa Cheyo wa Kanisa la Moravian, Muadhama Polycarp Pengo, Askofu Dr Alex Malasusa, Askfu Mokiwa wa Anglican, Gamnywa na Maskofu wengine. Kila aliyeongea naye alikuwa na ujumbe kuhusu tamasha.

Aligusia pia suala la kifo cha Rais wa Malawi.
.

Tangu lini Membe akawa msemaji wa makanisa? Anasema ana ujumbe wa maskofu toka kanisa katoliki, anglican, Lutheran, Morovian! Yeye ni nani kwenye haya makanisa mpaka apewe jukumu la kupeleka salamu kwa wananchi? Ni siku chache tu Lowassa alivamia huko Ifakara, sasa Membe naye anakuja na style yake! Hawa watu wa CCM wana matatizo gani?

Kama haitoshi Membe anaongelea mambo ya Bingu wa Mutharika? Amejisahau kwamba hapo siyo Malawi?

Kuna tabia inatia kichefuchefu ya viongozi wa CCM kugeuza makanisa kuwa majukwaa ya siasa. Viwanja vya Kawe kila Jumapili siku hizi kuna ibada nyingi pale na kunakuwepo na kiongozi mmoja wa ccm maalum kwa propaganda. Halafu hawa hawa hawa ccm utawasikia wanalia 'udini'. Wamefilisika humo vichwani sasa wanakimbilia makanisani. Watafukuza waumini kama walivyofukuza watu toka kwenye chama chao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom