Hujaelewa. Kuwapa watu uraia wa nchi mbili kunawafungulia milango huku kwetu ikiwa kule waliko wana uhuru wa kujiedeleza kiuchumi kama raia wa kule, kitu ambacho kwa sasa tunawazuia. Inachotokea ni kwamba kule waliko wanakwamishwa kufanya mambo fulani kama kuwekeza au kumiliki vitu fulani kwa kuwa wao sio raia wa nchi zile, na wao wanaogopa wakichukua uraia wa zile nchi watapoteza uraia wa Tanzania, kulingana na sheria ya uraia ya Tanzania ya sasa.
Tunasema kwamba, kama tukiwaruhusu kuwa raia wa nchi mbili, maendeleo yao ya kiuchumi kule waliko yatakuwa rahisi, kwa kuwa wataruhusiwa kumiliki au kufanya mambo yote ya kukuza uchumi wao waliko wakiwa raia wa nchi hizo. Hiyo ikitokea inakuwa rahisi kwa mapato yao ku-overflow kuja Tanzania ambako wana ndugu, viwanja, na assets nyingine ambazo watakuwa na uwezo wa kuziendeleza.
Mfano, Mtanzania aliyeko Ethiopia haruhusiwi hata kumiliki nyumba kama sio raia wa Ethiopia, hata kama ameoa Mu-Ethiopia. Kwa hiyo ili akue kiuchumi akiwa Ethiopia itabidi aukane uraia wa Tanzania ili achukue wa Ethiopia. Sasa akisha chukua uraia wa Ethiopia na kuwa sio raia wa Tanzania tena, anakosa haki ya mambo mengi tu aliyokuwa nayo Tanzania. Hata kama alikuwa na mashamba au viwanja hapa nyumbani, kisheria mashamba hayo na viwanja sio vyake tena. Akijua hili sio rahisi kwamba ataviendeleza. Sanasana ataishia kuwapa ndugu zake ambao labda kwa sababu za umasikini hawawezi kuviendeleza.
Na pia, ikiwa huyo Mtanzania aliyeko Ethiopia na aliechukua uraia wa Ethiopia anataka kutuma hela Tanzania, serikali ya Ethiopia haitamruhusu kirahisi. Ni sawa na wewe leo jaribu kutuma fedha za kigeni nje ya nchi utaona ilivyo ngumu. Kwanza huruhusiwi kama huna sababu kama kutibiwa, mtoto anasoma sijui nk. Lakini, ikiwa Ethiopia itaruhusu uraia wa nchi mbili, na huyo Mtanzania aliyechukua uraia wa Ethiopia akasema anataka kutuma hela Tanzania ambako kwake ni nyumbani pia, basi kunakuwa na taratibu zinazomruhusu kufanya hivyo. Lakini ikiwa Tanzania ilimnyanganya uraia baada ya yeye kuchukua uraia wa Ethiopia, Ethiopia wanaweza kumkataza kabisa kutuma hela zake Tanzania ambako sio raia tena!
Sasa jaribu kuwaelewesha na wale wengine wote wanaoleta pointi zao za vijiweni hapa kukataa uraia pacha, ooh sijui uzalendo, sijui tukipigana vita watakuwa upande gani!