Membe asisitiza kuhusu uraia wa nchi mbili

Happy nation

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
679
591
Leo waziri wa mambo ya nje mbwana membe amesema haoni sababu ya kuwakomoa diaspora wasiwe na uraia wa nchi mbili,ukweli tuna wahitaji ndugu zetu walioko nje kujenga uchumi wetu na kurudisha taaluma zao nchini na kujisikia hii ni nchi yao pia.

Lakini pia unaporuhusu sheria ya uraia wa nchi mbili siyo tu walioko nje watarudi ila kuna watakao pata fursa ya kuchukua uraia wa nchi ingine na hivyo kuwapa fursa ya kuhamisha mali zao kirahisi na hiyo ndiyo hatari yake.
 
Anaongea kama nani vile, au anatoa maoni kwa lowassa akiingia madarakan arekebishe sheria hiyo.....
 
mimi namuunga mkono membe hajakosea mnyonge mnyongeni haki yake mpeni dada zetu na kaka zetu wamekwama ulaya wanashindwa kuja kujenga nchi huku
 
mimi namuunga mkono membe hajakosea mnyonge mnyongeni haki yake mpeni dada zetu na kaka zetu wamekwama ulaya wanashindwa kuja kujenga nchi huku
 
stemcell

Namuunga mkono. Sioni hasara walizopata mataifa yaliyokubali uraia wa nchi mbili kwa muda mrefu tu sasa, na wale wote mnaopinga hamtoi mifano halisi ya jinsi nchi hizo zimeingia matatizoni kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili, pamoja na nchi jirani kama Kenya na Uganda.

Unajua kila nikisoma sababu za watu wanaopinga uraia pacha nashikwa na hasira unayopata unapomsikiliza mlevi akiongea pumba. Tatizo letu Watanzania tunapenda kubisha bila kuwa na facts, tunaishia ku-speculate tu. Hivi mnafikiri kutorosha mali kwenda nje ya za nchi ni rahisi kiasi hicho, kama watu wanavyofanya madawa ya kulevya?

Mnatoa hadithi za vijiweni huko mnataka ndio uwe msimamo wa serikali. Sijui kukosa uzalendo, sijui tukipigana vita watakuwa upande gani, ooh sijui watatorosha mali na siri za nchi. Hamna lolote la maana mnaongea, pumba tupu kama vile tu ni mjadala unafanyika kwenye shule ya chekechea. au klabu ya ulanzi, kayoga, mbeke, kangara, wanzuki, pyuwa, mataptap, nk. Kama ligi ni kubwa kukuzidi kaa kando acha wenye kelewa mambo waicheze kuliko kuleta hadithi za vijiweni kuhusu uraia pacha.
 
Last edited by a moderator:
Mantiki ya bwana Membe haieleweki, ikiwa anpita humu naomba anijibu, wawekezaji hata wasio na asili ya Tanzania wanapewa kipaumbele sasa hawa wenye asili ya Tanzania wanashindwa nini kuja kuwekeza? Sio lazima wapewe uraia ndipo wa nchi 2 ndipo waje, tumewakaribisha watu tofauti hatutashindwa kuwakaribisha hawa waliokua raia wa Tanzania kuwekeza, ikizingatiwa kuwa wana hata familia zao huku. SIO LAZIMA WAPATE URAIA WA NCHI 2 NDIPO WAWEKEZE. NINAVYOFAHAU NI KUWA MAREKANI HAIKUBALI URAIA WA NCHI 2( Membe amesema ni Tanzania tu ndio haikubali), URAIA WA NCHI 2 UNAONDOA UZALENDO, MNAMKUMBUKA ALBERTO FUJIMORI ALIKUA RAIS WA PERU LAKINI PIA ANA URAIA WA JAPAN? ALIPOHARIBU PERU ALIKIMBILIA KWAO JAPAN, TAFAKARI.
 
Namuunga mkono. Sioni hasara walizopata mataifa yaliyokubali uraia wa nchi mbili kwa muda mrefu tu sasa, na wale wote mnaopinga hamtoi mifano halisi ya jinsi nchi hizo zimeingia matatizoni kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili, pamoja na nchi jirani kama Kenya na Uganda.

Unajua kila nikisoma sababu za watu wanaopinga uraia pacha nashikwa na hasira unayopata unapomsikiliza mlevi akiongea pumba. Tatizo letu Watanzania tunapenda kubisha bila kuwa na facts, tunaishia ku-speculate tu. Hivi mnafikiri kutorosha mali kwenda nje ya za nchi ni rahisi kiasi hicho, kama watu wanavyofanya madawa ya kulevya?

Mnatoa hadithi za vijiweni huko mnataka ndio uwe msimamo wa serikali. Sijui kukosa uzalendo, sijui tukipigana vita watakuwa upande gani, ooh sijui watatorosha mali na siri za nchi. Hamna lolote la maana mnaongea, pumba tupu kama vile tu ni mjadala unafanyika kwenye shule ya chekechea. au klabu ya ulanzi, kayoga, mbeke, kangara, wanzuki, pyuwa, mataptap, nk. Kama ligi ni kubwa kukuzidi kaa kando acha wenye kelewa mambo waicheze kuliko kuleta hadithi za vijiweni kuhusu uraia pacha.
Umeanza vizuri lakini hapo mwisho umeharibu, hamna sababu ya kukashifu. wewe eleza faida ambazo taifa litapata kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili ambazo haziwezi kupatikana kwenye mazingira ya sasa.
 
Mantiki ya bwana Membe haieleweki, ikiwa anpita humu naomba anijibu, wawekezaji hata wasio na asili ya Tanzania wanapewa kipaumbele sasa hawa wenye asili ya Tanzania wanashindwa nini kuja kuwekeza? Sio lazima wapewe uraia ndipo wa nchi 2 ndipo waje, tumewakaribisha watu tofauti hatutashindwa kuwakaribisha hawa waliokua raia wa Tanzania kuwekeza, ikizingatiwa kuwa wana hata familia zao huku. SIO LAZIMA WAPATE URAIA WA NCHI 2 NDIPO WAWEKEZE, NINAVYOFAHAU NI KUWA MAREKANI HAIKUBALI URAIA WA NCHI 2, URAIA WA NCHI 2 UNAONDOA UZALENDO, MNAMKUMBUKA ALBERTO FUJIMORI ALIKUA RAIS WA PERU LAKINI PIA ANA URAIA WA JAPAN? ALIPOHARIBU PERU ALIKIMBILIA KWAO JAPAN, TAFAKARI.

Hujaelewa. Kuwapa watu uraia wa nchi mbili kunawafungulia milango huku kwetu ikiwa kule waliko wana uhuru wa kujiedeleza kiuchumi kama raia wa kule, kitu ambacho kwa sasa tunawazuia. Inachotokea ni kwamba kule waliko wanakwamishwa kufanya mambo fulani kama kuwekeza au kumiliki vitu fulani kwa kuwa wao sio raia wa nchi zile, na wao wanaogopa wakichukua uraia wa zile nchi watapoteza uraia wa Tanzania, kulingana na sheria ya uraia ya Tanzania ya sasa.

Tunasema kwamba, kama tukiwaruhusu kuwa raia wa nchi mbili, maendeleo yao ya kiuchumi kule waliko yatakuwa rahisi, kwa kuwa wataruhusiwa kumiliki au kufanya mambo yote ya kukuza uchumi wao waliko wakiwa raia wa nchi hizo. Hiyo ikitokea inakuwa rahisi kwa mapato yao ku-overflow kuja Tanzania ambako wana ndugu, viwanja, na assets nyingine ambazo watakuwa na uwezo wa kuziendeleza.

Mfano, Mtanzania aliyeko Ethiopia haruhusiwi hata kumiliki nyumba kama sio raia wa Ethiopia, hata kama ameoa Mu-Ethiopia. Kwa hiyo ili akue kiuchumi akiwa Ethiopia itabidi aukane uraia wa Tanzania ili achukue wa Ethiopia. Sasa akisha chukua uraia wa Ethiopia na kuwa sio raia wa Tanzania tena, anakosa haki ya mambo mengi tu aliyokuwa nayo Tanzania. Hata kama alikuwa na mashamba au viwanja hapa nyumbani, kisheria mashamba hayo na viwanja sio vyake tena. Akijua hili sio rahisi kwamba ataviendeleza. Sanasana ataishia kuwapa ndugu zake ambao labda kwa sababu za umasikini hawawezi kuviendeleza.

Na pia, ikiwa huyo Mtanzania aliyeko Ethiopia na aliechukua uraia wa Ethiopia anataka kutuma hela Tanzania, serikali ya Ethiopia haitamruhusu kirahisi. Ni sawa na wewe leo jaribu kutuma fedha za kigeni nje ya nchi utaona ilivyo ngumu. Kwanza huruhusiwi kama huna sababu kama kutibiwa, mtoto anasoma sijui nk. Lakini, ikiwa Ethiopia itaruhusu uraia wa nchi mbili, na huyo Mtanzania aliyechukua uraia wa Ethiopia akasema anataka kutuma hela Tanzania ambako kwake ni nyumbani pia, basi kunakuwa na taratibu zinazomruhusu kufanya hivyo. Lakini ikiwa Tanzania ilimnyanganya uraia baada ya yeye kuchukua uraia wa Ethiopia, Ethiopia wanaweza kumkataza kabisa kutuma hela zake Tanzania ambako sio raia tena!

Sasa jaribu kuwaelewesha na wale wengine wote wanaoleta pointi zao za vijiweni hapa kukataa uraia pacha, ooh sijui uzalendo, sijui tukipigana vita watakuwa upande gani!

Umeanza vizuri lakini hapo mwisho umeharibu, hamna sababu ya kukashifu. wewe eleza faida ambazo taifa litapata kwa kuruhusu uraia wa nchi mbili ambazo haziwezi kupatikana kwenye mazingira ya sasa.

Mkuu, kuna wakati huwa naelewa kwa nini Muhongo alisema Watanzania tukafanye biashara ya kuuza juice.

Hata hivyo, soma maelezo yangu ya kirefu kuhusu uraia pacha hapo juu.

Sipendi kubishana na mtu anaebishia kitu asichoelewa, napenda huyo mtu asibishe bali aombe kuelimishwa. Ndio maana sipendi kumsikiliza mlevi akitoa pointi zake.
 
Back
Top Bottom