Membe asihusishwe na wanaotajwa katika IPTL

Bwana Kiwuyo

Member
Joined
Oct 6, 2013
Posts
8
Reaction score
3
Jamii Forums ni moja ya vyanzo vya habari au tetesi zinazoendelea nchini iwe ni za ukweli au za uwongo.Ila kwa asilimia kubwa habari za Jamii Forums ni za kimihemko zaidi na kuvunjiana heshima au kuharibiana malengo na maisha ya kisiasa,uchumi au kijamii.

Sisi marafiki zake Membe tumesoma mjadala unaohusu sakata la Iptl lililoibuliwa na Kafulila ndani ya Bunge la Bajeti miezi kadhaa nyuma humu Jamii Forums tangu lilipoanza hadi lilipofikia sasa.Wanatajwa wafanyabiashara,majaji na wanasiasa kuhusika na sakata hili linaloigharimu nchi na serikali kwasasa.

Baadhi ya waliotajwa yupo pia Jack Gotham!Hatujajua ni misingi ipi au ushahidi upi ambao umetumika kumtaja Jack Gotham na kumuunganisha Membe katika sakata hili.Haina maana ukiwa rafiki na mtu basi uhusishwe na kila baya analofanya.Membe asihusishwe na Iptl kwasababu tuna imani kubwa kwamba hakuna ushahidi either direct au indirect unaomgusa katika Iptl.

Membe ni kati ya makada wa Ccm ambao hawaungi mkono pesa za Iptl(escrow)kuchotwa BOT.Membe hana historia yoyote mbaya ya kuhusika au kujihusisha na ufisadi wa aina yoyote ile ndani na nje ya nchi.Na pia Membe hawezi kuambatana na fisadi au mla rushwa.

Kama kweli Jack Gotham anahusika kwa namna moja au nyingine katika Iptl Saga basi tuna imani Membe ambaye sisi ni rafiki yetu atachukua hatua za nini afanye ili kuhakikisha haki inapatikana kwa kutoa ushirikiano wa namna moja au nyingine ili wahusika wa Iptl Saga wawajibishwe na huo ndio uzalendo ambao Membe anao.

Tunatoa wito kuwa watanzania msiaminishwe lolote kuwa Membe anahusika kwenye sakata la Iptl na asihusishwe na yeyote aliyeshiriki katika sakata la Iptl.Ahsanteni sana!

Imetolewa na Friends Of Hon.Membe.
 
vipi kuhusu zile hoteli mbili mtwara moja imeisha na inafanya kazi nyingine ndio inajengwa,,,,kuna haja ya kumtumia yule mmachinga kujificha nyuma ya mtumwingine,kama ni fedha za halali unaonaje hapo
 
Rafiki wa mwizi naye ni mwizi.
 
by rosemarie;
vipi kuhusu zile hoteli mbili mtwara moja imeisha na inafanya kazi nyingine ndio inajengwa,,,,kuna haja ya kumtumia yule mmachinga kujificha nyuma ya mtumwingine,kama ni fedha za halali unaonaje hapo



cc
Bwana Kiwuyo Usijifanye hujaona anachoeleza mkuu rosemarie hapo juu!
 
Last edited by a moderator:
kumhusisha Jack Gothan na IPTL Saga hawana lolote zaidi ya kutaka kumchafua Membe kwa mlango wa nyuma. Ni political science ya kawaida sana kwamba ukimshindwa mtu au mchungaji basi piga kondoo wake watawanyike ili uweze kumvaa kirahisi. Hata hivyo kwa wengine tumebahatika kuchungulia report ya ESCROW na hata bankstatement hakuna mahali POPOTE jina la Jack Gothan linatajwa iwe hata kwa kampuni yake au vinginevyo. Tunajua kuwa Jacky ni kiboko na mwiba na mfupa kooni kwa ****** na timu yake. Huko ni kutapatapa na dalili za kushindwa na ni ishara kuwa Membe ni threat.
 
kosa kubwa ulilolifanya ni kusema jf ipo kimihemko zaidi wakati tiss wanapeana zamu kuhudhuria humu. Membe ni ntu wa karibu sana na jk na jk ni moja ya walioileta kampuni ya kuuza mpunga kuja kuwekeza kwenye MW tz.

mpaka unakuja kumtetea membe humu maana yake habari za humu ni ukweli mtupu
 
Membe si mmiliki wa hoteli yeyote nchini na kwingineko. Taarifa ya usalama wa taifa iliyoratibiwa na mahasimu wa Membe ilihitimisha kwamba Membe sio mmiliki. Shaibu Juma ni mmiliki wa hotel na kwamba ela za ujenzi alipata kwa mkopo crdb na udalali wa korosho kwa wahindi ndivyo report inavyosema.
 
Wewe ni memaji wa membe au unazungumza kwa niaba ya membe kama nani?
 

krappppppppp....
 
Hili bandiko ndio limekaa kimemhuko zaidi maana halina uthibitisho wala haujasema umetumwa au umekurupuka tu duh nahisi wewe uko kwenye payroll mbili ya Lumumba buku 7 na ya Membe kwa wakati mmoja.
 
Mbona?!? Na kwa lipi hadi kutajwa? Uthibitisho ni yeye kutoka hadharani na kuukana aina yoyote ya ufisadi anaohusishwa na sio wewe mleta uzi kumsemea. Anaogopa nini? Na zile za marehemu Gaddaf wa iliyokuwa Libya alizokuwa anataka kujengea kiwanda cha saruji huko Lindi lilikwishaje?
Nchi hii wapigaji wengi hasa waliopo kwenye safu ya mteule wetu. Huyu atashindwaje kukwapua ili hali wenzake wanakula hata za marehemu tena bila haya? Yeye ana umalaika gani tofauti na hao wenzie hasa ukizingatia umahiri wake kitaaluma? Ni rahisi sana kufanya lobbing ili wengine wachafuke but hawezi kuukwepa uchafu na wizi ulioshamiri ccm. Mtoe hadharani aseme.
 
Wezi wakubwa WA nchi wanatoka kaskazini mwa nchi wakiongozwa baba LA mafisadi LA Richmond lowasaaaa.
 
Wakuu hii imekaa vema! Nadhani ni muda muafaka tujiulize kama huyu anayetuhumiwa anapaswa kub aki kwnye Kambi yetu. Tunaweza muacha ili abaki na tuhuma zake na Kambi yetu ibaki safi! Mwisho Mzee Membe atoe statement kama hawezi amwambie mwenzetu Mwambene atasaidia kusafisha hili! Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…