Membe apigia chapua uraia wa nchi mbili Katiba mpya

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1] [/h]Na Enles Mbegalo

23rd January 2014

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na waandishi baada ya kufungua mkutano unaojadili faida za uraia wa nchi mbili jijini Dsm jana.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewaomba wabunge, wasomi na Watanzania wawasaidie Bunge la Katiba ili liweze kupitisha hoja ya Watanzania kuwa na uraia wa nchi mbili ili uchumi wa nchi uweze kukua.

Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana kwenye ufunguzi wa semina ya majadiliano ya Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

“Kuna wasomi wengi wenye utalaamu wapo nchi za nje wanafanya kazi ila wanashindwa kusaidia nchi zao kwa kuwa hawana uraia wa nchi zao,” alisema Membe.

Alisema kumruhusu Mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili siyo kuhatarisha usalama wa nchi. “Anayeweza kuhatarisha usalama wa nchi ni sisi viongozi.

Sisi hatutetei hii hoja ya kuwa na uraia wa nchi mbili ila lazima ufike wakati tuamue kufanya hivi sio uhaini” alisema.

Alisema nchi nyingine ambazo raia wao wana uraia wa nchi mbili wamekuwa wakichangia uchumi wa nchi hizo kwa asilimia kubwa tofauti na nchi yetu.

Alitoa mfano wa nchi ya Ghana kuwa raia wake wenye uraia wa nchi mbili wamekuwa wakichangia uchumi wa nchi hiyo kila mwaka.

“Ghana wanachangia bilioni 2.1, Nigeria milioni 3.1, Kenya bilioni 1.6 ambazo ni dola za Marekani” alisema.

Alisema kwa Tanzania fedha zinazochangiwa na raia wake waliopo nje hazifiki hata 100,000 za Marekani, hali inayozorotesha uchumi wa nchi.

Upande wake, Msaidizi wa Waziri Mkuu Kitengo cha Uchumi na Uwekezaji, Suzani Mzee alisema Tanzania inaelekea kwenye uraia wa nchi mbili ambao utasaidia kuchangia maendeleo ya nchi.

“Mtanzania anayeishi nchi za nje anatoa misaada kwa kificho kwa kuwa hana uraia wa nchi yake ana uraia wa nchi anayoishi ifike wakati serikali ituunge mkono ili tuweze kuisaidia nchi yetu pasipo kificho,”alisema

CHANZO: NIPASHE
 
Jamani watanzania tuamkeeee uraia wa nchi mbili ni bomu la nyuklia mmeona tulivyouziwa mbuzi kwenye gunia kuambiwa balali si mtania alishachukua uraiya wa nchi nyingine chondechonde watanzania tusikubali uraia wa nchi 2 hawa wameshashtukia mbeleni segerea inawaita wanakimbilia kuhodhi uraia wa nchi mbili kikinuka wakimbilie ughaibuni ili tushindwe kuwakamata chukueni mifano km ya akina alex masawe hatukawii kusikia mkulu nae si mtanzania ni mmarekani yetu macho.
 
Na Enles Mbegalo

23rd January 2014

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na waandishi baada ya kufungua mkutano unaojadili faida za uraia wa nchi mbili jijini Dsm jana.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewaomba wabunge, wasomi na Watanzania wawasaidie Bunge la Katiba ili liweze kupitisha hoja ya Watanzania kuwa na uraia wa nchi mbili ili uchumi wa nchi uweze kukua.

Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana kwenye ufunguzi wa semina ya majadiliano ya Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

"Kuna wasomi wengi wenye utalaamu wapo nchi za nje wanafanya kazi ila wanashindwa kusaidia nchi zao kwa kuwa hawana uraia wa nchi zao," alisema Membe.

Alisema kumruhusu Mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili siyo kuhatarisha usalama wa nchi. "Anayeweza kuhatarisha usalama wa nchi ni sisi viongozi.

Sisi hatutetei hii hoja ya kuwa na uraia wa nchi mbili ila lazima ufike wakati tuamue kufanya hivi sio uhaini" alisema.

Alisema nchi nyingine ambazo raia wao wana uraia wa nchi mbili wamekuwa wakichangia uchumi wa nchi hizo kwa asilimia kubwa tofauti na nchi yetu.

Alitoa mfano wa nchi ya Ghana kuwa raia wake wenye uraia wa nchi mbili wamekuwa wakichangia uchumi wa nchi hiyo kila mwaka.

"Ghana wanachangia bilioni 2.1, Nigeria milioni 3.1, Kenya bilioni 1.6 ambazo ni dola za Marekani" alisema.

Alisema kwa Tanzania fedha zinazochangiwa na raia wake waliopo nje hazifiki hata 100,000 za Marekani, hali inayozorotesha uchumi wa nchi.

Upande wake, Msaidizi wa Waziri Mkuu Kitengo cha Uchumi na Uwekezaji, Suzani Mzee alisema Tanzania inaelekea kwenye uraia wa nchi mbili ambao utasaidia kuchangia maendeleo ya nchi.

"Mtanzania anayeishi nchi za nje anatoa misaada kwa kificho kwa kuwa hana uraia wa nchi yake ana uraia wa nchi anayoishi ifike wakati serikali ituunge mkono ili tuweze kuisaidia nchi yetu pasipo kificho,"alisema

CHANZO: NIPASHE

Katika dunia ya leo hii ambayo ni kijiji, hatuna budi kuingia katika uraia wa nchi mbili ili tuweze kutumia fursa za kuishi ng'ambo vizuri. Kwa sasa watanzania wengi sana wanapata shida sana kutokana na kutotambua uraia wa nchi mbili. Kwa wale wanaopinga suala hili nafikiri nikutokana na kukosa uzoefu na exposure ya jinsi dunia ya leo ilivyo. Hongera Membe kwa jitihada zako juu ya suala hilo.
Tuache mitizamo ya makundi yenye mlengo wa kisiasa, tutafakari maslahi ya nchi.
 
Membe ni kibaraka Wa mataifa ya ulaya tusimpe nafasi abomoe taifa hili kwa maslai yake ndugu za CCM tunapisha kwa mengi lakini uraia Wa nchi mbili tuwe pamoja na tuweke uzalendo mbele mtu akishasoma njee anajiona yeye ni bora kuliko watanzania wengine..membe na nyalandu ni watu Wa kuwaangalia kwa macho mawili..MTU anachuma Tanzania anaenda ishi Canada.. Angalia waindi wengi wanapesa lakini wamejazana kwa msajili hawajengi Nyumba zao wanakusanya pesa waende Canada au Australia.
Katiba itambue kama wewe ni mtanzania ni mtanzania tu.

Membe ni MTU hatari sana.
 
Tatizo lako umefungiwea ndani ya boksi la kifikra na Wahifadhina wa CCM wenye malengo ya kudumisha maslahi yao binafsi na kuyapuuza maslahi ya Taifa.Uraia wa Nchi mbili ni mzuri sana kiuchumi kwa Tanzania kwakuwa wale Watanzania wenye uraia wa nchi nyingine lakini wanaotaka kujihusisha maswala ya nchi kwa nia ya kusaidia watapata IMANI ya kurudi kusaidia.uliwahi kufikiria hatima ya Tanzanian soccer players walio nje?
 
samahani mkuu,naomba unieleze kwa kina faida za uraia wa nchi mbili kwa taifa hasa hili letu la tanzania.tusilete ushabiki tu bali naomba mambo ya msingi yanayoweza kuipeleka hii nchi katika maendeleo kutokana na uraia wa nchi mbili.
 
watanzania wa kawaida hawaitaji uraia wa nchi mbili..... wanaotaka uraia wa nchi mbili ni wahujumu uchumi mkubwa ili kikinuka apa aweze kukimbia nchi huwezi kuishi kama popo(wakishindwa ndege unakimbilia kwa wanyama wakishindwa wanyama unakimbilia kwa ndege)!!! kuna mtanzania gani anayezuiwa asilete misaada nyumban eti kwa sababu sio raia? kuna watu waliotummiza hapa tz kwa sababu ya urai wa nchi mbili kama kina jeetu patel ndie aliyefadhili mikataba ya ndege mbovu ya rais, rada mtumba kwa bei za kuruka hadi tukaonewa huruma na wabunge wa uingereza tukaambiwa tutakula nyasi ili ndege inunuliwe.... lakini kwa sababu ana uraia wa uingereza mpaka leo hajulikani alipo!!
 
Mojawapo kati ya wagombea wa urais ndani ya CCM ambaye hana sera za kuwabeba maskini ni Membe, hivi kwa mwananchi wa kawaida ambaye hata hiyo pasport hana ukimwelezea Diaspora atakuelewa? Nadhani huyu naye katumwa na mabwenyeye aje atekeleze sera zao.
Anadai eti nchi haindelei kwakuwa watu wanashindwa kuja kuwekeza! Lo! kwani hawa waliopo mbona wamewekeza? Kama tunawatanzania ambao walishauka uraia wa Tanzania waje tu wawekeze kama wageni kwani watapata hasara gani? Kama mtu anataka kuja kuwekeza Tanzania milango ipo wazi na wanamsharti nafuu kweli kweli,

Na Enles Mbegalo

23rd January 2014

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na waandishi baada ya kufungua mkutano unaojadili faida za uraia wa nchi mbili jijini Dsm jana.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe amewaomba wabunge, wasomi na Watanzania wawasaidie Bunge la Katiba ili liweze kupitisha hoja ya Watanzania kuwa na uraia wa nchi mbili ili uchumi wa nchi uweze kukua.

Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana kwenye ufunguzi wa semina ya majadiliano ya Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

"Kuna wasomi wengi wenye utalaamu wapo nchi za nje wanafanya kazi ila wanashindwa kusaidia nchi zao kwa kuwa hawana uraia wa nchi zao," alisema Membe.

Alisema kumruhusu Mtanzania kuwa na uraia wa nchi mbili siyo kuhatarisha usalama wa nchi. "Anayeweza kuhatarisha usalama wa nchi ni sisi viongozi.

Sisi hatutetei hii hoja ya kuwa na uraia wa nchi mbili ila lazima ufike wakati tuamue kufanya hivi sio uhaini" alisema.

Alisema nchi nyingine ambazo raia wao wana uraia wa nchi mbili wamekuwa wakichangia uchumi wa nchi hizo kwa asilimia kubwa tofauti na nchi yetu.

Alitoa mfano wa nchi ya Ghana kuwa raia wake wenye uraia wa nchi mbili wamekuwa wakichangia uchumi wa nchi hiyo kila mwaka.

"Ghana wanachangia bilioni 2.1, Nigeria milioni 3.1, Kenya bilioni 1.6 ambazo ni dola za Marekani" alisema.

Alisema kwa Tanzania fedha zinazochangiwa na raia wake waliopo nje hazifiki hata 100,000 za Marekani, hali inayozorotesha uchumi wa nchi.

Upande wake, Msaidizi wa Waziri Mkuu Kitengo cha Uchumi na Uwekezaji, Suzani Mzee alisema Tanzania inaelekea kwenye uraia wa nchi mbili ambao utasaidia kuchangia maendeleo ya nchi.

"Mtanzania anayeishi nchi za nje anatoa misaada kwa kificho kwa kuwa hana uraia wa nchi yake ana uraia wa nchi anayoishi ifike wakati serikali ituunge mkono ili tuweze kuisaidia nchi yetu pasipo kificho,"alisema

CHANZO: NIPASHE
 
Mojawapo kati ya wagombea wa urais ndani ya CCM ambaye hana sera za kuwabeba maskini ni Membe, hivi kwa mwananchi wa kawaida ambaye hata hiyo pasport hana ukimwelezea Diaspora atakuelewa? Nadhani huyu naye katumwa na mabwenyeye aje atekeleze sera zao.
Anadai eti nchi haindelei kwakuwa watu wanashindwa kuja kuwekeza! Lo! kwani hawa waliopo mbona wamewekeza? Kama tunawatanzania ambao walishauka uraia wa Tanzania waje tu wawekeze kama wageni kwani watapata hasara gani? Kama mtu anataka kuja kuwekeza Tanzania milango ipo wazi na wanamsharti nafuu kweli kweli,

Ingawa sina matatizo na Uraia Pacha, lakini sikubaliani na sababu zinazotolewa eti tutafaidika kiuchumi na kifedha! Mtanzania mwenye nia bado atawekeza bila kujali status ya Uraia wake!
 
Mimi ambaye nimezaliwa Tanzania na ukoo wangu upo hapa tangu enzi na enzi eti leo nihitaji uraia wa nchi 2 kwa lipi? Kama nataka kwenda huko kwingine kwani ni lazima nibadilishe uraia?
Membe anawatetea wahuni ambao walishalowea ulaya na Marekani na hata hawanapesa za kuwekeza ila ni madalali ili nao waje wafanye udalali katika maliasili zetu. Kam waliikana Tanzania iweje leo waione ni nzuri na watake tuwarekebishie?Watu wenyewe hata milioni 1 hawafiki.

Ingawa sina matatizo na Uraia Pacha, lakini sikubaliani na sababu zinazotolewa eti tutafaidika kiuchumi na kifedha! Mtanzania mwenye nia bado atawekeza bila kujali status ya Uraia wake!
 
watanzania wa kawaida hawaitaji uraia wa nchi mbili..... wanaotaka uraia wa nchi mbili ni wahujumu uchumi mkubwa ili kikinuka apa aweze kukimbia nchi huwezi kuishi kama popo(wakishindwa ndege unakimbilia kwa wanyama wakishindwa wanyama unakimbilia kwa ndege)!!! kuna mtanzania gani anayezuiwa asilete misaada nyumban eti kwa sababu sio raia? kuna watu waliotummiza hapa tz kwa sababu ya urai wa nchi mbili kama kina jeetu patel ndie aliyefadhili mikataba ya ndege mbovu ya rais, rada mtumba kwa bei za kuruka hadi tukaonewa huruma na wabunge wa uingereza tukaambiwa tutakula nyasi ili ndege inunuliwe.... lakini kwa sababu ana uraia wa uingereza mpaka leo hajulikani alipo!!

Kuna Watanzania imebidi wachukue uraia wa nchi nyingine kwasababu ya kupata ajira za kitaalamu,kuoa/kuolewa nje na shughuli kubwa za biashara na uchumi! Hawa ni sahihi kupata uraia pacha. Issue ni lile kundi kubwa ambalo wamejiripua bila mwelekeo wa aina yoyote!
 
kuna watu wanaangalia leo tu hawaoni kesho wala kesho kutwa, ndiyo mana wanajiita mtanzania wa kawaida, mtanzania wa kawaida. Hivi anaye andika katiba ni Mtanzania wa kawaida? Pamoja na elimu yako bado unajiita mtu wa kawaida? sasa kwa nini umeenda shule? Waelimishe wale wasiyo jua.

Majirani zetu, Kenya, Rwanda na sehem zingine uraia wa nchi 2 imebaki kua historia. kama mtu ni muhalifu atakamatwa popote pale alipo. Kwa kagame ata kama mtu (mhalifu) atakimbilia Afrika kusini atamkamata tu.

Hapa Morogo wapo waSwahili ambao tunawaita wa Tanzania wa asili ya Asia hawa watu wana uraia wa nchi 2 nawanaishi vizuri tu. Mtu kama Mhe Abood akitaka kwenda kwao Oman anaenda na atapokelewa vizuri tu. Ndugu zake wa Oman wanafaidika nakuwepo kwake hapa. kuchi kuchi Otae ndo usiseme wanaenda India na kurudi bila shida wakiwa India ni wa Indi wakiwa TZ ni wa TZ. lakini kwetu hapa bado tumelala tunasubiri mpaka IMF iingilie kati. Marekani wameshasahau siku nyingi mjadala kama huo.

Ama kweli naamini kinacho tufanya kua masikini ni (lack of positive gatittude and good responsability na siyo ukosefu wa Ardhi au rasilimali).
 
Jamani watanzania tuamkeeee uraia wa nchi mbili ni bomu la nyuklia mmeona tulivyouziwa mbuzi kwenye gunia kuambiwa balali si mtania alishachukua uraiya wa nchi nyingine chondechonde watanzania tusikubali uraia wa nchi 2 hawa wameshashtukia mbeleni segerea inawaita wanakimbilia kuhodhi uraia wa nchi mbili kikinuka wakimbilie ughaibuni ili tushindwe kuwakamata chukueni mifano km ya akina alex masawe hatukawii kusikia mkulu nae si mtanzania ni mmarekani yetu macho.

Yaani una akili kama ya Nyerere, hawa jamaa ni madalali wa wazungu, haiwezekani tukubali hilo, wao tayari washanunuliwa na hivi tuna uraia wa nchi moja wanatuchakachua sasa tukiwa na na uraia Kikatiba si tutakwisha kabisa.
 
Uraia wa nchi mbili haujawahi kuwa suala katika nchi hii ambayo hata huo uthibitisho wa uraia kisheria haupo. Leo hii mtu akinitaka nimthibitishie pasipo shaka kuwa mimi ni Mtanzania sina namna zaid ya kukimwaga kiswahili na kuelekeza mitaa ya kijijini kwangu jambo ambalo wapo wageni wengi tu wanaoweza kulifanya. Aidha, nafahamu Watanzania wa kawaida wenye uraia wa nchi nyingine lakini wanaingia bongo na kuendeleza maisha yao kama kawaida bila bugdha. Inatia shaka sana iweje akina Membe wahangaike na hii kitu wakati huu badala ya kuimarisha utambulisho wa Mtanzania mzawa kwanza ndani ya nchi. Hebu tumalize utoaji wa vitambulisho vya Taifa ndipo tuanze kuulizana haya mengine.
 
Yanayosemwa hapo yote ni ya kufikirika na kwa manufaa binafsi. Yaani Mh. Membe anataka kutuamiisha kuwa watanzania walioko nje hawachangii Kama walivyo wakenya, waghana, wanijeria na pengine waethiopia kwa sababu ya kuto kuwa au kuruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili! Je nchi hizi zote zina ruhusa uraia wa nchi mbili? Si kweli.

Haya ni mawazo potofu na hasitudanganye. Mtu hawezi kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa sababu tu ana uraia wa Marekani na uraia wa Tanzania. Kama alikuwa Mtanzania, akashindwa kuchangia, atawezaje atakapokuwa Mmarekani. Ukweli ni kuwa watanzania walioko nje ni wachache na wengi hawana kazi za maana kulinganisha na mataifa yaliyotolewa Kama mfano.

Wenzetu wengine ni sera kabisa ukipata kazi nje unatoka na kuhakikisha unawasaidia wengine kutoka pia. Sisi hapa ni kinyume wenye elimu wako serikalini na hawataki/wanaogopa kutoka nje. Wanaofanikiwa kutoka hawataki kuwavuta wenzao! Matokeo yake watanzania wenye kazi za ujuzi nje ya nchi ni wachache kuweza kuchangia mapato Kama mifano iliyoyolewa. Ebu tujiulize, ufilipino ambayo kipato chake kikubwa cha fedha za kigeni kinatokana na wafanyakazi wa kazi za ndani nje ya nchi, je hao wafanyakazi wanakuwa na uraia wa nchi ingine zaidi ya uraia wa nchi Yao ya ufilipino?
 
Hakuna cha urai pacha wala nini, watanzania tunakosa uzalendo kwa nini tusijivunie utanzania wetu...Hii kitu hakuna kupitisha wewe kama unataka kua mwingereza kua mwingereza, kama unataka kua mchina kua mchina..sie tuachie Tanznaia yetu tunayoipenda kwa moyo wa dhati!! Wameshindwa kukuza uchumi wanasingiziaa eti ni kwa ajili hatuna urai pacha
Membe ni janga tu....
 
Back
Top Bottom