Membe ananikumbusha Kolimba

Membe katoa maoni yake kama raia wengine humu na huko mtaani. Acheni kucomplicate mambo, sijui TISS, Kolimba etc
 
Ukisikia Mayowe kutoka upande huo Ujue ameshatumbuliwa.....kwahiyo Mkuu usipoteze muda wako....
 
Hivi si wizara yake ilitapanya karibu billioni 174 na ushee kwa safari za nje ?? Anataka kutuaminisha nini Membe ??
Huyu jamaa nadhani bado kwenye akili yake Kikwete anatawala ,kumshauri tu he should choose his battles wisely ,Kikwete is no longer his backborne
 
Duh
Kwa kadiri nilivosoma story ya Kolimba kumbukumbu zinanieleza Kolimba alikufa kwa kupigwa risasi licha ya kunyoosha mikono juu kuashiria kuwa amesalenda!!

Hiki kisa chako kumuhusu ni kipya kwangu. . hilo tu

BACK TANGANYIKA
Duh,, Kolimba Au kombe mkuu
 
Lakini huyu aliwahi kunukuliwa kuwa '' Mawaziri wa JK walikuwa wanapishana angani kana kwamba kuna moto ardhini''
Kabadilika ? Au labda pengine hata yeye safari zake za nje alizotegemea zitalipiwa na serikali ya JPM zinapigwa stop..
Huwa unawaamini wana siasa?
 
Kwa wanaojua historia ya ccm watajua anayeongea sio Membe ni kundi la watu wakubwa ndani ya ccm kama yeye alivyo mkubwa hawezi tumwa na wadogo. Anayoyajua membe magufuli hayajui yako mengi nyuma ya pazia sasa kama yako mengi nyuma ya pasia ayajuayo membe bila magufuli kujua nini maana yake? hapo ndo tuna conclude uasi mkubwa umepangwa na wana ccm kwa serikali ya magufuli. Shame on you ccm. CCM ni chama kisichopenda kabisa maendeleo ya Tanzania yaani wanatamani wananchi wote wangekuwa mazezeta ili wawaongoze bila kupata criticism. Sasa bahati tumepata Magufuli angalau kidogo yuko tofauti tayari washaanza kumfanyia hujuma hata miezi 4 haijafika
 
Hapana mkuu respect wa boda, aliyekufa hivyo ni mzee Kombe na si Kolimba. Kolimba alifia Dom na Kombe alifia karibu na nyumbani kwake kwa kupigwa risasi ili mambo flani yasitirike.
Hapana mkuu respect wa boda, aliyekufa hivyo ni mzee Kombe na si Kolimba. Kolimba alifia Dom na Kombe alifia karibu na nyumbani kwake kwa kupigwa risasi ili mambo flani yasitirike.

Tuko pamoja mkuu,

Unajua ukiwa unatype huku unadaiwa kodi, watoto wanasumbua ada na wenyekibanda wanataka kodi zao haya ndo matokeo yake..!!!

Thanks mkuu Frediluu na wengine wote hapo juu

BACK TANGANYIKA
 
Kwa kadiri nilivosoma story ya Kolimba kumbukumbu zinanieleza Kolimba alikufa kwa kupigwa risasi licha ya kunyoosha mikono juu kuashiria kuwa amesalenda!!

Hiki kisa chako kumuhusu ni kipya kwangu. . hilo tu

BACK TANGANYIKA
mkuu respect wa boda aliyeuawa hivyo ni aliyewahi kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa Meja jenerali Imrani Kombe Sio Kolimba
 
Membe Ana uhuru na haki ya kushauri kile ambacho anakiona ni sahihi kwake na kwa serikali.. Tutambue na kujua kuwa Membe sio mtu mdogo katika nchi hii na hata kule kwenye Idara alikuwa ni jasusi ambaye alitegemewa hasa kwa ujuzi wake. Kwahiyo kama unachoongea ni mpango mkakati basi wajipange
 
Hizo ni hofu za mfa maji.mm najiuliza je, kama membe angeweza kuwa mgombea kiti hicho urais na akapata angeongea hivo?!shida ni kwamba wana ccm wengi walijua ccm ni ileile iliyokuwa imejaa uchafu na kunuka ufisadi na rushwa kutawala.lazima sasa watanzania wajue hii ni serikali ya ccm.na anayeiongoza hii serikali sasa ni mtu tofauti na huyo walokuwa wamemzoea.mambo yamebadilika nchi hii sasa inaendeshwa ki sheria na taratibu.aache kuchonga wa kukosa ni wa kukosa tuu,atunze heshima yke.
 
*Imran
 
ni aibu kubwa na kumtukana horace kolimba kumfananisha na membe. ni aibu kwa sisi tunaoijua siasa. membe si wa kumfananisha na kolimba. membe ni wa kumfananisha na akina nape, kibajaji n.k kolimba alikuwa ni mtu mwenye akili na uwezo wa kjenga hoja. sitak kumzungumzia membe. namzungumzia kolimba kidogo tu. huyu alikuwa na mwono, alikuwa na uongozi ndani yake. huwez mlinganisha na membe hata kidogo. umenitia kichefuchefu sana kwa kumlinganisha membe na kolimba huu ni ukosefu wa heshima kwa mzee wetu na mtu aliyekuwa makini kumlinganisha na watu wa hovyo hovyo.
 
Kila siku thread kuhusu magufuli.magufuli mwenyewe haijui jf
 

Hivi imekuwaje nguri wa diplomasia anazungumza na media badala ya kumfuata mwenzake ofisini na kumpa ushauri in camera!

Kinacho shangaza Mh.Membe na Dk.Magufuli wote waliwahi kuwa Mapandri watarajiwa miaka ya nyuma, sina shaka walijifunza ethics fulani ambazo wanapaswa kuwa nazo mpaka mwisho wa maisha yao - moja wapo ya ethics hizo ni jinsi ya kumshauri mwenzako kwa upendo mkiwa wawili bila ya ku-involve mtu wa tatu, unapo fikia hatua ya kuvishirikisha vyombo vya habari hapo sasa itadhirisha kuna kitu cha ziada si bure.

Watanzani wote wenye akili timamu bila kujali itikadi za vyama vyao, wanajua wazi wazi kwamba Mzalendo Magufuli ndiye alikuwa chaguo la Mungu kuongoza Taifa letu, sitanii - kumbuka alivyo ruka vihunzi vya chama chake kimihujiza hujiza ya Mungu,aliwekewa spana kila sehemu lakini wapi bwana kahibuka kidedea na kuwashangaza wengi,lilipo kuja suala la kura za Urais that too ilikuwa plain sailing!

Nataka nawakumbushe wana CCM kwamba uchaguzi umekwisha pita, wote tunawajibika kumu-support Dk.Magufuli sio vizuri kujaribu kumpiga vita vya kichini chini - inaonekana vikundi remnant ndani ya CHAMA viko well and kicking i.e havijafa, wasipo vivunja vitasababisha CHAMA kugawanyika vipande vipande.
 
Unataka kutuaminisha kwamba unajua kila mtanzania anayekufa amekufaje? Are every where that you know for sure causes of the dearth? Ukiona watu wanachangia humu elewa kwamba some have facts so usibishe bishe tuu na kusema watu ni masikini wa mawazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…