Membe ananikumbusha Kolimba

Mkuu kuna sheria ya cyber crime, unaifahamu vizuri lakini au unaropoka Jamii Forum?, ukiombwa utoe ushahidi wa maneno yako utakuwa tayari kutoa ushirikiano?. Sio Kila kifo kina mkono wa mtu, usipende sana kusikiliza stori za mitaani
Peleka mikwara yako huko ulipolalia , hivi Nchi hii kuna kitu kinaitwa ushahidi? Tokea lini ushahidi ukakubalika mbele ya mwenye pesa? Kombe aliuawa kwa kufananishwa na jambazi tena aliinua mikono juu akajitambulisha lakini bado alipigwa shaba, kama unataka Ushahidi nenda nyumbani kwa Nyerere kawaulize ndugu wa Nyerere watakupa picha A-Z . Kisha kautoe unapotaka wewe.
 
Membe ana hasira katumia pesa nyingi kumwingiza Magufuli ikulu lakini mpaka sasa hajapewa Dili lenye Ulaji ili arejeshe pesa zake.
 
Membe analilia Ulaji pia ana Machungu sana maana kaiteketeza pesa ya marehemu Gaddafi wa libya kwa ajili ya Magufuli alafu leo hajapewa cheo chochote kile ! Katumwa na wengine awasemee hayupo peke yake yupo na kundi lake wakiwemo akina January makamba na wenzao ambao hawana ubavu wa kuthubutu kusema yaliyopo mioyoni mwao.
 
Magufuli akiugua mafua .. membe umesababisha.. haaa
 
Kwa kadiri nilivosoma story ya Kolimba kumbukumbu zinanieleza Kolimba alikufa kwa kupigwa risasi licha ya kunyoosha mikono juu kuashiria kuwa amesalenda!!

Hiki kisa chako kumuhusu ni kipya kwangu. . hilo tu

BACK TANGANYIKA
 
Nina wasiwasi kama umemuelewa The boss.
 
frankly speaking,mleta mada huwa anawazaga mambo ambayo hayapo,basi tu ilucinations zako na poilitics za nyumbani;nimeona sana kwenye post zako nyingi.
Niseme tu,mimi sio fan wa Membe ila nathani kama mwanachama na raia yoyote watanzania anayo haki kuhoji baathi ya mambo sababbu anao uzoefu kwa miaka mingi.
Mimi nathani sidhani kama ni chuki juu ya Magufuli na serikali yake,ndio maana wanaita siasa.Siasa sio ngumi,kuchukiana,bali kupingana kwa hoja.
Zama za kale sio sawa na zama za muda huu.Kolimba kwaa taarifa yako,hakuuwawa na mkapa bali chama.Inasemekana alikuwa mbioni kutoa siri za chama na kuanzisha chama chake na kuchukua baathi ya watu ndani ya chama.Basically,kuua chama cha mapinduzi but who knows.Haya ni ya kusikia tu.
Hivyo,sioni ajabu sana Membe kusema lolote juu ya serikali ya Magufuli.Tusitake kukuuza maneno na mambo ambayo hayamo na kuleta uchochezi kwa mambo madogo sana kwenye jamiii.
Mkuu,wewe ni mtu ambaye nakuona uko so negative sijawahi kuona uko optimistic na kitu chochote.I wish to meet you in person to prove me.Stay positive brother kaka.
 
Parapanda litalia paraparanda litalia kwenda kumuona bwana Yesu Mawinguni,wangapi mpo nami tayari kwenda jamani
Nenda peke yako sisi bado tunayapenda maisha ya hapa duniani
 
Membe ni Nyoka wa TISS hawamuwezi.

Mkuu Nchi ina mambo mengi ,umesahau Brigedia Kombe aliyekuwa mkuu wa Kitengo wakati wa Nyerere,akaendelea wakati wa Mwinyi na kufanya na Mkapa akastaafu wakati wa mkapa. Yaliompata alishukiwa eti ameiba gari la Mhindi akamiminwa risasi na kundi la polisi huko Moshi-Arusha."usicheze na Government cheza na serikali"
 
Huy
Membe ni Nyoka wa TISS hawamuwezi.
Hiyo ni moja mkuu Savimbi. La pili hapo ni watanzania waache ujinga wa kuogopa kutoa mawazo yao eti kisa kuna aliyetoa wakamfanyizia kwa ule utaalam wao wa kuweka mambo flani kwenye mike au mambo kama haya. Mimi nakumbuka sana yaliyomkuta Jamaa yule, ila isiwekigezo cha kuwanyima watanzania wa leo kutoa maoni yao kwa kile kisa, No hata kidogo. Kama hoja ina nguvu basi na vigezo vizingatiwe na kama haina mashiko basi mhusika aeleweswhwe wapi kachemka na si KUMLINGANISHA NA MAREHEMU. Tunahisi bila kuthibitisha kuwa yule walimkolimba kiaina maana hata hakumaliza ile hoja yake ya ccm haina dira wala muelekeo, hawakumpa chance ya kuimaliza angalau watz tumuelewe alikua na maana gani. Sasa huyu wa sasa haimaanishi hajui yale mambo yao, najua anajua sana na labda anayo maana yake kusema aliyosema, so why the big boss na mlingano wako huu?? Au ndo unamfundisha uoga??? Kwani JPM ni Mungu asikosolewe??? Kwani unapokua kiongozi ndo unakua more perfect???? Oode mbe.. Kama yule walimkolimba, poa ila alisema kwa kinywa chake na wapo waliomuelewa sana tu, na huyu wakimmembe bado itakua poa tu maana kana watz weengi tu wamemuelewa na kifo chake kitakua changamoto zaidi kwa hali ya sasa.
 
Kwa kadiri nilivosoma story ya Kolimba kumbukumbu zinanieleza Kolimba alikufa kwa kupigwa risasi licha ya kunyoosha mikono juu kuashiria kuwa amesalenda!!

Hiki kisa chako kumuhusu ni kipya kwangu. . hilo tu

BACK TANGANYIKA

Hapana mkuu respect wa boda, aliyekufa hivyo ni mzee Kombe na si Kolimba. Kolimba alifia Dom na Kombe alifia karibu na nyumbani kwake kwa kupigwa risasi ili mambo flani yasitirike.
 
Kama utakataa kukosolewa katika maisha hutojifunza chochote coz no one is perfect

Huu ujumbe unatakiwa umkute JPM direct bila kupitia popote, maana kuna watu wanamwona tayari kama malaika ama Mungu wao kabisa.
 
Mimi sijawahi kukuona siwezi kukupiga mikwara, nakukumbusha tu hali halisi ya sasa. Watanzania tunabakia kuamini sababu za ziada za vifo, hata siku moja mtanzania hafi kifo cha kawaida lazima kuna hadithi ndefu nyuma ya kifo chake. Huu unaitwa umasikini wa mawazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…