Membe: Ama zao ama zetu waliohusika rada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: Ama zao ama zetu waliohusika rada

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Feb 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  Membe: Ama zao ama zetu waliohusika rada [​IMG] Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati), akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (kulia), na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge nje ya ukumbi Bunge Dodoma jana.
  Salim Said
  SAKATA la kashfa ya ununuzi wa rada ya kijeshi nchini, limeingia katika sura mpya baada ya serikali kuahidi lazima iwashughulikie watuhumiwa wote waliohusika katika kashfa hiyo, ili kulinda heshma ya nchi katika sura ya kimataifa.

  Hivi karibuni kampuni ya BAE Systems inayodaiwa kumlipa dalali zaidi ya Sh12 bilioni kwa kufanikisha kwake serikali ya Tanzania kununua rada ya kijeshi ya Plessey Commander Fighter Control System kwa Sh 40 bilioni, imekiri makosa na kuahidi kurudisha fedha kwa serikali ya Tanzania.

  Wiki iliyopita BAE System ilikiri kufanya makosa kwa kulipa rushwa katika mkataba wa kuiuzia serikali ya Tanzania rada hiyo ya kijeshi, chini ya Sheria ya Mikataba ya Makampuni ya mwaka 1985.

  Akizungumza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC), mjini Dodoma jana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema lazima serikali isafishe wale wote waliohusika na kashfa hiyo kwa kulinda heshma ya nchi.

  Alisema kashfa ya sakata la rada imefikia katika ukingo wake, baada ya BAE System kukiri makosa na kukubali kujisafisha kutokana na makosa hayo.

  "BAE imejisafisha, imekiri makosa na imekubali kujisafisha na ule ndio uaminifu, wanakwenda wanafanya uchunguzi, wanagundua udhaifu, wanakiri makosa na wanajisafisha," alisema Membe.

  Membe alifafanua kuwa baada ya BAE System kukubali kujisafisha kwa kuirudishia Tanzania "chenji" yake, kazi kubwa iliyobaki ni kwa serikali kuhakikisha inawashughulikia wahusika.

  Alisema, "…..lakini la pili ambalo sihitaji ushauri wala utaalamu kulisemea, ni kwamba safari hii ya sakata la rada imefikia ukingoni, wenzetu wameshajisafisha na sisi hatuna budi kujisafisha katika sura ya dunia,".

  "Kwa hiyo sasa shughuli ni kwetu sisi, mimi nina uhakika kabisa zile nchi zilizoguswa na kashfa hii zitachukuliwa kutoka pale, ili zisafishwe na sisi Watanzania sasa lazima tujiweke sawa tujisafishe katika sura ya kimataifa, yaani katika ngazi ya kimataifa ya nchi zinazoheshimika katika utawala bora," alisisitiza Membe.

  Membe alifafanua kuwa, "Lazima tulifikishe suala hili katika hitimisho lake, yani lazima tujisafishe, tukae vizuri ili tuonekane kwamba mashimo yote ya rushwa yamefukiwa na kama kuna mtu yeyote amehusika katika kashfa hii, hiki ndicho kipindi ambacho, utawala bora wa Tanzania unatakiwa kuimarishwa."

  Membe alisistiza kuwa suala la rada nchini halitopita hivihivi bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria ili Tanzania ijionyeshe katika sura ya dunia kwamba inawajibika.

  "Suala hili halitoisha hivihivi kwa sababu tumesemwa sana na lazima tujionyeshe katika serikali za dunia na katika uhusiano wa kimataifa kwamba na sisi tuko 'responsive' (tunawajibika) kwa maana tunajibu mapigo," alisema Membe na kusisitiza;

  "Kama hili limetokea na tumepata ushahidi, lazima tusafishane humu ndani kwa heshima ya nchi,".

  Juzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Sofia Simba alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hadi sasa hakuna taarifa rasmi ambayo serikali imepokea kuhusu sakata la kashfa ya rada, isipokuwa wamekuwa wakisoma katika magazeti na katika mitandao ya kimataifa.

  Hata hivyo, aliahidi kuwa, watakaohusika katika kashfa hiyo watachukuliwa hatua za kisheria.

  Katika moja ya ziara zake nchini Uingereza, Rais Jakaya Kikwete aliambia Serikali ya Wingereza kwamba kama kuna fedha imezidi katika ununuzi wa rada anaomba chenji yao.

  Membe alisema jana kuwa, hatimaye sasa chenji hiyo inarudi na kwa maana hiyo Tanzania imeula kwa kurudishiwa fedha hiyo takribani paundi 28 milioni kwani miradi mingi itafanikiwa.

  "Tanzania tumeula na tunasema Alhamdulillaahi, nilisema na narudia tena kwa vile tunarudishiwa chenji yetu tumeula, miradi yetu itakwenda vizuri, kilimo kwanza kitakwenda vizuri, elimu yetu itakwenda vizuri na masuala mengine yatakwenda vizuri,"alisema Membe.

  Wanaotuhumiwa na kashfa ya rada ni Mwanasheria Mkuu wa wakati huo Andrew Chenge, Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Dk Idrisa Rashid na dalali mwenye asili ya Asia, Saileth Vithlani.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni mtu alioongoza wanaharakati katika kufichua sakata la ununuzi wa rada na ndege ya rais tangu wakati wa rais Mkapa, alisema anashangazwa na kigugumizi cha serikali kuchangamkia fedha hizo.

  "Nastaajabu sana ufisadi ndani ya nchi hii, nyinyi mmetapeliwa na taarifa zimo katika vyombo vya habari vya uhakika, lakini waziri anaulizwa anasema serikali haijapata taarifa rasmi, si ufuatilie," alihoji Lipumba.

  Alisema kigugumizi cha serikali kwenda kudai fedha hizo kinakuwapo kwa sababu, waliohusika na kashfa hiyo wapo madarakani na hivyo wanaogopa kuwajibika.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17859
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  RICHMOND, KIWIRA KUWASILISHWA LEO

  [​IMG]
  Bunge la Tanzania.​

  Leo Bunge litapokea taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu zabuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, mgodi wa makaa ya Mawe wa Kiwira na hoja binafsi ya kiongozi wa kambi ya upinzania bungeni, Hamad Rashid Mohamed...

  Hoja ya Mohamed ni kutaka Bunge la Jamhuri liunge mkono Baraza la Wawakilishi lililoridhia kupigwa kwa kura za maoni kwa ajili ya kuunda Serikali ya mseto Zanzibar pamoja na kuwapongeza Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuonyesha nia ya kumaliza mpasuko wa kisiasa visiwani humo.

  Naibu Spika, Anne Makinda, aliwaambia waandishi wa habari katika viwanja vya bunge jana jioni kuwa iwapo mjadala wa maazimio hayo utamalizika asubuhi, atawasiliana na Kamati ya Bunge ya Miundombinu ili kuona kama taarifa ya kampuni ya kupakua na kupakia makontena katika bandari ya Dar es Salaam (Ticts) na ya kampuni ya Rites ziko tayari kuwasilishwa.

  Alisema kukwama kuwasilishwa kwa taarifa za Ticts na Rites kunatokana na kwamba kamati ya Miundombinu haikuwa imekamilisha kazi ya kuzipitia.

  Ratiba ya Bunge imekuwa ikibadilika kila mara jambo linalosababisha utaratibu wa vikao vya Bunge kutoeleweka.

  Jana asubuhi ratiba iliyokuwa imetolewa na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, ilionyesha kuwa baada ya kipindi cha maswali na majibu, Bunge lingepokea na kujadili taarifa ya athari za mazingira za mgodi wa North Mara.

  Ghafla, ratiba ilibadilika na Dk. Kashilillah alitoa taarifa kuwa Bunge lingepokea na kujadili taarifa za Rites na Ticts jambo ambalo hata hivyo halikutekelezwa.

  Katika hali ya kushangaza, kikao cha jioni ambacho kingepokea taarifa hizo kilikaa kwa takribani dakika moja tu baada ya Makinda kutangaza kuahirisha kikao hicho kutokana na kutokamilika kwa taarifa hizo.

  Kabla hata hajakaa Makinda alisema: “Waheshimiwa wabunge taarifa za Ticts na Rites hazijakamilika kwa hiyo natangaza kuliahirisha Bunge hadi kesho (leo) saa 3:00 asubuhi.”

  Alipohojiwa kuhusiana na hali hiyo, mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, alisikitishwa na kitendo hicho na kueleza kuwa hayo ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

  “Wabunge wanakula posho bila kufanyakazi…haya ni matumizi mabaya sana ya fedha za wananchi masikini, inasikitisha sana na haipendezi,” alisema.

  Dk. Slaa ambaye pia ni mmoja kati ya wajumbe katika Kamati ya Bunge ya Uongozi ambayo ndiyo yenye jukumu la kupanga ratiba, alisema: “Binafsi sielewi kinachoendelea.”

  CHANZO: NIPASHE
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  Mjadala wa sakata hilo unatarajiwa kuwa wa moto hasa baada ya serikali kukwepa kuwasilisha utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge yaliyotokana na mjadala baada ya ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na kamati teule kubaini mapungufu mengi katika utoaji wa zabuni hiyo mwaka 2006.

  Serikali imekuwa ikipiga ngonjera kuhusu kuwasilisha ripoti hiyo na takriban mikutano mitatu ya Bunge imeshindwa kupokea ripoti hiyo kutokana na serikali kupiga chenga ya mwili.

  Januari 28 mwaka huu, Spika Samuel Sitta alilazimika kuwatoa hofu wabunge alipoahidi kuwa safari hii suala hilo lazima liwasilishwe na kujadiliwa.

  Katika mkutano uliopita kulikuwa na ahadi kama hizo kuwa suala hilo lingejadiliwa, lakini ikatangazwa baadaye kuwa kashfa ya Richmond haitajadiliwa na Spika Sitta alieleza kuwa kutojadiliwa huko kulitokana na kupunguzwa muda wa mkutano huo kulikosababishwa na mtikisiko wa kiuchumi.

  Hata hivyo, kabla ya suala hilo kuzimwa serikali iliwahi kulipiga sarakasi mara kadhaa wakati wa vikao vya kamati za Bunge ambako pia serikali haikuwasilisha taarifa yake baada ya Waziri wa Nishati na Madini kueleza kuwa wamekubaliana na wajumbe wa kamati ya sekta hiyo kuwa ripoti hiyo isomwe Dodoma, ambako pia haikusomwa.

  Kwa mujibu wa ratiba mpya ya vikao vinavyoendelea vya mkutano wa 18 wa Bunge iliyotolewa jana, taarifa ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni ya Richmond, imewekwa siku ya mwisho kabisa.

  Ratiba hiyo pia imeonyesha kuwa siku hiyo hiyo, mhimili huo wa dola utapokea taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu kashfa hiyo iliyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

  Aidha katika siku hiyo ya mwisho ya mkutano wa 18 wa Bunge chombo hicho pia kitapokea taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini juu ya taarifa ya serikali kuhusu ubinafsishwaji wa Mgodi wa Kiwira. Ripoti hiyo itawasilishwa na kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed.

  Leo bunge litapokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu taarifa ya serikali ya utekelezaji wa azimio la Bunge kuhusu kushughulikia utendaji mbovu wa kazi kwenye kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binafsi ya Ticts.

  Ticts iliingia mkataba unaoipa ukiritimba wa kuendesha kitengo hicho kwa miaka 15 na baadaye kuongezewa miaka 10 hata kabla ya kukamilisha mkataba wa awali, mambo ambayo yalipingwa na Bunge.

  Pia litajadili taarifa ya serikali ya utekelezaji wa azimio la Bunge kuhusu uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli (TRL), kampuni ambayo sehemu kubwa ya hisa zake inamilikiwa na RITES ya India .

  Kwa mujibu wa ratiba mpya serikali pia itapokea taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu athari za mazingira katika mgodi wa North Mara na pia litapokea taarifa ya kamati hiyo kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu Loliondo.

  Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kesho baada ya kipindi cha maswali na majibu wabunge watafanya uchaguzi wa wawakilishi wake katika vyuo mbalimbali na baadaye siku hiyo Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi wa Mwaka 2009.

  Alhamisi serikali itawasilisha muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa mwaka 2009, muswada wa sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa wa Mwaka 2009 ambao awali ulikataliwa na wabunge wakitaka ufanyiwe marekebisho.

  CHANZO: MWANANCHI
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  RICHMOND, KIWIRA KUWASILISHWA LEO

  [​IMG] Hoja ya Mohamed ni kutaka Bunge la Jamhuri liunge mkono Baraza la Wawakilishi lililoridhia kupigwa kwa kura za maoni kwa ajili ya kuunda Serikali ya mseto Zanzibar pamoja na kuwapongeza Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuonyesha nia ya kumaliza mpasuko wa kisiasa visiwani humo.

  Naibu Spika, Anne Makinda, aliwaambia waandishi wa habari katika viwanja vya bunge jana jioni kuwa iwapo mjadala wa maazimio hayo utamalizika asubuhi, atawasiliana na Kamati ya Bunge ya Miundombinu ili kuona kama taarifa ya kampuni ya kupakua na kupakia makontena katika bandari ya Dar es Salaam (Ticts) na ya kampuni ya Rites ziko tayari kuwasilishwa.

  Alisema kukwama kuwasilishwa kwa taarifa za Ticts na Rites kunatokana na kwamba kamati ya Miundombinu haikuwa imekamilisha kazi ya kuzipitia.

  Ratiba ya Bunge imekuwa ikibadilika kila mara jambo linalosababisha utaratibu wa vikao vya Bunge kutoeleweka.

  Jana asubuhi ratiba iliyokuwa imetolewa na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, ilionyesha kuwa baada ya kipindi cha maswali na majibu, Bunge lingepokea na kujadili taarifa ya athari za mazingira za mgodi wa North Mara.

  Ghafla, ratiba ilibadilika na Dk. Kashilillah alitoa taarifa kuwa Bunge lingepokea na kujadili taarifa za Rites na Ticts jambo ambalo hata hivyo halikutekelezwa.

  Katika hali ya kushangaza, kikao cha jioni ambacho kingepokea taarifa hizo kilikaa kwa takribani dakika moja tu baada ya Makinda kutangaza kuahirisha kikao hicho kutokana na kutokamilika kwa taarifa hizo.

  Kabla hata hajakaa Makinda alisema: “Waheshimiwa wabunge taarifa za Ticts na Rites hazijakamilika kwa hiyo natangaza kuliahirisha Bunge hadi kesho (leo) saa 3:00 asubuhi.”

  Alipohojiwa kuhusiana na hali hiyo, mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, alisikitishwa na kitendo hicho na kueleza kuwa hayo ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

  “Wabunge wanakula posho bila kufanyakazi…haya ni matumizi mabaya sana ya fedha za wananchi masikini, inasikitisha sana na haipendezi,” alisema.

  Dk. Slaa ambaye pia ni mmoja kati ya wajumbe katika Kamati ya Bunge ya Uongozi ambayo ndiyo yenye jukumu la kupanga ratiba, alisema: “Binafsi sielewi kinachoendelea.”

  CHANZO: NIPASHE
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  RICHMOND YAPANGWA SIKU YA MWISHO BUNGENI

  [​IMG] Mjadala wa sakata hilo unatarajiwa kuwa wa moto hasa baada ya serikali kukwepa kuwasilisha utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge yaliyotokana na mjadala baada ya ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na kamati teule kubaini mapungufu mengi katika utoaji wa zabuni hiyo mwaka 2006.

  Serikali imekuwa ikipiga ngonjera kuhusu kuwasilisha ripoti hiyo na takriban mikutano mitatu ya Bunge imeshindwa kupokea ripoti hiyo kutokana na serikali kupiga chenga ya mwili.

  Januari 28 mwaka huu, Spika Samuel Sitta alilazimika kuwatoa hofu wabunge alipoahidi kuwa safari hii suala hilo lazima liwasilishwe na kujadiliwa.

  Katika mkutano uliopita kulikuwa na ahadi kama hizo kuwa suala hilo lingejadiliwa, lakini ikatangazwa baadaye kuwa kashfa ya Richmond haitajadiliwa na Spika Sitta alieleza kuwa kutojadiliwa huko kulitokana na kupunguzwa muda wa mkutano huo kulikosababishwa na mtikisiko wa kiuchumi.

  Hata hivyo, kabla ya suala hilo kuzimwa serikali iliwahi kulipiga sarakasi mara kadhaa wakati wa vikao vya kamati za Bunge ambako pia serikali haikuwasilisha taarifa yake baada ya Waziri wa Nishati na Madini kueleza kuwa wamekubaliana na wajumbe wa kamati ya sekta hiyo kuwa ripoti hiyo isomwe Dodoma, ambako pia haikusomwa.

  Kwa mujibu wa ratiba mpya ya vikao vinavyoendelea vya mkutano wa 18 wa Bunge iliyotolewa jana, taarifa ya utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni ya Richmond, imewekwa siku ya mwisho kabisa.

  Ratiba hiyo pia imeonyesha kuwa siku hiyo hiyo, mhimili huo wa dola utapokea taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge kuhusu kashfa hiyo iliyosababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

  Aidha katika siku hiyo ya mwisho ya mkutano wa 18 wa Bunge chombo hicho pia kitapokea taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini juu ya taarifa ya serikali kuhusu ubinafsishwaji wa Mgodi wa Kiwira. Ripoti hiyo itawasilishwa na kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed.

  Leo bunge litapokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu taarifa ya serikali ya utekelezaji wa azimio la Bunge kuhusu kushughulikia utendaji mbovu wa kazi kwenye kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binafsi ya Ticts.

  Ticts iliingia mkataba unaoipa ukiritimba wa kuendesha kitengo hicho kwa miaka 15 na baadaye kuongezewa miaka 10 hata kabla ya kukamilisha mkataba wa awali, mambo ambayo yalipingwa na Bunge.

  Pia litajadili taarifa ya serikali ya utekelezaji wa azimio la Bunge kuhusu uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli (TRL), kampuni ambayo sehemu kubwa ya hisa zake inamilikiwa na RITES ya India .

  Kwa mujibu wa ratiba mpya serikali pia itapokea taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu athari za mazingira katika mgodi wa North Mara na pia litapokea taarifa ya kamati hiyo kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu Loliondo.

  Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kesho baada ya kipindi cha maswali na majibu wabunge watafanya uchaguzi wa wawakilishi wake katika vyuo mbalimbali na baadaye siku hiyo Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi wa Mwaka 2009.

  Alhamisi serikali itawasilisha muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi wa mwaka 2009, muswada wa sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa wa Mwaka 2009 ambao awali ulikataliwa na wabunge wakitaka ufanyiwe marekebisho.

  CHANZO: MWANANCHI
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,914
  Trophy Points: 280
  MMWANASIASA KIJANA APASUA JIPU LA MJADALA WA RICHMOND

  --- [​IMG] Kamati umeshatangaza kwamba imeshaliza kazi yake, Bunge nalo litangaze kufunga huo mjadala kwa bunge zima badala yake sasa ufuatiliaji uachwe kwa kamati za kisekta. Kwa hiyo sasa ripoti za utekelezaji zitapelekwa kwenye kamati za kisekta kwa kuwa kamati husika imesharidhika mpaka sasa kwa utekelezaji ambao serikali imefanya mpaka sasa.

  Wakati Kamati ikiyasema hayo inasema kuhusu Kiwira kuwa inaendelea kumshauri CAG afanye ukaguzi kuhusu bilioni 17 zilizoingizwa na serikali kwenye kiwira .(Tujiulize, muda gani agizo hili lilitoka? Kwanini mpaka sasa ukaguzi haujafanyika). Kwa maneno mengine, baada ya serikali kuamua kuuchukua upya mgodi, tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka za kina Mkapa, Yona na wenzao sasa sinaelekea kufunikwa kwa nguvu zote.

  Usanii mkubwa zaidi unajidhihirisha kwenye sakata zima la Richmond, ambayo mitambo yake dada ya Dowans ipo mpaka sasa hapa jimboni ubungo. Zikitafutwa kila namna za kuingiza mitambo husika kwenye mkondo wa kuhudumia na kulipwa na serikali ya Tanzania.

  Kamati inakiri kwamba ni kweli kuna double payment kwenye ulipwaji wa dola milioni tatu kwa kampuni ya Dowans, kamati inasema tu kwamba inaishauri serikali hizo fedha zirudishwe. (Toka kwa kampuni ya Dowans- ambayo kama ilivyo kwa Richmond inaonyesha kwamba ni kampuni hewa, uhalali wa usajili wake una mushkeli mkubwa). Kamati inatamka kwamba watendaji husika mamlaka zao za kinidhamu zimeona hawana hatia. Kamati inasema viongozi wa kisiasa wakina Msabaha, Karamagi nk uchunguzi wa ndani kuhusu ushiriki wao kwa ajili ya kuwajibishwa umeshakamilika, lakini sasa serikali imeanza uchunguzi wa nje wa kimataifa unaendelea. Kamati inatamka kwamba sasa suala hili likikamilika lipelekwa kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Usalama( Sasa sio Bungeni tena). Ajabu sana! Suala hili lilianza mwaka 2007; maazimio ya Bunge ni kujiuzulu kwa Lowassa ilikuwa 2008; mpaka leo uchunguzi unaendelea.

  Kituko kikubwa zaidi ni hitimisho la Kamati, kwamba kuhusu kumwajibisha Mkurugenzi wa TAKUKURU Hosea kwa TAKUKURU(Wakati huo TAKURU) kuisafisha Richmond; kwamba kamati haiwezi kulizungumzia tena suala hilo na wala haitarajii bunge ilizungumzie kwa kuwa Hosea naye anawachunguza wa bunge(rejea tuhuma kuhusu posho mbili). Hivyo kamati inasema suala hili sasa inaachiwa mamlaka ya juu zaidi(Soma Rais Kikwete). Ningeweza kuchambua azimio moja baada ya lingine katika ya maazimio 13 ambayo yalibaki kabla ya 23 (Hata yale 10 mengine yalikuwa mchanga wa macho).

  Lakini yatosha kusema kwamba suala hili ni ishara kwamba sasa makundi ndani ya CCM (lile linalojiita la wapambanaji dhidi ya ufisadi na lile linaloitwa la mafisadi) yanakaribiana kufunika tofauti zao kwa maslahi ya chama chao na utawala wao tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2010 ama pengine huo ndio uzalendo?. Inaonyesha kamati ya chama (party caucus) imefanya kazi yake kwa kile kinachoitwa ‘kuchukua maamuzi magumu (soma mabovu/bomu). !. Hii inaweza kutoa ishara kuhusu nini kitatokea kwenye ripoti ya Kamati ya Mwinyi na mwelekeo wa chama hicho tawala kwa ujumla. Haya ni madhara ya kuwa na hodhi (dominance/monopoly) ya chama kimoja bungeni.

  Hii ni changamoto kwa umma tunapoelekea katika uchaguzi mkuu. Tukumbuke maneno ambayo CHADEMA tuliyasema mwaka 2005; Kwamba mabadiliko ya kweli katika taifa letu, hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale kwa Ari, nguvu na Kasi mpya. Kwa falsafa ya chukua chako mapema(ccm), Tanzania yenye neema haiwezekani. Tuunganishe nguvu ya umma kuchagua viongozi mbadala wenye dira na uadilifu tuweze kujenga taifa lenye uwajibikaji kwa kubadili mfumo wa utawala; mabadiliko ya kweli yanawezekana. Tuwe wakala wa mabadiliko tunayotaka kuyaona; Mwenyezi Mungu atuwezeshe kufika salama.

  ZAIDI MTEMBELEE HAPA:http://mnyika.blogspot.com
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,961
  Likes Received: 9,612
  Trophy Points: 280
  Hivi kukubali makosa ndio "kujisafisha"?
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,387
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Kikwete na serikali ya kisanii na kishkaji!!!atampa wakati mgumu sana pres ajaye....itabidi asafishe mnooo....uozo wote wa mtandao!!
   
 9. M

  Mchili JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hizi porojo za tut... tuta zitaisha lini? Hatuoni aibu serikali ya Uingereza inatuonea huruma kwa umaskini wetu na sisi tunalindana tu. Mkuu wa nchi anatembeza bakuli la kuomba wakati mabilioni yetu halali yako mikononi mwa watu. Hata wenyewe watakua wanatushangaa kama Membe alivyosema tumechafuka sana kimataifa.
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,116
  Likes Received: 2,413
  Trophy Points: 280
  Yamewashinda ya Richmond, itakuwa haya?

  Btw, yule jamaa wa Richmond kufikiswa mahakamani jana na ishu za Richmond kuhitimishwa bungeni, is it really just a mare concidence?
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,936
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Jamani hatuna serikali kabisaa, yaani vitu vipo dhahiri kabisaaa lkn mtu anapeta tu mtaani, na nyadhifa kibao serikalini.Hizo za Membe ni porojo tuu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.

Loading...